Mzalendo2015
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 6,710
- 9,063
Wana JF na Watz wote,
Ukweli lazima usemwe ili kuweka bayana ya kile kinachoendelea kuhusu mgogoro wa Makinikia na wezi wa Dhahabu yetu kati ya Wabunge wa CCM na wale wa UKAWA.
Inasikitisha kuwa Serikali ya JPM na Wabunge wa CCM hivi sasa wanajaribu kuwashambulia Wabunge wa Upinzani kuwa ndio wanaotetea wezi wa Madini na Raslimali za nchi yetu ilhali ukweli ni kinyume chake. Nina hoja zifuatazo zenye kuthibitisha hilo:

- Mikataba na sheria zote za wawekezaji wa Madini zililetwa Bungeni kwa HATI YA DHARURA na kupitishwa na CCM kwa uwingi wao wa KURA za NDIYOOOOOOOOOOOOOOOO!
- Kamati ya Osoro imetaja Mawaziri wastahafu na waliop kazini, Wanasheria Wakuu, Makamishina na Wasaidizi wao wote kutoka Serikali ya CCM hakuna mpinzani hata 1.
- Rais Magufuli naye ameendelea kutetea wezi wa Dhahabu na Makinikia kwa kuwakingia kifua Marais waliopita Mkapa na Kikwete kwa kuzuia media zisiwaguse ati walifanya kazi nzuri sana.
- Rais ameonyesha udhaifu mkubwa kwa kujaribu kuwalinda na kuwatetea Viongozi ambao walihusika kwa njia moja au nyingine katika kuingia Mikataba hii ya kinyonyaji.
- Haingii akilini hata kidogo kusema Waziri wa Madini, Mwanasheria Mkuu na Kamishina wa Madini ndio walihusika na Mikataba mibovu ya Madini lakini Rais hahusiki. Miswada yote ya Sheria zilizopelekwa Bungeni kwa Hati ya Dharura haziwezi kuwa sheria mpaka RAIS AWE AMESAINI.Hivo sheria zote zinazotumika kwenye Mikataba hii zina signature za Marais hawa.
- Wabunge wote waliosimama Bungeni vipindi hivo kupinga au kuhoji Mikataba na Sheria hizombovu waliishia KUFUKUZWA BUNGENI wakiwemo Tundu Lissu, Zitto Kabwe, John Mnyika na wengineo.
- Anachofanya Rais Magufuli kwa sasaa ni kuwalaghai Watz kuwa anatetea Madini lakini kiuhalisia siyo kweli. Huwezi kumshtaki Waziri, Kamishina au Mwanasheria wakti alifanya hivo kwa maelekezo ya Mkuu wa nchi.
- Kinachotakiwa sasa ni CCM na Serikali yao wakiri Makosa, watubu na waombe msamaha kwa Watanzania na waungane na UKAWA kuanza kuboresha sheria ya Madini.