Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Kama matokeo ya uchaguzi ya zanzibar yamefutwa na zec je?
matokeo ya Tanzania bara yana uhalali gani kisheria na kikatiba?

kwasababu Raisi wa muungano anachaguliwa pia na wazanzibar
tusaidiane mawazo tafadhali.
 
Sasa kama uchaguzi Zanzibar ulikuwa na kasoro nyingi, je kura za Zanzibar kwa rais wa Muungano nazo si ni batili? Hivyo Matokeo pia yaliyotangazwa na NEC ni batili.

Kura za Muungano organiser wake ni NEC sio ZEC
 
nilikuwa nasema ile mahakama ya icc inawaonea waafrika lakini leo nimeamini kwamba ile mahakama ni kwa ajili yetu na inatuhusu kabisa.
 
ZEC kufuta uchaguzi ni upuuzi uliopitiliza, tangazeni tu mshindi halali. Mnavyofanya hivi ndo mnaharibu zaidi aliyeshindwa akubali kipigo hiki mnachofanya ndo upuuzi zaidi. Sasa mnafikiri nani atakubali awaamini tena kurudi kupiga kura?
 
Sijui kama anawezatangazwa rais wa Muungano wakati upande wa pili wa Muungano matokeo yamefutwa! Mungu utupatie hekima na busara katika maamuzi haya
 
[h=2]Kama matokeo ya uchaguzi ya zanzibar yamefutwa na zec je?[/h]
matokeo ya Tanzania bara yana uhalali gani kisheria na kikatiba?
kwasababu Raisi wa muungano anachaguliwa pia na wazanzibar
tusaidiane mawazo tafadhali.
 
kwanini iwe hivi, Inasikitisha sana, naona sasa uchaguzi umekuwa moto kwetu. Sasa tunaanza upya, hakuna Rais wa JMT mpya kuapishwa. Kwanini iwe hivi
 
Nilijua tuna viongozi wabinafsi, lakini hata siku moja sikuwahi kufikiri ubinafsi wao ungefikia kiwango hiki. Last election ilibidi waunde serikali ya mseto, this election kuna iiregularities, mbona zinatokea tu wakati ccm wameshindwa? Nimesikitika mno.

Huu ni UFISADI mkubwa kuliko Richmond, EPA, na Escrow.

Tume ivunjwe, iundwe mpya.

Washitakiwe kwa matumizi mabaya ya madaraka na mali ya umma

Ni kutia Taifa umasikini kwa kuendekeza ubinafsi.

NB: Kikwete ataendelea kuwa raisi kwa muda huu, kisheria. Na Wasira bado ni Waziri.
 
Back
Top Bottom