Tumedanganywa sana na Utawala wa Awamu ya 5, ushahidi ni tril. 360 kuwa kanyaboya

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,074
Leo nimewaza sana baadhi ya matukio ya serikali ya awamu ya 5 baada ya kumsikia mhanga wa shambulio la kupigwa risasi wakati wa utawala wa Mwendazake.

Jambo nililolikumbuka ni hili la tril.360 za makinikia. Nikikumbuka jinsi tume zilivyoundwa na majaji na maprofesa kuchunguza suala hili na kuja na majibu kuwa tuliibiwa sana na Barrick na mwisho kuja na hitimisho la kuwa tunawadai tril.360.

Niliamini kweli Mwendazake anaipigania nchi lakini baada ya ukimya kutawala wa kulipwa hizo fedha na mwisho Prof. Kabudi kuwatamkia watanzania kuwa zile tril.360 zilikuwa ni kayaboya niliishiwa nguvu, na kuamini kuwa kumbe Mwendazake alikuwa anatudanganya mambo mengi sio hili tu.

Niwatakie Jumamosi nono.

Tril.360 ni "KANYABOYA".

1664915659087.jpg
 
Mbona mnaanzisha thread usiku wa manane???
Nyie ni wachawi?? Kwamba hamlali
Madaktari mahospitalini hawalali wanahangaika kuokoa maisha ya watu je nao Ni wachawi?

Madereva wa malori wanafanya kazi Sasa hivi kwenda mikoani na nchi jirani kupeleka bidhaa na huduma huku wakiweka ugali mezani nao Ni wachawi?

Radio and TV stations zinafanya kazi usiku huu kutoa habari na mengineyo huku wachapa magazeti wakiandaa mzigo wa kesho nao Ni wachawi?

Kuna watu wako kwenye kiwanda Cha kuchakata mbususu ili wapate watoto hao Ni wachawi?

Kuna watu wako majumbani na mahospitalini Ni wagonjwa wanaoigania uhai pamoja na wanaowahudumia nao Ni wachawi?

Kuna vyombo vya ulinzi na usalama vipo macho Sasa hivi kwa ajili ya usalama wa Mali, watu, na nchi je nao Ni wachawi!

Kwanini hamtaki kuwa GT? KUFIKIRI KABLA YA KUANDIKA IMEKUA NI ADHABU Pascal Mayalla Mshana Jr
 
Awamu ya tano na ya sita viongozi wa juu ni hao hao kasoro mmoja. Hata aliyechukua nafasi za juu tatu nae ni wa awamu ya tano pia.

Porojo zenu za kutenganisha mnaboa Tu..
Unadhani Ni kwanini Ni wale wale!?
Ilifaa katiba iseme kutakua na uongozi wa mpito then baada ya mwaka uchaguzi mwingine ufanyike! Kwakua CCM et. all waliona Hilo wakaona namna yabkujilinda bora wapokezane humo humo ndio Mana tuko tulivyo! Sasa tukisema we need a new constitution tunamaanisha haya! Tatizo wajinga flani wanakinganisha katiba na chakula mezani! Na mtu akishagusa tumbo it's done
 
Leo nimewaza sana baadhi ya matukio ya serikali ya awamu ya 5 baada ya kumsikia mhanga wa shambulio la kupigwa risasi wakati wa utawala wa Mwendazake.

Jambo nililolikumbuka ni hili la tril.360 za makinikia. Nikikumbuka jinsi tume zilivyoundwa na majaji na maprofesa kuchunguza suala hili na kuja na majibu kuwa tuliibiwa sana na Barrick na mwisho kuja na hitimisho la kuwa tunawadai tril.360.

Niliamini kweli Mwendazake anaipigania nchi lakini baada ya ukimya kutawala wa kulipwa hizo fedha na mwisho Prof. Kabudi kuwatamkia watanzania kuwa zile tril.360 zilikuwa ni kayaboya niliishiwa nguvu, na kuamini kuwa kumbe Mwendazake alikuwa anatudanganya mambo mengi sio hili tu.

