Bwana Balile. Ukitaka kuwa msafi katika utumishi wowote ule, pale bosi wako anapofanya makosa, wewe unatakiwa kunawa mikono kwa kujiuzulu, ili usiunganishwe na huo uamuzi. Bwana Maswi aliposhauri vizuri, wenzake na mabosi wake walipoenda mrama, alitakiwa ajiuzulu ili kunawa mikono, abaki msafi. Kwa kubaki kwakwe ofisini, mambo yameenda vibaya ofisini kwake yeye akiwa mtendaji mkuu. Nani awajibike? Huwezi kubaki ofisini ukiwa na kosa kubwa, ukaendelea kudai huo uamuzi ulifanywa na wakubwa, wewe huhusiki, wakati taasisi yako ndio imeyumba na kuporomoka. Unakosa uhalali wa kuwepo ofisini kama mtendaji mkuu na mfanya maamuzi mkuu. Tena pale ushauri wake ulipotupiliwa mbali na Ikulu na CAG, tayari alishadharaulika, alitakiwa aombe kuachia ofisi. Tunawaomba watumishi wote wa umma kuwa imara katika ofisi zao, kufanya kazi kwa misingi ya sheria, na kujiamini kitaaluma na kiuweledi. Hii itapunguza kuingiliwa na wanasiasa na watendaji wengine waganga njaa na mafisadi. Tanzania ya leo inahitaji watumishi imara katika maamuzi, kujiamini, uwazi na weledi.