Tume: Hakuna gharama kuendesha Serikali tatu

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,483
Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, imewabeza watu, hususan wanasiasa wanaosimama majukwaani kueleza Muundo wa Muungano wa Serikali tatu utaongeza gharama za kiuendeshaji kuwa ni uongo na sababu hizo hazina tija.
Mjumbe wa Tume hiyo, Humphrey Polepole alisema hayo jana wakati wa mkutano wa kuijadili Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba Mpya mbele wa Wajumbe wa Baraza la Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara.
Alisema Muundo wa Serikali tatu hauna gharama zozote kwani chanzo cha mapato cha kuongoza Serikali ya Muungano kuwa tayari kimebainishwa.
Polepole alisema gharama za kuongoza Serikali hiyo zitatokana na Kodi ya Ushuru wa Bidhaa ambapo jumla yake zinazokusanywa si chini ya Sh1 trilioni.
"Mpaka sasa Serikali ya Muungano inakusanya zaidi ya Sh3 trilioni hivyo kama itatumika Sh1 trilioni na zitakazobaki zitaelekezwa katika shuguli zingine, fedha zitakuwepo," alisema Polepole na kuongeza:
"Nashangaa wanasiasa wanaosimama majukwaani kueleza wananchi kuwa kutakuwa na mzigo wa gharama, hii si kweli kwani Tume tumekwisha bainisha chanzo chake cha mapato na hao wanaozungumza hayo hawafuatilii mchakato kwa umakini."
Alisema uchambuzi walioufanya juu ya kodi inayokusanywa mwaka 2003/04 zilikusanywa jumla ya Sh500 bilioni na mwaka 2011/12 zilikusanywa Sh1 trilioni ambapo kila mwaka mapato hayo yanaongezeka.
"Uzoefu unaonyesha kila mwaka mapato yanaongezeka hivyo uwepo wa Muungano wa Serikali tatu ni dhahiri hautaathiri kitu chochote na utasaidia kutatua kero zilizopo zinazojitokeza kila mwaka kila kukicha," alisema Polepole
Polepole aliwataka Wananchi kutokuwa na shaka na mapendekezo hayo ya Tume juu ya Muundo wa Muungano kuwa wa Serikali tatu kwani utapunguza malalamiko ya muda mrefu yaliyopo.
"Hivi sasa kuna kero zaidi ya 47 na kwa Muungano huu uliopo hautamaliza na wala hauwezi kuyafanyia kazi lakini kutokana na mapendekezo ya Tume ya Serikali tatu ninahakika yatapungua na kila upande kutokuwa na malalamiko," alisema Polepole.
Polepole amesisitiza kwa kuwaomba wananchi kuendelea kutoa maoni katika hali ya kutoshinikizwa kwa namna yoyote.
"Kila mtu anapaswa kuwa huru kutoa maoni yake bila kuogopa chochote. Lengo la uwepo wa katiba mpya ni kujua hitaji hasa la wananchi ni nini na kwamba katika kutoa maoni wananchi wanapaswa kufanya hivyo bila woga," alisisitiza Polepole.
Baadhi ya watu wengine walioshiriki kwenye tukio hilo waliomba Tume ya Katiba kuangalia namna ya kufanya ili hatimaye kweli Katiba itakayopatikana iwe ni kwa ajili ya wengi, si zaidi.
Walisema kwamba kuna watu wamekuwa maoni ambayo mengine yanaweza kuonekana kutokuwa na masilahi kwa baadhi ya vyama au viongozi, ni suala la msingi sana kufanya kila wanaloweza kuhakikisha kuwa maoni ya wengi yanazingatiwa ili hata watu wawe na wepesi katika kuzingatia yale ambayo yatakuwemo kwenye Katiba hiyo.
Ni wazi kwamba ikiwa katiba itazingatiwa vizuri kwa maana ya kujali wanachosema wananchi, hakutakuwa na ugumu wa kuitekeleza

Source Star tv,akizungumza sasa hivi kupitia kipindi cha tuongee asubuhi mh .Wenje ameitaka CCM kutokupotosha wananchi kuhusu gharama za serikali tatu akitoa mfano kwa serikali ya sasa ya CCM anasema ina mawaziri zaidi ya 30 na manaibu waziri 35 ambapo hata ndani ya baraza la mawaziri wa sasa kuna waziri wa wizara isiyo maalumu,pia kuna makamu wa rais watatu3 wabunge wa sasa wa bunge la Jamhuri wapo 357 je hizi sio gharama kubwa anasema ni vyema CCM wakaja na majibu tofauti haiwezekani leo ccm wakasema kuhusu gharama za serikali wakati wao wana serikali kubwa kuliko iliyopendekezwa katika Rasimu ya sasa,Mh Wenje anawataka Watanzania kuwa makini na muongozo uliotolewa na ccm kwani umepinga mambo mengi ya misingi ambayo tume ya katiba imeyapendekeza kwenye Rasimu mpya .
 
