Tumeanza uchunguzi bei mpya ya mafuta-EWURA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumeanza uchunguzi bei mpya ya mafuta-EWURA

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Rutashubanyuma, Jul 10, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Na Godfrey Ismaely

  MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema imeanza kufanya uchunguzi kuwabaini wafanyabiashara wanaoendelea kuuza mafuta ya
  dizeli na petroli kwa bei ya juu ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.

  EWURA imesema baada ya serikali kushusha kodi katika bidhaa hiyo wafanyabiashara wote walitakiwa kuanza kushusha bei tangu Julai mosi mwaka huu.

  Mamlaka hiyo imesema kwa mujibu wa tangazo la serikali namba tano la Januari 9, 2009 EWURA imepewa wajibu wa kudhibiti na kusimamia mwenendo wa mafuta nchini ikiwa ni pamoja na kutoa machapisho ya bei elekezi na kikomo kwa mafuta hayo.

  Akizungumza na Majira jana, Ofisa Uhusiano wa mamlaka hiyo Bw.Titus Kaguo, alisema mabadiliko ya awali katika marekebisho ya mafuta hayo yalianza kutekelezwa rasmi kuanzia Julai mosi na kwamba mfanyabiashara yeyote anayeendelea na bei ya juu anafanya makosa.

  "Baada ya marekebisho ya kodi katika kanuni ya ukokotoaji wa bei za mafuta, Dizeli imepungua kwa asilimia 4.86 hivyo bei elekezi ikiwa ni sh.1,939 kwa lita.

  "Kwa upande wa bei mpya ya mafuta ya taa ikiongezeka kwa asilimia 21.88, bei elekezi ikiwa ni sh. 1,940 kwa lita," alisema Bw.Kaguo.

  Hata hivyo alisema bei hizo zinaweza kutofautiana kadri mafuta yanavyosafirishwa mbali na soko la Dar es Salaam kuanzia kilomita 30.

  Alisema licha ya kurekebisha tozo za gharama zingine kwenye mafuta pia EWURA imeanza mchakato ambao utawezesha kupungua kwa gharama za nishati hiyo ifikapo Agosti Mosi mwaka huu.

  "Ushirikiano ni jambo la msingi sana kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali, kwa kuzingatia shughuli za ukusanyaji wa maoni na uhandaaji wa kanuni mpya ya rasimu kwa ajili ya maandalizi ya kukokotoa bei za mafuta kwa lengo la kupunguza gharama hizo," aliongeza Bw. Kaguo.

  Alisema mamlaka hiyo itaendelea kutoa takwimu sahihi mara kwa mara kwa umma na wafanyabiashara ili waweze kutambua mabadiliko na hata viwango vya bei za mafuta zinavyokwenda.

  Uchunguzi wa Majira ulibaini kuwa licha ya serikali kupunguza kodi ya mafuta ya dezeli na petroli wafanyabiashara wameendelea kuwalangua wananchi kwa kuwauzia kwa bei ya zamani huku wakisingia kuwa walikuwa na akiba kubwa kwenye maghala.
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  EWURA, SUMATRA, TAKUKURU ni taasisi za ulajiulaji tuuuu.

  EWURA ina maana hamuoni bei kwenye vituo vya mafuta au mnatuzingua???? Huo uchunguz hapo si unahitaji mapesa tena,yaani hadi raia walalamike???? Sijui nyie mnafanyia kazi wapi???? Kwani hivi vituo vya mafuta vipo kila mahali.....

  Pia nyie watu wa EWURA tangu chombo kiundwe naona matatizo ndio yamechachamaa.....nyie mmeshindwa kupambana na wachakachuaji wa mafuta hadi bei ya mafuta ya TAA imepanda,hamna maana kabisa nyie,bhalafu ndio wa kwanza kulalamikia POSHO...........
   
 3. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  huu sasa ni upumbavu!! uchunguzi wa nini badala ya kwenda polisi na kukamata wote!! acheni kujibaraguza EWURA.. mbona vituo vyote vimepandisha bei baada ya julai mosi. sijaona kituo kinachouza chini ya 2,100.
  hata CARMEL waliokuwa wanauza 2040 wamepandisha hadi 2100.
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280

  Hizi siasa zitaishia lini?.....kweli tunahitaji uchunguzi kwenye jambo ambalo lipo wazi.................wanachopaswa kufnya ni kuwachukulia hatua mara moja....................................siyo kufanza utafiti...............................give us a break and we really need one................
   
 5. Ikumbilo

  Ikumbilo JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 455
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mamlaka mengine ni ulaji tu hakuna wanachosimamia wala nini.
   
 6. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Huu mbona mchezo wa kuigiza tena,walisema bei itapungua kati ya 300/- mpaka 400/- sasa hata mia haijapungua mbona kama tunadanganyana wajameni.
   
 7. j

  jmura Member

  #7
  Jul 11, 2011
  Joined: Apr 27, 2010
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania tumelaaniwa. Tuna viongozi wasiojali wananchi.

  Mafuta ya taa ndio yangepaswa yapunguzwe bei ili miti isikakatwe sana sasa tunaharibu mazingira na kutesa walala hoi, hiyo bei ya petrol na dizel haijapungua chonde chonde ewura acheni kuwatesa watanzania. Serikali acheni uongo wa kuhadaa wananchi! Watu wanateseka sana kwa sababu maisha yako juu sana!

  Viongozi waoga hawatufai
   
 8. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,105
  Likes Received: 6,579
  Trophy Points: 280
  1,9.... ni nini, sorry nina hasira, hii nchi bora warudi wazungu watawale, enough is enough.
   
 9. NYENJENKURU

  NYENJENKURU JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Sehemu nyingine za Morogoro ni Sh 2250 kwa lita.Kweli tutafika?
   
 10. Sailor Boy

  Sailor Boy Senior Member

  #10
  Jul 11, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 105
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi c mtambui kiwete kama raisi wangu!
   
Loading...