Tumesalitiwa na waandishi wa habari na vyama vya siasa na akili zetu wamezichezea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumesalitiwa na waandishi wa habari na vyama vya siasa na akili zetu wamezichezea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Waberoya, Oct 20, 2011.

 1. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #1
  Oct 20, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280

  Yule mtu anayejulikana na kuandikwa ni mwizi aliwaita wale wasio wezi nyumbani kwake na kula chakula chake!!!! Ili ni tusi lingine kwa waandishi wa habari. Aidha kwa kujua au kutokujua. Wengi waliuliza swala la Richmond nd Dowans tangu mwaka 2008…mpaka leo eti hawa waandishi hawana majibu hawajui….ila kila siku wanaandika. Eti kuthibitisha ukweli wa habari zao ni mpaka wamuulize muhusika!!!! Salaaaale! Kuwa iko siku mwizi atasema ya ‘moyoni' mwizi huyu lazima ni wa tofauti sana hapa ninajaribu kuwaza


  Haya ni baadhi ya maswali ambayo utawakuta baadhi ya watanzania wenzetu ama kwa kukosa akili, au ujinga au upumbavu huwa wanauliza na kujiuliza kuhusu Lowassa na utakuta maneno haya yamo sana kwenye nakala nyingi sana za magazeti ya kitanzania..kuwa eti;


  1. Lowassa atubu dhambi zake na kukiri tutamsamehe tu

  2. Lowassa aombe msamaha tu na yataisha

  3. Lowassa anataka kuwa rais 2015

  4. Lowassa ni fisadi lazima ajibu maswali yakuhusu Dowans na Richmond

  5. Lowassa ajivue gamba

  6. Lowassa …etc


  DPP na timu yake mpaka leo wamekaa kimya na hakuna chochote kilichofanyika cha kuuthibitishia umma kuwa Lowassa ni mwizi, ila umma wote unajua kuwa Lowassa ni mwizi. Na adhabu za JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NI KUNYOOSHA VIDOLE NA kusema yule mwizi.. huyu fisadi ukisema tu haya maneno ni kama vile…FEDHA INARUDISHWA!na kwa sababu SERIKALI HAIJAWEZA KUWACHUKULIA HATUA WALE WEZI BASI WENYE MAKOSA NI watuhumiwa…na hawa waliopaswa kuwaweka lupango hawa wezi wako huru na wanafanya kazi sana!!!.

  Tanzania ikimpata mwizi ambaye hana mshipa wa aibu, asiyejali na ambaye ata-avoid kusoma magazeti basi mwizi huyu ataishi na kudumu bila wasiwasi.
  Magereza ni sehemu ya wale wezi wasioandikwa magazetini.mahakamani ni sehemu ambazo wanaotakiwa kushtakiwa ni wale tu ambao wanatakiwa kwenda gerezani.washtakiwa wasioenda gerezani wote wataandikwa sana ili magazeti yauze.

  Watanzania nilichoandika hapo juu ni usaliti unaofanywa na vyombo vya habari Tanzania, vyombo ambavyo vinatakiwa kulilinda taifa hili. Ni vyombo vilivaa umimi, ubinafsi, makundi na ni vyombo ambavyo vinapumbaza na kudumaza bongo za watanzania wengi.Waandishi wa habari hawa ndio waliomweka Kikwete na Lowassa madarakani, ni watanzania wenzetu hawa ambao wako tayari kuandika maswali na maoni ya kipuuzi na kuruhusu nakala ambazo ukisoma unapata kujua na kung'amua kuwa watanzania wenzetu wanaumwa.


  Hawa waandishi wamekubali kuitwa na fisadi, kawaita kwake nyumbani…hao hao wanaandika Lowasa kafunguka , ila hajasema lolote kuhusu Richmond. NAJIULIZA LOWASA MNATAKA ASEME NINI WAKATI NYIE WAANDISHI MMEUAMINISHA UMMA WA WATANZANIA KUWA LOWASSA NI FISADI!! najiuliza hivi?.

  Au:

  1. Wakati mnaandika kuwa EL mWIZI hamkuwa na uhakika na mnataka awahakikishie

  2. Mnajua ukweli muhusika wa Dowans ni nani na mnataka Lowassa aseme ili muandike tena na kuuza

  3. Lowasa ni mtaji wenu wa biashara bila lowassa hamna biashara ya magazet

  i
  4. Mnatumika na Lowassa katika mbio za 2015 kama mlivyotumika 2005!!


  Watanzania… magazeti yanayoandikwa na hawa wenzetu yana sifa zifuatazo;

  1.
  Huandika habari ambayo humfanya msomaji atengeneze conclusion mwenyewe

  2. Hazina uwazi na uhakika wala mwendelezo kuwa hizo ni investigative journalism

  3. Nyingi zimejaa kumtukana muhusika mwanzoni ili ununue na magazeti

  4. Tofauti ya magazeti haya na ya shigongo ni kuwa ya shigongo ni udaku wa mapenzi na haya ya ‘watu' ni ya udaku wa kisiasa.

