Tume huru ya uchaguzi ndiyo dawa Tanzania

Soweto2006

Member
May 8, 2021
45
208
Tumefatilia suala la Ole Sabaya kwa undani. Alichaguliwa na mamlaka za teuzi zilizochaguliwa na wananchi.

Tatizo lililopo Tanzania kwa sasa sio wakuu wa Mikoa au wilaya, tatizo ni kupata viongozi wanaostahili kuongoza nchi kwa mujibu wa uelewa wa Watanzania.

Manake ni kwamba kabla hatujachagua kiongozi tunakuwa tunamjua na kumfahamu, tumeishi naye sana.

Kitendo cha wananchi kuchagua viongozi halafu watu wachahce wanabadilisha ndiyo linatokea jambo la kuletewa mtu kama Sabaya.

Hapo Tanzania tunaamini wapinzani wa kweli ni Chadema, tunaishauri ipambane sana kwenye swala la tume huru ya uchaguzi, hayo mengine ya kupambana Sabaya atoke ni kupoteza muda.

Sabaya aliteuliwa na watu waliongizwa madarakani kinyume na taratibu, mfumo ubomolewe tupate viongozi halali wanaofaa kuongoza nchi, dawa ni tume huru ya uchaguzi.
 
Katiba pendekezwa ya warioba ilifuta hivyo vyeo vya kisiasa.
Kwa mtazamo wangu tume huru inaweza kupatikana bila katiba mpya, namaanisha kwamba swala la katiba ni ngumu na CCM hawapo tayari bora mapambano yaelekezwe kwenye tume huru, linaonekana ni jambo dogo lakini litaleta mabadiliko makubwa.
 
Tume ipo kwenye katiba Mkuu ,hauwezi kupata TUME Huru bila kufanya changes kwenye katiba...sasa kwanini ufanye nusu nusu wakati katiba nzima inatakiwa ifanyiwe changes?
 
Tumefatilia swala la Ole Sabaya kwa undani. Alichaguliwa na mamlaka za teuzi zilizochaguliwa na wananchi.

Tatizo lililopo Tanzania kwa sasa sio wakuu wa Mikoa au wilaya, tatizo ni kupata viongozi wanaostahili kuongoza nchi kwa mujibu wa uelewa wa Watanzania.

Manake ni kwamba kabla hatujachagua kiongozi tunakuwa tunamjua na kumfahamu, tumeishi naye sana.

Kitendo cha wananchi kuchagua viongozi halafu watu wachahce wanabadilisha ndiyo linatokea jambo la kuletewa mtu kama Sabaya.

Hapo Tanzania tunaamini wapinzani wa kweli ni Chadema, tunaishauri ipambane sana kwenye swala la tume huru ya uchaguzi, hayo mengine ya kupambana Sabaya atoke ni kupoteza muda.

Sabaya aliteuliwa na watu waliongizwa madarakani kinyume na taratibu, mfumo ubomolewe tupate viongozi halali wanaofaa kuongoza nchi, dawa ni tume huru ya uchaguzi.
To make matter even worse,viongozi wa kuumuliwa hawataki hata maendeleo ya nchi
 
Kama ilivyo ada nawasalimu kwa jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania .Mimi Kama mkereketwa wa siasa za nchi yangu nimeona sio mbaya nikawakumbusha ndugu zangu hawa.Huu ndo ulikua muda sahihi wakuanza kudai Katiba mpya,tume HURU ya uchaguzi ili uchaguzi ujao wasiwe tena na malalamiko ya kuibiwa kura au kuporwa uchaguzi Kama wanavyoita.Ndugu zangu Hawa kitu Cha kushangaza Sasa ivi wako busy kuipa maelekezo TAKUKURU wachukue hatua dhidi ya watu flani wakizani hao ndo tatizo lililowafanya washindwe kushika dola . CHADEMA tatizo sio makonda Wala sabaya
 
Hivi wewe mtanzania una elimu ya Uraia kweli?
Ni Nani aliekufundisha kuwa suala la Katiba,au katiba mpya Ni la Chadema?
Au Ni Nani aliekufundisha kuwa suala hilo ni la vyama vya Siasa?
Ndugu yangu Mtanzania,suala la Katiba,au katiba mpya Ni la watanzania wote,dini zote,kabila zote na Jamii zote,ni la wakulima,wafanyakazi na wafanyabiashara,ni la vijana na wazee,wakubwa na wanafunzi.
Kwa ufupi Ni la watanzania wote,bila kujali vyama,amka wewe.
Acha kukaliili maneno.
 
Siyo rahisi hivyo lazima kuwe na Elimu na awareness kwa jamii nzima, binafsi nchi yetu naona hilo swala si rahisi sana maana tabaka tawala linanufaika na katiba iliyopo, na watawaliwa bado wako gizani kabisa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom