Tume ya Uchaguzi (NEC) yakabidhi ripoti ya Uchaguzi 2015 kwa Rais Magufuli. Mikutano ya Vyama vya Siasa marufuku hadi 2020

Anampongeza Rais kwa kutenga bajeti kukamilisha uchaguzi Mkuu. Anamuomba Kikwete kukaa kwa salama na asisikilize kelele zinazotolewa kwani ni wajibu wake kuhakikisha Wastaafu wanalindwa
 
Anamshukuru Rais wa Zanzibar kwa kutenga fedha za kutosha kufanikisha uchaguzi wa Oktoba na ule wa machi
 
Anawapongeza viongozi wa vyama vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi uliomalizika na amewapongeza wale waliofika kwenye hafla hii akiwemo Mzee wa Mapesa
 
Sijaelewa JPM anaposema rais mstaafu (Jakaya Kikwete)uko SALAMA usisikilize maneno ya hovyo hovyo ya watu?
 
Mshindani huyo huyo anateua msimamizo wa mechi!. Ebu tutumie hata alikili ndogo tu!.Hivi hata tunapokwenda Msikitini au Kanisani kweli hatulioni hili kuwa ni dhambi na bado tunashika misahafu na bibilia kuomba tusamehewe lakini baada ya masaa bado tuko kwenye ndimbwi lile lile?

....huu muda wa maigizo sijui wanautoa wapi, halafu wanajidai hapa kazi tu!
 
Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana ulikuwa ni wa kipekee kwa sababu ulifanyika kwa mara ya kwanza kwa kutumia BVR. Hivyo NEC ililazimika kuboresha daftari ya wapiga kura kwa kutumia BVR. Hivyo tume ililazimika kuhutaji mashine 15,000 hata hivyo zilipatikana 8,000 tu. hata hivyo, tume ilifanikiwa kuandikisha watu kwa zaidi ya asilimia 99
 
Anawapongeza viongozi wa vyama vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi uliomalizika na amewapongeza wale waliofika kwenye hafla hii akiwemo Mzee wa Mapesa
Mkuu tunakushuru endelee kutupa kinachojili kwenye hiyo hafla.
 
Uchaguzi wa Mwaka jana ulikuwa na mvuto, ushindani wa pekee na ulivuta hisia ndani na nje ya nchi. Hata hivyo anashukuru uchaguzi umefanyika kwa njia ya amani na utulivu. Anawapongeza NEC kwa kusimamia uchaguzi huo. Walifanya kazi kubwa sana. Waangalizi wa kimataifa wamekiri kuwa uchaguzi ulifanyika kwa uwazi, haki na uhuru
 
Pamoja na mafanikio hayo, zipo changamoto ambazo hata hivyo zisiwakatishe tamaa.
 
Changamoto hazikosekani na ndo maana zipo nchi walilazimika kuhesabu kwa Mkono. Hapa Kenya inalengwa
 
Wapo wakosoaji wa aina mbili.
- wale ambao wanapenda kuishauri nchi na TUME ili wasahihishe makosa yao. Ameitaka Tume kupokea mapendekezo yao na wayafanyie kazi.
- wale ambao wanakosoa tu kwa vile mgombea wao hakushinda. Ameiomba Tume kupuuza kwa vile lengo lao si jema
 
Back
Top Bottom