  5. Watanzania wenzetu hawa wamesoma nyakati na saikolojia zetu, kuwa tunapenda sana habari za kuambiwa na kusikia na hatupendi results na matendo..ndiyo tabia za wanasiasa wetu Waandishi hawa wakakubali kwenda Arusha na wakalipwa per diem zao na leo kutuletea habari zile zile na kuuza magazeti.. walioliwa ni wananchi tena…poleni!


  Lazima tukubali kuwa

  1. System za nchi yetu zimeoza na haziwezi kuwauliza wala kuwashtaki viongozi wetu

  2. Mahakama zetu hazina nguvu na zina matukio ya msimu ya kufurahisha watu

  3.
  Wananchi wa Tanzania hawana nguvu yeyote ile na wengi wanaishia kusema na ili tatizo halijatafutiwa ufumbuzi! They keep on talking!!!...  Ikiwa kwa muda wa miaka sita au saba sasa akina JK na timu yake wameambiwa na wezi na hakuna kilichofanyika ni wajibu wa kulitayarisha taifa letu lisitumbukie kulekule.Ujenzi wa taifa ufanywa na wazalendo, wakweli wenye uchungu na taifa hili na wasioyumbishwa na habari za msimu au mvua za vuli. Wajenzi wa taifa huwa wakweli na uangalia mbali sana. Nyerere alikuwa mmoja wao na matokeo yake mpaka leo tunayaona mazuri yake na mabaya yake yalikuwa sehemu ya kulijenga taifa!Leo utasikia na kuona swala la ufisadi ni kila kona na sio hawa wachache wanaotamkwa kila siku

  Waandishi wawaeleze watanzania kuwa

  1.
  Ufisadi uko kila mahali na kufanywa na wale ambao machoni pa watu wanaonekana malaika

  2. Rushwa ni janga la kitaifa na wapitishe hata promotion na zawadi za watu kufichua wala rushwa na kuzifanyia kazi

  3.
  Waandishi watafute mbinu za kuimarisha mahakama na sio kulea uozo uliopo


  Ili tuendelee tunahitaji system nzuri ni wajibu wa waandishi wa habari kuwauliza wanaolia mageuzi wawaulize maswali yafuatayo

  1. Wapinzani say Chadema itajenga mfumo gani mzuri wa kuzuia kutengeneza akina Lowassa wengine? Kwa mfano Mbowe ni mfanyabiashara je akiwa waziri mkuu atajitenga vipi na biashara au ni yaleyale ya kuwaleta watu wengine wapya ili waibe kwa upya na kuneemeka kwa upya?

  2. Je upinzani mfano chadema leo hii imetoa ufumbuzi gani wa kupigana na ukosefu wa ajira wamesema nini?

  3. Tatizo la elimu yetu liko wapi na chadema wanasemaje kuongeza quality ya elimu pamoja na sera nzuri ya free education?

  4. Chadema na wenzao wamefanya nini ili kupata free electoral committee? Katiba ibadilishwe yote au tuanze na tume huru? Au Chadema wako tayari kuingia kwenye uchaguzi mwingine ambao baada ya uchaguzi wanaanza kulia tumeibiwa kura, faulo imechezwa…

  Kama waandishi mkiwauliza chadema na wakawapa majibu mazuri ambayo ni practical why not start campaining for chadema from today?

  Badala ya kuwaongelea akina Lowassa ambae mnasema mwizi na anawakaribisha chakula chake mnakula!!
  Kama chadema au wapinzani hawana majibu ya matatizo yetu tuambieni tuendelee kula rushwa kutokana na urefu wa kamba zetu. Kuwa sema akina Lowassa ni usaliti mkubwa wanafsi na taifa linaloangamia kila kona na maamuzi mabovu ya viongozi wasio na uwezo.

  Nchi imekuwa ya kuongea kila mtu anaongea na yule anayeongea hajui kuwa anaongea anafikiri anatenda, ukitenda kitu kitafanyika mtikisiko wa tendo lako utaonekana..kamwe hamna mtikisiko kwenye kusema na kuongea mlilotegema jana kwa Lowassa halija tikisa mmendeleza usaliti ule ule wa kula fedha za watanzania kupitia habari zenu ambazo ni ‘news'

  Alichofanya jana Lowassa ni mwendelezo uleule wa 2005! mwenye macho asikie

  Waambieni wananchi kuwa CCM imeshindwa kazi.. na waelezeni nani anaweza...anayeweza asiweze kwa maneno kama CDM wanavyofanya sasa waweze kwa kusema sera zinazotekelezeka sio kusema tu...wale mafisadi..haitoshi

  nilikuwepo


   
 2. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  nilichoshindwa kumuelewa EL ni kwamba ati haoni mapungufu ya Rais................nikakumbuka kumbe mgao wa billion 111 ni wa wote.
   
 3. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  woote wezi tu hakuna wa kumuamini hata mmoja ndio maana sisomi teena magazet ya tanzania
   
Loading...