Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,438
Shost alipata msichana wa kazi kutoka mikoani. Ni binti aliyetoka kwenye familia yenye hali ngumu mno kimaisha. Akiwa na miaka 14, baada ya kumaliza darasa la saba, wazazi wamemtoa aende Darisalama akafanye kazi kwa makubaliano ya kupelekewa nusu ya ujira wake kila mwisho wa mwezi.
Binti huyu kazi za kawaida za kufua na kupiga deki zilionekana kumshinda. Mwajiri wake aliona ni kheri ampeleke hospitali kwa uchunguzi. Amefika kule baada ya vipimo vyote iimegundulika kuwa binti ana moyo mkubwa.
Mwajiri ameamua kumrudisha kijijini kwani hawezi gharama za kumtibu na anaogopa asife mikononi mwake. Kweli tumekosa utu namba hii?