Tumeacha mambo ya Msingi tunajadili upuuzi!

Tumeacha mambo ya Msingi tunajadili upuuzi!

Lord Denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
23,494
Reaction score
57,869
Heri ya Mwaka Mpya kwenu wadau!
Natumai wote tu salama na tunaendelea vyema na majukumu yetu.

Mwaka 2020 umeshaingia. Na kila mtu anajua kuwa mwaka huu ni wa Uchaguzi Mkuu ambapo Watanzania wanaenda kuchagua viongozi wao Wakuu kwa ajili ya kuwaongoza.

Lakini pamoja na kuwa ni mwaka wa uchaguzi , tumekaribishwa na ripoti nzito ya IMF inayoelezea hali ya ukuaji wa kiuchumi hapa Tanzania.

Kwa watu wenye akili na wanaotafakari vizuri hiki ndiyo kilikuwa kipindi murua kwa Watanzania kujadili kwa kina bila kificho juu ya kwa nini tumefika hapa na nini kifanyike ili tutoke hapa.

Imenisikitisha sana kuona jukwaa hili limeanza kuwa mfu kiasi hiki kiasi kwamba pamoja na ripoti hii kuonesha hali si shwari hapa kwetu kwenye ukuaji wa uchumi still watu hawajadili jambo hili la msingi na wamekalia vijembe vya CCM na CHADEMA pamoja na nyimbo za kusifu na kuabudu

Nchi haishtuki, viongozi hawashtuki, Wananchi ndio wamelala usingizi wa pono pamoja na hali ya uchumi kuwa mbaya sana na dalili zote kuwa wazi.

Wiki hii kuna habari za kiwanda cha tiles Chalinze kufungwa kutokana na Kukosa biashara, Vilevile kwa kipindi kirefu kuna Habari nyingi za biashara mbalimbali kufungwa, watu kupunguzwa kazini na mambo mengi yanayoonesha uchumi wetu hauko sawa ila watu wamelala kila siku kuimba nyimbo za kusifu na kuabudu pamoja na vijembe vya vyama.

Kwa hali inayoendelea sasa kiuchumi Tanzania ilipaswa kila siku watu kutafakari na kujadili hali ya kiuchumi kiasi kwamba hata watawala watashtuka ila wapi watu wamekalia vijembe na kusifu na kuabudu.

Simshangai aliyesema Africa is a dark continent.

Tanzania tulisharogwa kitambo sana.
 
Wenye akili wame-resign kwenye fact kuwa aliepo madarakani hana mental capacity wala willingness ya kuelewa uliyoyaandika hapa.

Sasa hivi busara ni kuangalia what to do personally to mitigate what is sure to come tukisubiri mtu mwenye kutumia akili yake ipasavyo awe kiongozi wa nchi. Lini?

Only God knows but surely it won't be very wrong, maana aliepo sasa hivi anajikaanga mwenyewe.
 
Inasikitisha sana kwa kweli. Hali ni mbaya sana kiuchumi and it’s like watu wamefungwa akili
 
Kweli mkuu, biashara zikifungwa wanasema ikifungwa moja nyingine 100 zinafunguliwa, tena alisema mtu mwenye akili timamu kabisa! Hili la kiwanda cha vigae ni dhihirisho tosha kuwa mzunguko wa hela na uchumi hauko hali nzuri!
 
Ni hatari sana. Mbaya zaidi pamoja na wenye akili ikiwemo wasaidizi wake kuona shida na tatizo ila wamekuwa wakimpaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Wamekuwa wakimsifia kwenye uongo.

Hali ya kiuchumi ni mbaya sana kwa Tanzania
Nchi inaendeshwa na akili za mtu binafsi badala ya sheria na utawala bora, wewe JK unajua ulichotutendea watanzania?
 
Usitudanganye wewe, hali ya uchumi na maisha viko stable kabisa na mtaani watu wanafurahia maisha.
Wanaolalamika wengi ni wapiga dili, na hivyo viwanda vinavyofungwa ni wapiga dili waliozoea kuwaibia wanyonge...
 
K
Kweli mkuu, biashara zikifungwa wanasema ikifungwa moja nyingine 100 zinafunguliwa, tena alisema mtu mwenye akili timamu kabisa! Hili la kiwanda cha vigae ni dhihirisho tosha kuwa mzunguko wa hela na uchumi hauko hali nzuri!
Kweli kabisa. Purchasing power imeshuka sana kwa wananchi. Kasi ya watu kutoka kwenye low class kwenda middle class imeshuka sana. Kasi ya watu wa middle class kushuka hadi low class imeongezeka sana and people never seems to care
 
Usitudanganye wewe, hali ya uchumi na maisha viko stable kabisa na mtaani watu wanafurahia maisha.
Wanaolalamika wengi ni wapiga dili, na hivyo viwanda vinavyofungwa ni wapiga dili waliozoea kuwaibia wanyonge...
Kiwanda kinawaibiaje wanyonge. Tumia akili ndugu
 
Usitudanganye wewe, hali ya uchumi na maisha viko stable kabisa na mtaani watu wanafurahia maisha.
Wanaolalamika wengi ni wapiga dili, na hivyo viwanda vinavyofungwa ni wapiga dili waliozoea kuwaibia wanyonge...

Walewale waimba mapambio,

ni wapi Tanzania hii Wananchi wanafurahia maisha?
 
Back
Top Bottom