Niwatakie Jumamosi nono.

Tril.360 ni "KANYABOYA".

View attachment 2505321
Wewe una chuki binafsi na Awamu ya 5, bila shaka ulifaidi kuibwa makanikia yetu. Kuna mawakili waliokuwa wa shauri wa kampuni za madini na ni washauri mpaka leo wamekuwa mabilionea kwa posho zao kulipwa kina Barrick. Mmechukia sana kunyanganywa tonge mdomoni. Angesema tunadai bilioni 10 kumbe ni bilioni 900 hapo tungechukia, lakinikuna kosa gani kudai 900 kumbe ni 90 ukapata 90? Kuna hasara gani hapo?
 
niliishiwa nguvu, na kuamini kuwa kumbe Mwendazake alikuwa anatudanganya mambo mengi sio hili tu.

Niwatakie Jumamosi nono.

Tril.360 ni "KANYABOYA".
Nashauri tupunguze kumsema kwa ubaya na kumtuhumu mtu asiyeweza jitetea!. Hizo triioni 360, JPM hakutudanganya bali ni yeye ndiye alidanganywa, watu wakusaidia asidangayike tukamwambia anadanganywa, very unfortunately akadanganyika,
ila baadaye akaambiwa ukweli, hivyo tukalifuta hilo deni kimya kimya. Maendeleo ya kweli Tanzania yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye, Tusidanganywe, Tusidanganyike!
 p
 
Ila yeye pekee ndie aliyejenga Mazingira ya kudanganywa hasa kwenye exaggerated data! Na aliwapa vyeo na tuzo waliomdanganya na yeye badala ya kuchuja anakuja nazo public zilivyo!

Umesahau apple punch ya kwa Andre Rajoilina?

Watu wanashindwa kuelewa Nini maana ya kumuacha apumzike! (Wàche kumsifia au wakosoea na kuanika udhaifu wake?).

Kaka P unaweza kusaidia mstari uchorwe wapi ili apumzike. Mana Kama amekufa hawezi kujitetea Basi amekufa na hawezi kupokea sifa aachwe alale!
 
Mkuu DolphinT , asante kuni tag hapa.
P
Unani-inspire Sana katika uandishi wako ambao unahitaji kusoma, kufikiri, kung'amua, kuchambua nakutafuta hidden meaning na kujua falsafa na mrengo wa mwandishi!

Unaipa JF sababu ya kuwa GT platform sio FB ndio Mana nikakutag!

Nimesoma post zako miaka mingi kabla ya kuamua kuanza KUANDIKA! Sasa Kama mtu anaamini wachawi tu ndio hawalali what kind of mentality is this? Si aibu.

Asante
 
Ila yeye pekee ndie aliyejenga Mazingira ya kudanganywa hasa kwenye exaggerated data! Na aliwapa vyeo na tuzo waliomdanganya na yeye badala ya kuchuja anakuja nazo public zilivyo!
He is a human being, wakati anadanganywa hakujua kuwa ni anadanganywa ndio maana akaja public, baada ya kujua amedanganywa hakuzungumzia tena hilo deni!.
Umesahau apple punch ya kwa Andre Rajoilina?
Nakumbuka sana, that was giving it a try, hakuna ubaya kujaribu jambo lolote kwa nia njema ya kuokoa taifa lako!.
Watu wanashindwa kuelewa Nini maana ya kumuacha apumzike! (Wàche kumsifia au wakosoea na kuanika udhaifu wake?)
Kumuacha apumzike ni kutomzungumzia marehemu kwa ubaya, usimtuhumu mtu ambaye hawezi kujitetea.
Kaka P unaweza kusaidia mstari uchorwe wapi ili apumzike. Mana Kama amekufa hawezi kujitetea Basi amekufa na hawezi kupokea sifa aachwe alale!
Tuna utamaduni, marehemu hasemwi vibaya, wakati yale mema na mazuri yanaendelea kuishi na kusemwa daima milele !.
P
 
Back
Top Bottom