Tume ya Jaji Augustino Ramadhani yaamua naibu Jaji Mkuu avuliwe madaraka!!!

Naibu jaji mkuu wa Kenya apatikana na hatia




6 Agosti, 2012 - Saa 11:18 GMT

Jopo maalum la majaji lililoteuliwa na rais Mwai Kibaki kuchunguza tuhuma zilizokuwa zinamkabili Naibu Jaji Mkuu wa Kenya Nancy Baraza kumdhalilisha mlinzi mmoja katika duka moja kubwa mjini Nairobi, imependekeza, jaji huyo kuondolewa madarakani.

Akisoma hukumu hiyo mjini Nairobi leo, mwenyekiti wa jopo hilo, Jaji mkuu mstaafu wa Tanzania, Augustino Ramadhan, amesema Nancy Baraza akiwa mtumishi wa chombo cha kusimamia sheria na haki hakutakiwa kwa namna yoyote kutenda kosa hilo dhidi ya mlalamikaji Bi Rebecca Kerubo.

Amesema kitendo alichofanya Nancy Baraza na ni cha utomvu mkubwa wa nidhamu na hivyo kupendekeza kwa Rais Mwai Kibaki kumwondoa katika wadhifa wake wa naibu jaji mkuu.

Nancy Baraza alituhumiwa kumnyanyasa na kumpiga Bi Kerubo tarehe 31 Desemba 2011, baada ya kutakiwa kufanyiwa ukaguzi kabla ya kuingia katika duka hilo, utaratibu ambao umekuwa ukitekelezwa kwa wateja wote

BBC Swahili - Habari - Naibu jaji mkuu wa Kenya apatikana na hatia

wangekua wanarecoomend hivi basi hata huku nyumbani tungewapongeza..... amekua hapa tanzania hadi anastaafu, sijui ameacha legacy ipi?
 
Ramadhani mbona huru alikushinda? Baada ya kutoka madarakani ukadai ulishinikizwa na serikali kutoa hukum ulotoa, je tutaamini vipi kibaki hajakushinikiza kutoa hukum hiyo kwa huyo mama!
 
..............and that is why Kenya continues to be superior to Tanzania; Kibaki knows how to govern.
 
du hisroria haitakaa iumsahau kuhusu kesi ya mgombea binafsi
Ni kweli ile kesi ilimuondolea heshima na hata yeye akikumbuka, nafsi inamsuta anajiona kama kama yuko uchi, na zimwi la ile kesi litamfua milele.
 
Lazima tukubali Kenya wako mbele SISI (Tangayika tunafuata nyayo). Sijui Siku Kenya wakidai Lake VICTORIA tunaweza kuwavimbia kama Malawi?. Just thinking aloud.

Kwetu huku VIONGOZI NI MIUNGU WATU. Hivi mnakumbuka ile kesi ya Mlinzi wa bank aliyemwambia Ngereja (wakati huo waziri wa Nishati) atoke ndani ya ATM aongee na simu yake akiwa nje kwasababu kuna wateja wanasubiri huduma?! Masikini kauli hiyo tu ikamponza mlinzi wa watu akafukuzwa kazi, kwa maelekezo ya Ngereja eti amedhalilisha! Bongo ni zaidi ya uijuavyo.
 
Hii haina uhusiano na katiba mpya ya Kenya.

Ni sheria ya Commonwealth. Jaji yeyote hawezi kuondokewa madarakani akifanya makosa mpaka panel ya majaji watatu kutoka nchi za Commonwealth waamue.

Hata Tanzania jaji akivunja sheria itabidi raisi aunde panel ya majaji kutoka nchi za Comminwealth kumhukumu.
 
Ni kesi gani iliyopelekwa mbele yake ambayo mnasema alishindwa kutoa hukumu ya haki?..
Mkuu pamoja na heshima zote ninazompa,

Jaji mkuu mstaafu, alikubali kushikwa masikio na CCM na kupindisha hukumu ya mgombea binafsi. Aliyumba sana pale, akatoa wrong judgement akiwa na jopo la majaji 7.

 
Ya nyumbani yamemshinda anaenda kuwa jaji w kwa jirani.

Aliteuliwa na rais wa Kenya, na hakuwa yeye tu bali kulikuwa na majaji toka nchi zingine - hii ni kutengeneza fairness, kesi ya nyani.... (angalia hukumu za mahakama ya kazi Vs Madaktari VS walimu VS Serikali)
 
Wengi ya watumishi wa serikali ya Tanzania wakitumika mahala pengine huonekana wanafanya vizuri, sijui wanapatwa na Setani gani wanapofanya mambo ya tanzania
 
hapo hakuna utani, huyu mama hakuelewa maana ya katiba mpya kwa WAKENYA, hakuna wa kumlaumu ajilaumu mwenyewe kwa kuleta ukandamizaji mahali pasipostahili. IMEKULA KWAKE
 
ila wakenya wametudhalilisha,jaji mkuu wetu anaenda kuunda tume ya kufatilia madai madogo na ya kijinga kama hayo!!wangemchukua graduate yoyote jobless akaenda kugain experience
 
alikuwa anachagua ma jaji bila vetting, kenya anakuwa na kihelehele!
 
Retired CJ Ramadhani Augustine chaired a Mwai Kibaki judicial commission that has recommended suspended Deputy Chief Justice of Kenyan Supreme Court Nancy Baraza to be removed forthwith in her judicial capacity due to gross misconduct following the confirmation of charges against her. She has 10 days to appeal against the decision........

Safi sana, fundisha sheria hao jirani...:hat:
 
Huyu si ndiye M/kiti wa Tume ya Uchaguzi??? Kama ndiye atende haki pia na kwenye Tume ya Uchaguzi (asichakachue matokeo 2015)
 
The seven-member inquiry team says it found all counts against Baraza to be true, after she assaulted security guard Rebecca Kerubo at the Village Market last year.

Former Tanzanian Chief Justice Augustino Ramadhani who chaired the tribunal says they interviewed all those who witnessed the incident on New Year's Eve.


Source: capitalfmkenya YOUTUBE
 
Last edited by a moderator:
Mwanamuke wa kikenya akipitia shule na kuwa na madaraka wanakuwa na taabu na majivuno sana huwadharau hata wanawake wenzao ambao hawawajafikia hadhi zao,wana jeuri ya kujilinganisha na wanawake wa kizungu,hao ndio wenye mchezo ''chips funga''
 
huyu agustino ramazani si ndio yule aliyekua akilalamika kwamba baada ya kustaafu sirikali ya jk imemnyima ulinzi???!!!!

aangalie yule mkenya taahira asimpeleke mabwepande ohoooooooooooo
 
Back
Top Bottom