Maswala mengine ya wananchi katiba mpya itapatikana tu tena itakuwa nzuri.
 
Hakuna harama kweli ,alivyofanya Mh Warioba ni kupunguza harama kwa vigogo wa ccm kuwatowa tonge mdomoni. kati ya mawaziri 80 kuwapunguza kuwa 15 kwa wizara 7 za Muungano? hivyo mimi nasema hao kumi na 15 ni wengi kwa mambo 7 ya Muungano. Jee kuondosha Wabunge 300 na kufanya wabunge 70 nikupunguza harama au kuongeza?. Kama ni harama basi ilikuwa ni Serekali ya Zanzibar lakini hivi sasa itakuwa kila upande wa Serekali una mambo yake ispokuwa yale 7 ya Muungano tu. Kama ilikuwa kuibebe Zanzibar ni mzigo sasa naituliwe .
 
Wanaosema Serikali 2 iendelee au Serikali 1 basi ni MAPIMBI hayo
 
Bado nina wasiwasi na haya mabaraza ya wilaya kwani yalihodhiwa na CCM na wamepewa maelekezo maalum kuwa kinyume na hii rasimu.
 
I don't really care about 1 or 2, I want to see my Tanganyika and Mgombea binafsi.
 
Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, imewabeza watu, hususan wanasiasa wanaosimama majukwaani kueleza Muundo wa Muungano wa Serikali tatu utaongeza gharama za kiuendeshaji kuwa ni uongo na sababu hizo hazina tija.
Mjumbe wa Tume hiyo, Humphrey Polepole alisema hayo jana wakati wa mkutano wa kuijadili Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba Mpya mbele wa Wajumbe wa Baraza la Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara.
Alisema Muundo wa Serikali tatu hauna gharama zozote kwani chanzo cha mapato cha kuongoza Serikali ya Muungano kuwa tayari kimebainishwa.
Polepole alisema gharama za kuongoza Serikali hiyo zitatokana na Kodi ya Ushuru wa Bidhaa ambapo jumla yake zinazokusanywa si chini ya Sh1 trilioni.
“Mpaka sasa Serikali ya Muungano inakusanya zaidi ya Sh3 trilioni hivyo kama itatumika Sh1 trilioni na zitakazobaki zitaelekezwa katika shuguli zingine, fedha zitakuwepo,” alisema Polepole na kuongeza:
“Nashangaa wanasiasa wanaosimama majukwaani kueleza wananchi kuwa kutakuwa na mzigo wa gharama, hii si kweli kwani Tume tumekwisha bainisha chanzo chake cha mapato na hao wanaozungumza hayo hawafuatilii mchakato kwa umakini.”
Alisema uchambuzi walioufanya juu ya kodi inayokusanywa mwaka 2003/04 zilikusanywa jumla ya Sh500 bilioni na mwaka 2011/12 zilikusanywa Sh1 trilioni ambapo kila mwaka mapato hayo yanaongezeka.
“Uzoefu unaonyesha kila mwaka mapato yanaongezeka hivyo uwepo wa Muungano wa Serikali tatu ni dhahiri hautaathiri kitu chochote na utasaidia kutatua kero zilizopo zinazojitokeza kila mwaka kila kukicha,” alisema Polepole
Polepole aliwataka Wananchi kutokuwa na shaka na mapendekezo hayo ya Tume juu ya Muundo wa Muungano kuwa wa Serikali tatu kwani utapunguza malalamiko ya muda mrefu yaliyopo.
“Hivi sasa kuna kero zaidi ya 47 na kwa Muungano huu uliopo hautamaliza na wala hauwezi kuyafanyia kazi lakini kutokana na mapendekezo ya Tume ya Serikali tatu ninahakika yatapungua na kila upande kutokuwa na malalamiko,” alisema Polepole.
Polepole amesisitiza kwa kuwaomba wananchi kuendelea kutoa maoni katika hali ya kutoshinikizwa kwa namna yoyote.
“Kila mtu anapaswa kuwa huru kutoa maoni yake bila kuogopa chochote. Lengo la uwepo wa katiba mpya ni kujua hitaji hasa la wananchi ni nini na kwamba katika kutoa maoni wananchi wanapaswa kufanya hivyo bila woga,” alisisitiza Polepole.
Baadhi ya watu wengine walioshiriki kwenye tukio hilo waliomba Tume ya Katiba kuangalia namna ya kufanya ili hatimaye kweli Katiba itakayopatikana iwe ni kwa ajili ya wengi, si zaidi.
Walisema kwamba kuna watu wamekuwa maoni ambayo mengine yanaweza kuonekana kutokuwa na masilahi kwa baadhi ya vyama au viongozi, ni suala la msingi sana kufanya kila wanaloweza kuhakikisha kuwa maoni ya wengi yanazingatiwa ili hata watu wawe na wepesi katika kuzingatia yale ambayo yatakuwemo kwenye Katiba hiyo.
Ni wazi kwamba ikiwa katiba itazingatiwa vizuri kwa maana ya kujali wanachosema wananchi, hakutakuwa na ugumu wa kuitekeleza
Mimi nakubaliana sasa na muundo huu wa serikali tatu kwa ushauri wa kuwa na Rais mmoja wa Muungano kwa mambo ya muungano tu. Huendeshaji wa serikali hiyo uwe ni kwa serikali za Zanzibar na Tanganyika kuchangia kwa uwiano wa kiuchumi. Serikali tatu kwa nchi yenye uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi hazina gharama yoyote. Mbona tunaongeza idadi ya serikali za mikoa na wilaya kila mwaka? Wajumbe wa mabaraza ya katiba wengi wamebeba mawazo ya vyama vyao, hivyo naiomba tume iangalie maoni yao mara mbili ili wasije kufanya masahihisho ya rasimu ambayo baadaye wananchi tutaikataa kwa kura za maoni.
 
