Mzalendo39
JF-Expert Member
- Apr 17, 2015
- 882
- 1,029
Hivi karibuni Serikali ya awamu ya sita imetangaza kuwepo kwa mlipuko wa Corona na kuuarifu umma kuchukua taahadhari ya kujikinga na ugonjwa.
Kinachoshangaza serikari hiyo hiyo inayotangaza kuchukua tahadhari dhidi ya Corona ndiyo inayoongoza kuvunja Taratibu za kujikinga na Corona kwa kuruhusu mikusanyiko.
Mfano:
1. Rais Samia alimpigia Simu Nandy simu akiwa Dodoma kwenye #Nandyfestival ilihali akujua kuwa mkusanyiko huo ni kichocheo cha kusambaa virusi vinavyosababisha #Corona
2. Huko Mtwara jana wamehitimisha Michezo ya #umitashumita na viongozi wakuu wa serikali wakahudhuria na katika video inaonesha uwanja ukiwa umefurika kupita kiasi.
3. Maonyesho ya sabasaba# Unawezaje ukatangaza uwepo wa mlipuko wa Corona na ukaruhusu maonyesho yanayoendelea ya sabasaba.
4. Mechi ya simba na yanga ilitakiwa leo mechi ya simba na yanga ichezwe bila mashabiki kutoka na mlipuko wa wimbi la tatu la Corona, lakini bado Serikali hiyo hiyo inaruhusu mashabiki kuingia uwanjan
5. Kumbi za starehe Ukitembea kwenye majiji makubwa ambayo ni #Dar es salaam #Mwanza #Arusha #Dodoma msongamano ni mkubwa mno kwenye kumbi za starehe, lakini bado Serikali inashindwa kuchukua hatua na tahadhari ya kupambana na Covid licha ya kiongozi mkubwa wa nchi kutangaza
Nchi jirani na Tanzania tayari nimechukua hatua ya kujikinga na ugonjwa huu kwa
1. Kudhibiti mikusanyiko
2. Kufunga mashule
3. Kufunga Mabaa
4. Kudhibiti watu(lockdown) kwa mchana na usiku
Serikali yangu ya Tanzania imekuwa ikijivuta kama jongoo/Konokono katika kushughulikia na kudhibiti janga hili la Corona. Serikali kama haiwezi kupambana na ugonjwa huu iachie wananchi uhuru kama ilivyokuwa kwa #Mwendazake kuliko kutangaza ugonjwa covid upo na hatua zinachukuliwa kujikinga sifuri.