Tumepoteza ujauzito wetu leo

mkonowapaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
1,493
767
Wapendwa..

Leo tumepoteza ujauzito wa mke wangu wa takribani mwez mmoja na nusu.
Alianza kulalamika maumiv ya tumbo kisha bleed ilianza.Tuliwah hospital akapatiwa Dawa tu kisha kuruhusiwa kurud nyumbani na baada ya hapo maumivu yalizid na baada ya muda kiumbe kilitoka..
Ni uchungu mkubwa sana kwetu hasa ukizingatia tulivyomtafuta kwa muda mrefu...lakini mapenz yake Mungu yatimizwe.
Ushauri maoni yanapokelewa.
Tunatarajia kwenda hosptal jumatano kwa ajili ya usafishwaji wa kizazi.
 
tulia mzeiya baada ya kusafisha mjiandae tena piga penalty nyingine nyavu zitatikisika tuu.
 
Hakuna sababu ya kuleta huku aisee, hapo kuna sababu nyingi za kutokea misacarriage. Hapa zaidi ya jokes na pole zisizo na impact tu utapata.

Wacha ujinga, enda kwa Dr atawapa ushauri wa kitaalamu. Na fuateni huo na sio story za huku PERIOD
 
Poleni sana Mkuu. Mtafanikiwa tu msikate tamaa na kama kuna masharti ya Doctor basi myazingatie sana.
 
Poleni sana kwa kupoteza kiumbe inabidi mtulie apumzike hata six month ndo mjaribu tena, na akiipata tu awahi hospital ili kujua hilo tatizo. Msisahau kumuomba Mungu
 
Hakuna sababu ya kuleta huku aisee, hapo kuna sababu nyingi za kutokea misacarriage. Hapa zaidi ya jokes na pole zisizo na impact tu utapata.

Wacha ujinga, enda kwa Dr atawapa ushauri wa kitaalamu. Na fuateni huo na sio story za huku PERIOD
Acha kumchamba mleta mada mkuu kashatoka hospital hapa tuna mpa matumainj ka tiba ya kisaikolojia pia waliopitia same experience kushare walifanyaje.
 
Back
Top Bottom