Tumelidhalilisha jeshi pasipo na sababu za msingi, kuna siku litasema 'No thank you'

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Kila jambo na 'professionalism' yake, kazi ya jeshi ni kulinda nchi na mipaka yake, kazi ya jeshi siyo kubangua korosho, jeshi lina taratibu zake na utaalamu wake, limezoea amri, lina nidhamu yake, ndiyo maana ilibidi kwanza litii amri ya CiC ingawa lilijua kabisa kazi linayopewa ya kubangua korosho ni ngumu kwake.

Binafsi sikuona sababu zozote zile za msingi kulitumia jeshi kubangua korosho wakati wazoefu wa kazi hiyo wapo I mean wameshindwa wajibu wao, jeshi halina uzoefu wowote wa ununuzi na ubanguaji wa korosho, kama ingekuwa ujenzi wa madaraja sawa, kazi ya uokoaji sawa kwa sababu jeshi lina vitengo hivyo lkn halina kitengo cha kubangua korosho.

Tushukuru Mungu safari hii jeshi lilitii amri lkn kuna siku litasema hatutaki tena kudhalilishwa kwa mara ya pili, tuombe siku hiyo isiwepo, lkn kwa kilichotokea Mtwara hadi jeshi kusema limekwamishwa kutokana na ukiritimba wa baadhi ya watendaji basi kuna siku halitakubali kukwamishwa tena.

Pengine hili lichukuliwe kama changamoto na fundisho kwa watawala wetu kuwa, next time wanapoamua kulitumia jeshi kuwe na jambo la dharura na sababu za msingi kiasi kwamba bila jeshi kuingilia kati basi usalama wa nchi utakuwa hatarini, wasilitumie jeshi kama mgambo wa jiji kutatua mambo madogo madogo ambayo yanaweza kutatuliwa na kada zingine, otherwise itakuwa ni kulikosea heshima jeshi linapoonekana limeshindwa wakati mwingine ni kutokana na uzembe wa baadhi ya viongozi.

Viongozi tuepuke kulitumia jeshi letu kwa political mileage, lisiwe dumping basket kwa makosa ya wanasiasa, ferry mbovu tulilitupia, korosho tumelitupia, jeshi ni silaha yetu ya 'mwisho', tukilikizoea sana kuna hatari ya jeshi kuamua kuchonga mzinga wake lenyewe nakusema 'enough is enough'.
 
Mhh
IMG-20181230-WA0027.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viongozi wa Tanzania hawajui kutumia raia wake utakuta barabara inajengwa na wachina. Sasa kwanini serikali haijanunua zana zake wenyewe na kutumia wataalamu wake. Ili kutandaza barabara nchi nzima? Lakini utakuta ina nunua mashangingi kwa wabunge kila miaka 5. Badala ya kununua vifaa vya kutengeneza barabara, halafu utasikia serikali inasomesha wasomi mpaka ulaya. Lakini inatumia wasomi wa kichina kutengeneza barabara.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
hii habari ya Jeshi kushindwa na korosho ni uongo ,mbona sijaiona wala kuhakikishiwa kuwa ipo kurasa za ndani ya magazeti ya leo 31-12-2018.
 
Sun Tzu katika art of war anasema " Avoid a powerful enemy, attack the weak". Kwa mujibu wa Sheria hiyo, Jeshi halitakiwi kufanya kitu ambacho baadae kitaoneka KIMEFELI!. Jeshi kutuma message ya kufeli inampa adui kuevaluate uwezo wake wa kudeal na issue na kujua udhaifu wake!.

Sasa inapokuja kwa mission kama hizi ambazo ni purely za Kiraia, Jeshi siyo Rahisi KUWEZA, kwa sababu Either itabidi litumie protocol za Kijeshi ( Nguvu) ama Litumie Diplomasia katika sehemu kadha wa kadha. Likitumia Nguvu bado ni counterproductive kwa sababu kwanza siyo Heshima jeshi kuwaonea Watu wa Taifa lake ( Yaani katika Cycle za Kijeshi Duniani kote Jeshi kuumiza raia huwa ni aibu isiyo na mfano kwa makamanda, Sijajua huku Afrika huwa wanaonaje, lakini kwa jeshi lenye Discipline hiyo huwa ni taboo).
Lakini linapokuja katika suala la Diplomasia, Jeshi by nature ni chombo cha nguvu/ Mabavu, Halijawa Trained kuhandle issue za kudiplomasia, hiyo ni kazi ya viongozi wa Kisiasa. Sasa inapotokea viongozi wa kisiasa wanakwepa wajibu wao wa kudeal na issue za kiraia na kulitupia jeshi, Consequence za Jeshi kushindwa hiyo mission ni kubwa sana.

Nalishauri jeshi kabla halijakubali mission linazopewa na viongozi wa kisiasa liangalie hatua zifuatazo

1. Mosi, Je kuna solution ya kijeshi katika mission, au ni mtawala wa kiraia anayetaka kukwepa jukumu lake la kuprovide leadership na hivyo kulitupia jeshi zigo la kiraia?

2. Pili, kama kuna solution ya Kijeshi, Je Jeshi linao uwezo wa kudeliver hiyo Task kwa mujibu wa resources zilizopo. Ifahamike kwa mujibu wa Sun Tzu ni kwamba Jeshi likifanya mission ikafeli basi inatuma meseji mbaya sana ya udhaifu kwa adui wa ndani na nje, kuna watu wa Intelijensia katika kila nchi wapo wanafuatilia mission za kila jeshi ili kupima strength na weakness za majeshi ya nchi nyingine. Sasa ikitokea jeshi linashindwa mission kama hizi tayari adui ashajua nguvu ya jeshi ktk planning, logistics na execution ya mission

3. Liangalie consequence za hizo missions, Je zina haki ndani yake, je zinaumiza raia pasipo sababu, Je zinalinda uhuru wa watu, nchi na rasilimali zake au ni kwa ajili ya manufaa ya kisiasa ya mtu mmoja tu?

Naamini Amiri jeshi mkuu anaweza kuamuru jeshi kufanya analoona linafaa, lakini Makamanda kwa heshima na taadhima wanayofursa ya kumpa informed analysis na feasibility ya hiyo mission bila kuwa insubordinate!

Kwa kweli kwa mfano wa hii ishu ya Korosho, Wananchi wa mikoa ya Kusini wakiona Magari ya Jeshi yanakuja kusomba Korosho zao bila kulipwa eti kwa kuwa hawana mashamba Wanaona kuwa Jeshi ndilo linalowanyang'anya korosho zao, Kwa kweli hii haijakaa sawa hata kidogo kwa heshima ya Jeshi!.
 
Boti mbovu ilipewa jeshi ili msiiongelee, korosho nayo walipewa wanajeshi ili msiiongelee! Unapoiongelea korosho ni sawa na kuongelea mizinga na mabefaru. Hata kudai malipo ya korosho iliyotaifishwa ni sawa na kuvamia kambi ya jeshi!
 
Good analysis.
Walengwa take note!
 
Aisee mkuu Missile of the Nation umenikumbusha mbali sana kuhusu huyu Gen. Tzu na kitabu chake kilichojaa hekima za kimapigano. Anakwambia "General never wrong" kwamba lolote analoamulu generali lazima liwe executed ila kabla ya generali kutoa amri ni lazima hilo analotaka kuliamrisha awe amelipima na kujua matokeo yake yatakuwa ya namna gani "Always lazima yawe matokeo chanya, kama yatakuwa hasi basi ni aibu kubwa kwa generalized"
Back to the topic... Binafsi nilipoona hili swala limeusishwa jeshi na lenyewe likakubali moja kwa moja nilipata sana ukakasi wa kimkakati.
India yenye viwanda vya kubangua korosho vikijitahidi sana ile mitambo inabangua tani 20,000 kwa mwaka. Je sisi ambao hatuna hata kiwanda kimoja cha kubangua tungeweza kubangua hizo tani 200,000? Labda ndiomana ikatoka ile kauli ya "watabangua hata kwa meno". Hii ilikuwa kauli ya kisiasa kuonesha kuwa jeshi halishindwi. Sasa limekili kushindwa. Ni aibu kubwa katika falsafa za kijeshi
Wataalamu wanakwambia itachukua miaka 2-14 kumaliza kuzibangua hizo tani 200,000. Hivi ni kwamba kweli hakutani na wataalamu wa jambo husika na kushauriwa? Kama hili jambo limeshindikana kwa maamuzi yake ya kukurupuka, wananchi wanapata picha gani alipowawajibisha wale mawazili wawili kwaajili ya swala hili? Yawezekana walimshauri kuwa haiwezekani ila ye akawatimua na kalazimisha ifanyike anavyoona yeye. It was a pathetic act of our country's leadership. Hapa amejishushia heshima
Sichelewi kufikiria kuwa yawemezekana ile timua timua ni kwa personal interests zake na si kwa manufaa mapana ya nchii yetu.

Back
Top Bottom