Tumeikumbuka Dar ya Makonda ghafla

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,775
21,687
Tuseme ukweli tu, wakazi wengi wa Dar tumeshammisi mkuu wetu wa mkoa aliyepita mheshimiwa Paul Makonda.

Kwa jinsi Dar ilivyo, kiongozi kama Paul Makonda aliiwezea haswa maana alikuwa anajua watu wake wa dar tunapenda nini haswa kifanyike kwenye uongozi wake.

Makonda alikuwa ana mikakati mingi sana mizuri kuhusu jiji hili , mfano kulifanya jiji la Dar liwe la masaa 24 yani wakazi wake wawe huru kutembea na kufanya biashara kwa masaa yote 24 kadri wapendavyo huku suala la usalama likiimarishwa zaidi.

Jiji la Dar , linahitaji kiongozi anayejua bata haswa maana hili sio jiji la wachimba chumvi au wakulima , hili ni jiji la kujiachia.

Hakuna mkuu wa mkoa yeyote aliyewahi kuwa karibu na wasanii (waigizaji na wanamuziki ) kama mh Paul Makonda hivyo ilikuwa ni rahisi kwa wasanii kutatulia kero zao ndogo ndogo ndani ya muda mfupi.

Paul Makonda ,ndiye mkuu wa mkoa pekee aliyewaandalia wanavyuo wa dsm tamasha kubwa la kuwakaribisha wanafunzi wa vyuo mwaka wa kwanza na aliwaletea wasanii wengi sana kuwaburudisha, tamasha alilifanya Mlimani City, na aliwapa ahadi kuwaletea wasanii wakubwa zaidi kutoka nje ya nchi.

Paul Makonda ndiye mkuu wa mkoa pekee ambaye alikuwa na uwezo wa kuwashawishi wafanyabiashara mbalimbali waweze kushusha bei za bidhaa zao kama kunatukio muhimu lenye faida kitaifa, mfano kushushwa kwa bei za vinywaji (bia) mf Taifa stars waliposhinda nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la shirikisho barani Africa.

Paul Makonda aliwajali sana wajane, mayatima na wanawake wanaonyanyasika kwenye ndoa zao , wengi walikuwa wanamkimbilia yeye kama mtetezi wao na wengi walifanikiwa na ushahidi ninao.

Dar ya Kunenge kwa kweli hainogi ,kwanza haingiliki .

Viva Makonda, viva

Makonda oyeeeeeee.

team_paul_makonda-20200811-0001.jpg
 
Kizazi cha burudani na tafrija! Kwa hio kukosekana kwa matamasha ndio tumepoteza kiongozi?

Walikuwepo wengi nao wametoka wamewaachia wengine nao watatoka na maisha yanaendelea.

Dar es laam ipo kabla ya makonda na iliendelea na itakuwepo baada yake na itaendelea.

Dar es laam ni kubwa hapa tanzania, ipo kabla ya kuzaliwa tanganyika na baadae Tanzania. Ikiitwa mzizima, na walikuwepo wakuu wake. Leo hawapo ila Dar ipo!

Lakini pia huu mji sio wa starehe broo! Ni mji wa mishe na ndio maana tunaona yaliopo jinsi yalivyo.
 
Back
Top Bottom