Tume ya Ushindani nchini (FCC) yawaonya Wafanyabiashara wanaopandisha bei ya Sukari

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Tume ya Ushindani Nchini (FCC) imetoa onyo kwa Wasambazaji na Wauzaji wa jumla na rejareja wa sukari nchini kuwa ni kosa kisheria kujihusisha na vitendo vya upandishaji bei na kuwataka kuacha mara moja

Imesema kitendo cha hivi karibuni cha baadhi ya Wafanyabiashara kupandisha bei ya sukari hadi kufikia Tsh. 4,000 kwa KG 1 ili kujipatia faida kubwa isivyo halali kwa kuwaumiza walaji pindi mahitaji ya sukari yatakapoongezeka

Tume hiyo imesema Wafanyabiashara wamekiuka Sheria ya Ushindani, hususan makatazo ya kupanga bei ya washindani pamoja na kuficha, kupinguza au kukataa kusambaa sokoni bidhaa kwa lengo la kupandisha bei ili kujipatia faida kubwa

Tume hiyo inajishughulisha na ushajiishaji na ulindaji wa ushindani wa biashara na kuwalinda walaji dhidi ya mienendo isiyo ya haki na ya kupotosha katika uchumi

EFD0AE2B-9B81-4610-8410-C29AF5E70707.jpeg
 
Hii tume ndio naisikia. Ndio washapandisha hivo kilo elfu 3,200 jana. Wanafanyeje sasa.
 
Back
Top Bottom