Tumeikumbuka Dar ya Makonda ghafla

Tumeikumbuka Dar ya Makonda ghafla

Hovyo Kwanza mkoani kwetu hatutaki mtu asiyekuwa na kazi, mzururaji, na mbangaizaji. Polisi kamateni watu wa aina hii, wazee wa mission town.
 
Saizi yuko zake London anakula bata anapunguza stress za wajumbe wa Kigamboni
Huko hawajamzuia kuingia? Kuna watu wanashupaza shingo kufurahia 'kukwama' kwa Makonda hata airport hawajui ndani ikoje!
 
Embu kwaanza tutoke uchaguzi mkuu,tutaandamana lazima arudi.
 
Huko hawajamzuia kuingia? Kuna watu wanashupaza shingo kufurahia 'kukwama' kwa Makonda hata airport hawajui ndani ikoje!
Huyu alizuiwa na Pompeo na si kwa kina Borris.
 
Tuseme ukweli tu, wakazi wengi wa Dar tumeshammisi mkuu wetu wa mkoa aliyepita mheshimiwa Paul Makonda.

Kwa jinsi Dar ilivyo, kiongozi kama Paul Makonda aliiwezea haswa maana alikuwa anajua watu wake wa dar tunapenda nini haswa kifanyike kwenye uongozi wake.

Makonda alikuwa ana mikakati mingi sana mizuri kuhusu jiji hili , mfano kulifanya jiji la Dar liwe la masaa 24 yani wakazi wake wawe huru kutembea na kufanya biashara kwa masaa yote 24 kadri wapendavyo huku suala la usalama likiimarishwa zaidi.

Jiji la Dar , linahitaji kiongozi anayejua bata haswa maana hili sio jiji la wachimba chumvi au wakulima , hili ni jiji la kujiachia.

Hakuna mkuu wa mkoa yeyote aliyewahi kuwa karibu na wasanii (waigizaji na wanamuziki ) kama mh Paul Makonda hivyo ilikuwa ni rahisi kwa wasanii kutatulia kero zao ndogo ndogo ndani ya muda mfupi.

Paul Makonda ,ndiye mkuu wa mkoa pekee aliyewaandalia wanavyuo wa dsm tamasha kubwa la kuwakaribisha wanafunzi wa vyuo mwaka wa kwanza na aliwaletea wasanii wengi sana kuwaburudisha, tamasha alilifanya Mlimani City, na aliwapa ahadi kuwaletea wasanii wakubwa zaidi kutoka nje ya nchi.

Paul Makonda ndiye mkuu wa mkoa pekee ambaye alikuwa na uwezo wa kuwashawishi wafanyabiashara mbalimbali waweze kushusha bei za bidhaa zao kama kunatukio muhimu lenye faida kitaifa, mfano kushushwa kwa bei za vinywaji (bia) mf Taifa stars waliposhinda nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la shirikisho barani Africa.

Paul Makonda aliwajali sana wajane, mayatima na wanawake wanaonyanyasika kwenye ndoa zao , wengi walikuwa wanamkimbilia yeye kama mtetezi wao na wengi walifanikiwa na ushahidi ninao.

Dar ya Kunenge kwa kweli hainogi ,kwanza haingiliki .

Viva Makonda, viva

Makonda oyeeeeeee.

baba kegan
 
.....
 
Mji umekuwa kimya sana, maana kukicha unawaza leo ataamka na lipi.
 
20171211_111557.jpg

Picha ya tarehe 2017 December 11
 
Back
Top Bottom