Tume ya haki za binadamu na utawala bora yalaani kitendo cha Tundu Lissu kupigwa risasi

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
1,745
4,277
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli
S.L.P 2643, DAR ES SALAAM
Simu: +255 22 2135747/8; 2137125; 2135222
Faksi: +255 22 2111281
B/Pepe: chragg@chragg.go.tz
Tovuti: www.chragg.go.tz
Septemba 8, 2017​



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Tamko la THBUB kuhusu Mhe. Tundu Lissu (Mb) kupigwa risasi
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesitushwa na kusikitishwa na kitendo cha Mhe. Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika kupigwa risasi, tukio lililotokea Septemba 7, 2017 mjini Dodoma.

Tume inalaani vikali kitendo hicho kwani ni kitendo cha uvunjifu mkubwa wa sheria na haki za binadamu.

Tukio hili ambalo limekuja siku chache tu baada ya tukio la ofisi za wanasheria wa IMMMA zilizoko jijini Dar es Salaam kulipuliwa kwa bomu siyo la kawaida, na limeleta hofu siyo kwa familia ya Mhe. Tundu Lissu pekee, bali kwa wananchi wengi nchini.

Isitoshe, matukio haya hayaleti picha nzuri kwa nchi inayoheshimu demokrasia, haki za binadamu na utawala bora.

Hivyo, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora:

1. Inalitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha linakamilisha haraka upelelezi wa tukio hilo na kuwapeleka wahusika katika vyombo vya sheria.

Tume inaamini kuwa iwapo wahusika wa tukio hili watachukuliwa hatua kali itasaidia kukomesha vitendo vya aina hii vinavyofanywa na makundi ya watu wanaojichukulia sheria mkononi ambayo yanaonekana kujitokeza hivi karibuni.

2. Aidha, inapenda kukumbusha kuheshimu haki za binadamu na misingi ya utawala bora na kuepuka ukiukwaji wa Katiba na sheria za nchi.

3. Mwisho, inamtakia Mhe. Tundu Lissu kila la kheri katika matibabu yake ili apone haraka.

Imetolewa na:

(SIGNED)

Mhe. Bahame Tom Nyanduga

Mwenyekiti

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Septemba 8, 2017
 
  • Thanks
Reactions: BAK
"Tume inaamini kuwa iwapo wahusika wa tukio hili watachukuliwa hatua kali itasaidia kukomesha vitendo vya aina hii vinavyofanywa na makundi ya watu wanaojichukulia sheria mkononi ambayo yanaonekana kujitokeza hivi karibuni."

Mshaanza kuwehuka na kitume chenu
 
Risasi 32 kumiminwa ndani ya eneo la Dodoma
Bunduki ya kivita iko mkononi mwa mtu
Viongozi wa juu wa serikali, bunge na mahakama wako Dodoma
Wauaji wamefanya mchana ( waliona jioni itachelewa kufika)

Sawa. Zamu ya Lissu imepita. Waliobaki usalama wao uko wapi ikiwa silaha na risasi nyingi ziko mikononi mwa watu wasiojulikana.
 
Hivi walipomuita Bashite alienda.kweli kwenye ile kesi??

Kama.hakwenda walimfanya nini??Na.kama.hawakumgusa.basi hata hawa hawana moral authority ya kuwaadabisha Polisi. Ni wale wale Tawi la.CCM
 
Hii ni tume ya kuchagua matukio ya kulaani, haikulani wananchi waliovunjiwa nyumba zao ubungo, raia alieuawana polisi akipita njiani pale immigration kisa amefuga ndevu, kuzuia vyama vya siasa kuendesha mikutano ya, kuvamiwa kwa studio ya clouds n.k
kwa mlolongo huu mchache wa matukio ambayo tume hii haijawahi kuonyesha ujasiri wake na kujitokeza hadharani kulaani, ni kielelezo tosha hii tume si lolote si chochote ni tume kibogoyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ashakum si matusi, lakini ukweli hii tume ni ya kipuuzi! Na popote mlipo ujumbe huu uwafikie. Nyie ni wazandiki na wanafiki wakubwa sana!

Katika matukio yote ya kupigwa risasi, sawa na hili la Lissu, kule Kibiti hamkuwahi kutoa tamko hata moja! Watoto wadogo wametekwa na kuuwawa kinyama Arusha, mko kimya kama maboga! Zaidi ya hayo yapo matukio mengi tu huwa hamtoi hayo mnayoita matamko. Why Lissu? Ni binadam sana kuliko watanzania wengine?! Mna double standards na wanafiki msio maana!

Sent from Moto G
 
Back
Top Bottom