PreGE2025 Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi INEC, yaanza uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu la pili

PreGE2025 Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi INEC, yaanza uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu la pili

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Nipe Maji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
335
Reaction score
190
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi INEC Jaji Jacob Mwambegele amesema tume hiyo imeanza awamu ya pili ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ikihusisha mikoa 15 mzunguko wa kwanza huku huku akiwataka wananchi ambao hawakuboresha taarifa zao awamu ya kwanza watumie nafasi hiyo kuboresha taarifa zao.
 
View attachment 3322605

Tanzania hakuna Tume Huru ya Uchaguzi.

Kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT, inatambua uwepo wa Tume ya Uchaguzi, yaani NEC LAKINI siyo Tume Huru ya Uchaguzi (INEC). INEC kwa mujibu wa Ibara hiyo ya Katiba ni Kitu BATILI kwani haitambuliki na Katiba. Marekebisho ya jina la Tume ya Uchaguzi kutoka NEC kwenda INEC yalipaswa kutanguliwa na Marekebisho ya Katiba iliyopo kwanza, hususani Ibara hiyo ya 74.

Katiba inasema kwamba kutakuwa na Tume ya Uchaguzi wala siyo Tume Huru ya Uchaguzi. Mabadiliko haya ya Sheria ya Uchaguzi yaliyosababisha kubadilisha jina la Tume ya Uchaguzi kutoka NEC kwenda INEC ni BATILI kwa mujibu wa Ibara hiyo ya 74 kwani Mabadiliko haya yanakinzana na matakwa ya Katiba ya nchi.

Kwa maana hiyo, Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC) ni Taasisi au kitu ambacho hakitambuliki na Katiba ya nchi hivyo ni BATILI KWA UJUMLA WAKE. Taasisi hiyo haitambuliki kisheria kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT.
 
Tanzania hakuna Tume Huru ya Uchaguzi.

Wajinga hao, wanapoteza pesa, waendelee kutawala tu, sisi hatuhangaiki na uchaguzi wa hovyo.
CCM wanajua wanaochukia uchaguzi ni watu wa Chadema au upinzani, lah si hivyo, kwanza watanzania wengi hawana vyama, ni wachache sana ndo wanachama wa Chama flani. Wengi wapiga kura hatuna Chama, Bali tunapenda haki na tutachagugua yoyote yule awe CCM , act au Chadema, Ili mradi mchezo Uwe huru
 
Back
Top Bottom