Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,436
- 5,234
Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani ya Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, imekutana na kufanya mahojiano na aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya leo Februari 24, 2026.
Kikao hicho kilichofanyika katika ofisi za Tume zilizopo ndani ya jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es Salaam, ni sehemu ya mfululizo wa mahojiano ambayo Tume inayafanya na viongozi wa sasa, wastaafu, na wadau mbalimbali ili kukusanya taarifa sahihi na ushauri wa kitaalamu.
Soma Pia: Tume ya Jaji Chande yakutana na Jaji Warioba kujadili matukio ya Uchaguzi wa 2025
Katika mkutano huo yamejadiliwa kwa kina namna matukio ya uvunjifu wa amani yalivyoanza, athari zake kwa wananchi, mali zao na miundombinu, pamoja na ushauri na mapendekezo ya namna ya kudhibiti na kuzuia matukio kama hayo yasijirudie siku zijazo.