Watanzania ni uoga ndo uliosababisha kufika hapa tulipo, watu wanatekwa mchana kweupe wakijua watanzania hakuna kitu watafanya.
Ila siku tukishinda huu uoga, tukaungana kwa wingi wetu bila kujali itikadi za vyama na wala dini, ni rahisi sana kuitoa serikali iliyopo madarakani, kwanini?, kwasababu Tanzania haijawah kutokea movement kubwa kuipinga serikali hivyo hata serikal hawaja wekeza kwenye resources za kutosha kupambana na hvyo vitu.
Mfano kenya ina uzoefu, ndo maana hata askari wao wana hadi kinga za miguu kama za waendesha piki piki, ili kuzuia kupigwa mawe ya ugoko wakati Tanzania wanavaa field force tena sio wote, magari ya washa washa hayazidi kumi Dar nzima, idadi ya askari active ni ndogo sana tofauti na kenya ambayo ina recruit polisi wengi ili kujiandaa na maandamano ya kila kukicha.
Kama Tanzania ikiandamana, mfano Dar tukajitokeza watu kuanzia 20,000 kwenda juu, serikali inaanguka masaa machache tu.
Zanzibar tu ilibidi vijana wa JKT wavalishwe nguo za polisi, na hyo ilikuwa ni upinzani tu, imagine watu wote bila kujali chama wakaungana.
Mtwara ilibidi ipeleke Jeshi kwenye lile sakata la gesi. Kwa ufupi polisi wa Tanzania kwenye swala la maandamano ni bado sana, nguvu yao ni ndogo, Na hyo ndo faida TZ inayo kama siku tukiamka kupambania Haki.