Tume ya Katiba kesho iko Missenyi, tuwaeleze nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume ya Katiba kesho iko Missenyi, tuwaeleze nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mr.kibulala, Jul 15, 2012.

 1. M

  Mr.kibulala Member

  #1
  Jul 15, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF,

  Kuanzia kesho Jumatatu hadi Jumatano, Tume ya Katiba itakuwa Missenyi (Kagera). Je, wananchi tupendekeze nini?

  Tafadhali weka pendekezo lako ili tuweze toa maoni
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  1. Serikali ya Tanganyika yenye bendera, wimbo wa taifa na mamla kamili juu ya Tanganyika.

  2. Kwa wale wanaotaka muungano, basi ningependekeza mtu akishashika nafasi ya urais Zanzibar asiruhusiwe tena kugombea urais katika ngazi ya muungano. Kuruhu hili ni kuwa na mtu mmoja kwenye uongozi bila kuwa na uelewa hali halisi. Na pia anakuwa hana tena jipya.

  3. Iwe ni marufuku kwa vyama vya siasa kujiingiza kwenye biashara. Hili ni muhimu sana sana sana kwa sababu chama kikiwa mwanahisa kwenye sekta fulani (kama ilivyo kwenye mafuta/CCM) wanakuwa hawana tena uwezo wa kuisimimia na ipo hatari ya kubadilisha sera ya nchi ili kukidhi mbia mwenza kinyume na maslahi ya taifa.

  4. Majimbo ya uchaguzi yawepo kisheria, sambamba ni hilo baraza la mawaziri liwe na ukomo - lisizidi watu 18.
   
 3. M

  Mr.kibulala Member

  #3
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shukrani mkuu, tutazingatia hayo leo
   
 4. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #4
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  FJM,

  Safi, nadhani hata pia tufikirie kuvifuta vyama vyote vya siasa na kuanza upya.

  Aidha, mawaziri waajiriwe na si kuteuliwa na rais; Rais asiteue majaji pia!

  Mr.kibulala
  Pendekezeni pia viti maalum bungeni kufutwa, hatuna tija navyo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Duh mkuu Invisible unataka tufute vyama vyote kweli! Labda tuweke masharti magumu ili tuwe na vyama vichache vyenye nguvu kuliko tunavyoshuhudia utitiri wa vyama ambapo uhai wa vyama vingine hauna uhakika.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  1. Serikali ifute ruzuku kwa vyama vya siasa.

  2. Mgombea binafsi kwa nafasi za Urais, Ubunge, Udiwani.

  3. Mawaziri wasiwe wabunge.

  4. Jaji Mkuu na Mwanasheria Mkuu majina yependekezwe na rais wabunge wawapigie kura.
   
 7. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  1. Mbunge wa huko huko ni STD VII, mgombea ubunge lazima awe na at least first degree
  2. Matokeo ya URAIS yahojiwe mahakamani
  3. Vyeo vya RCs, DCs, WEOs ubunge wa Viti maalumu, ubunge wa kuteuliwa vifutwe.

  PS: Mengine nilishayaandika kwenye thread kama hii
   
 8. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  1.Vyeo vya DC, RC vifutwe kazi zao zitekelezwe na DAS/DED na RAS.
  2.Madiwani wawe na elimu ya kuanzia diploma
  3.serikali ya Tanganyika irudishwe na kuunda serikali ya shirikisho
  4.Majimbo yaundwe kwenye serikali ya Tanganyika.-majimbo nane-ZIWA,MAGHARIBI,KUSINI,NYANDA ZA JUU,PWANI,DAR ES SALAAM,KASKAZINI,KATI NA BONDE LA UFA.
  5.Wabunge wasiwe mawaziri na kama atateuliwa ateme nafasi ya ubunge.
  6.Madaraka ya Rais yapunguzwe na abaki ya amiri jeshi mkuu.Uteuzi wa nafasi za wakurugenzi ufanywe na bodi zake, na siyo Raisi
  7.Matokeo ya uchaguzi wa Raisi yapingwe mahakamani ndani ya siku 14 baada ya kutangazwa
  8.Wagombea binafsi wa nafasi ya rais,mbunge ,na madawini uruhusiwe.
  9.Mapato ya vyanzo na usimamizi wa bajeti ya serikali za mitaa utamkwe kwenye katiba ambapo ni 50% ya bajeti ya serikali-OC, DEVE,NA PE.
  10. Bunge liwe na wawakilishi wa majimbo na yapunguzwe hadi 150 tu Tanzania na visiwani kuwe na wabunge 10.
  11.Baraza la mawaziri liwe na mawaziri kamili 14 na manaibu 12.
  12.Serikali itoe huduma muhimu kwa wananchi wake kupitia kodi zinazolipwa.
  13. Wananchi kumfukuza kazi mbunge au diwani kupitia vikao maalum vya wananchi.
  14.Raisi kushitakiwa mahakamani bila kikwazo akiwa au baada ya kutoka madarakani kwa matumizi mabaya ya ofsi,madaraka na rushwa
  15.Tume uhuru ya uchaguzi isiyo na upendeleo na vyama na kuthibitishwa wajumbe kwenye baraza la wananchi-wabunge
  16.Kuwa muundo tofauti tuwe na Rais na makamu wa Raisi bila waziri mkuu au kuwa na Rais na waziri mkuu bila kuwa na makamu ili kuondoa ukubwa wa Serikali maana wote wanaonekana ni watendaji tu.
  .......................................etc.etc.
   
 9. m

  muhinda JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2012
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 340
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  1. kitamkwe kama ndio Lugha ya taifa
  2. Mikataba ya madini itoe % ya kwenda kwa wazawa wa eneo yalipogundulika
  3. Viti maalum vipunguzwe au viondolewe kabisa (hatujaona faida yake)
  4. Usalama wa raia (sina uhakika tufanyeje) lakini swala hili liangaliwe kwa mapana yake
   
 10. M

  Mr.kibulala Member

  #10
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wanajf ndio 2ko kwenye uwanja 2nasubiri kutoa maoni,ila ratiba ya tume ni mbovu kwa maeneo kuwa mbli na wananchi
   
 11. brazilian

  brazilian JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 607
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  na mimi haya ndio mapendekezo yangu.
  -HASA MA- DCs na RCs wafutwe
  -Muungano uvunjwe
  -majaji wasiteuliwe na rais
   
 12. brazilian

  brazilian JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 607
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Viti maalumu vya wabunge viondolewe
   
 13. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  1.Rais asiwe nje ya ikulu robo 1/5 ya siku 360
  2.Vyeo kama DC,DED,RC ni vya kisiasa vifutwe kabisa,kuwe na Governor wa mkoa
  3.Tuwe na mamlaka ya kumwadabisha rais pasipo kuingiliwa na chombo chochote
  4.Tume huru ya uchaguzi
  5.Warudishe Azimio la arusha,miiko ya uongozi
   
Loading...