LESIRIAMU
JF-Expert Member
- Feb 12, 2008
- 8,721
- 13,959
Kuna maneno nimemsikia katibu akiongea wakati Tundu Lissu anakabidhiwa fomu, nikaona ni busara ya hali ya juu sana ambayo hata Madiwani na watia nia Ubunge wangepewa hiyo fursa.
Nimemsikia akisema wakajaze fomu na wana ruhusiwa kurudi tume siku mbili au tatu kabla ya kuzirudisha ili zikakaguliwe kama zimejazwa sawa au kunahitajika marekebisho.
Hii ni busara maana sioni sababu ya kutegana ili kuenguana kwenye kinyang'anyiro.
Tumezoea wagombea ubunge na udiwani wakitegwa kwenye kukosea kujaza fomu ili waenguluwe. Kwanini hili pia lisiende huko ili fomu za wabunge/ madiwani zilizokosewa nazo zifanyiwe marekebisho? Hii ndiyo tume tunayotaka.