GE2025 Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi yawateua Samia na Nchimbi kugombea urais kwa tiketi ya CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewateua Rais Samia Suluhu Hassan na mgombea mwenza wake, Dk Emmanuel Nchimbi, kugombea nafasi ya urais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.

Akizungumza leo Jumatano, Agosti 27, 2025 jijini Dodoma, Mwenyekiti wa INEC, Jaji Mstaafu Jacobs Mwambegele, amesema wagombea waliopendekezwa na CCM wametimiza masharti yote ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo kuthibitishwa rasmi kuwania nafasi hizo.

Soma pia: Utaratibu uliotumiwa na CCM Kumpitisha Samia Kugombea Urais 2025 Umetengeneza Dangerous Precedent Kwa Chama!

“Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inawateua Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dk Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Jaji mstaafu Mwambegele.

Uteuzi huo unawafanya Samia na Nchimbi kuingia rasmi katika kinyang’anyiro cha urais kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu ambao kampeni zake zinatarajiwa kuanza kesho Agosti 28, 2025.
 
Hamna Haja ya uchaguzi, wapewe tu wanachokitaka CCM.
 
View attachment 3454611

“Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inawateua Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dk Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Jaji mstaafu Mwambegele.

Uteuzi huo unawafanya Samia na Nchimbi kuingia rasmi katika kinyang’anyiro cha urais kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu ambao kampeni zake zinatarajiwa kuanza kesho Agosti 28, 2025.
Lolote baya liwakute wote kabla ya October.
 
SAFI SANA CCM MBELEKWAMBELE TUNASONGA MBELE MASKINI LUHAGA MPINA CHALIIIIIIIIIIIIIIIII
 
Samia na Salum Wazanzibari wanaogombea rais wa Tanganyika baada ya kumfungia Mtanganyika gerezani.
 
Kwaio yeye atagombea na mwandishi wa habari salumu ? 🤣🤣🤣🍺
 
Hawajakidhi Kigezo Cha Wadhamini Hao,ni Uhuni Huo.
Halafu Tume(INEC) Huwa Inapitisha Au Inateua Wagombea ? Kwani Ilikuwa Na Option Ya Kuwateua Wengine Zaidi Ya Hao Ndani Ya CCM?
 
Back
Top Bottom