Tumejipanga kudhibiti mamluki: ADC

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
Jumatatu, Septemba 03, 2012 05:19 Na Christina Gauluhanga, Dar es Salaam

CHAMA cha ADC, kimesema kimejipanga vizuri ili kudhibiti watu wabaya wanaoweza kukivuruga chama hicho. Akizungumza na MTANZANIA jana, Mwenyekiti wa chama hicho, Said Miraj, alisema wapo baadhi ya watu wanaweza kutumia nafasi zao vibaya, ili kukisambaratisha chama, lakini wao wako imara kukabiliana na watu hao.

Tunamshukuru Mungu kwa kupata usajili wa kudumu, hii ni hatua njema kwetu na tuna imani tutapiga hatua na kufikia malengo.

Lakini ole wao watakaojipenyeza kutuvuruga waelewe nafasi hiyo kwetu haipo sisi tunachohitaji ni maendeleo tu, alisema Miraj.

Alisema kwamba, ili kuhakikisha chama kinapiga hatua, chama hicho kimemtangaza mgombea wao wa ubunge katika Jimbo la Bububu ambaye ni Zuhura Bakari Mohamed (47).

Kwa mujibu wa Miraj, mgombea huyo ni askari polisi mstaafu aliyekuwa na cheo cha Koplo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita tulizindua kampeni za uchaguzi huo katika eneo la Kijichi kwa Geji, Mkoa wa Mjini Magharibi na nawasihi sana wananchi wajitokeze kumuunga mkono mgombea wetu.

Naziomba pia taasisi mbalimbali zijitokeze kumuunga mkono mgombea wetu, kwani awali kulikuwa na mfumo dume ambao ulichangia wanawake wengi kuwa nyuma kimaendeleo.

Kwa hiyo, hii ni nafasi pekee kwa wanawake kumpa nafasi mgombea wetu na leo tumeanza kutembea katika taasisi mbalimbali za kutetea haki za wanawake ili ziweze kumwezesha mwanamke mwenzao, alisema Miraj.

Mwenyekiti huyo pia alisema, wameanza mchakato wa kufanya ziara nchi nzima, ili kuwashukuru wananchi waliowawezesha kupata usajili wa kudumu.

Tumeanza mchakato wa kufanya ziara nchi nzima, ili kuhakikisha tunatembea kila kona kwa ajili ya kujieneza na kuwashukuru waliotuunga mkono, alisema.

Toa Maoni yako kwa habari hii
 
Mi namuita Chalii yule wa CUF aliekuja kwenu alipoulizwa juu ya msimamo wa Chama juu ya serikali 2,1 au 3 katika majibu yake akasema " WANASEMA jambo litakua ni maamuzi wa watanzania" This means hajui anachokiamini.
 
Back
Top Bottom