Wanaosema serikali 3 ni gharama hawasemi ni kwa nini isiwe 1 badala ya Serikali kama hoja ni gharama

Mkuu Ben wanaoendeleza ajenda ya kuwa serikali 3 ni gharama ni CCM ili ku-justify serikali mbili. Lakini ukweli ni kuwa "issue" sio idadi ya serikali, suala hapa ni muungano, na kwa kweli bila kufikia "muafaka" wa serikali moja ni bora kuvunja tu huu muungano sasa, "options" zingine zote serikali 2 au 3 ni njia ndefu tu ya kuuvunja muungano. Period!!!
 
Wanaosema serikali 3 ni gharama hawasemi ni kwa nini isiwe 1 badala ya Serikali kama hoja ni gharama
Ben Saanane do you know anything as to why we cannot have two states? I mean free Tanganyika and Free Zanzibar?
 
Last edited by a moderator:
Hawa watu ni mazuzu,wanalalamika serikali tatu ni gharama,lakini hawaoni gharama ya kuongeza mikoa na wilaya kila uchao!!!"GO TO HELL CCM".
 
Hawa watu wa tume ya katiba wajikite kwenye kitu wanachokijua ambacho ni sheria. Huyu anayesema gharama hazitaongezeka kwa sababu kuna mapato mapya, hajui anazungumza nini. Kwa jinsi alivyotoa majibu yake ameonyesha ya kuwa gharama zitaongezeka! Kuwa na vyanzo vingine vya mapato sio sababu ya kutokusema ya kuwa gharama hazitaongezeka. Naona Kiswahili kimekuwa kigumu sana siku hizi.
 
Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, imewabeza watu, hususan wanasiasa wanaosimama majukwaani kueleza Muundo wa Muungano wa Serikali tatu utaongeza gharama za kiuendeshaji kuwa ni uongo na sababu hizo hazina tija.

Mjumbe wa Tume hiyo, Humphrey Polepole alisema hayo jana wakati wa mkutano wa kuijadili Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba Mpya mbele wa Wajumbe wa Baraza la Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara.

Alisema Muundo wa Serikali tatu hauna gharama zozote kwani chanzo cha mapato cha kuongoza Serikali ya Muungano kuwa tayari kimebainishwa.

Polepole alisema gharama za kuongoza Serikali hiyo zitatokana na Kodi ya Ushuru wa Bidhaa ambapo jumla yake zinazokusanywa si chini ya Sh1 trilioni.

“Mpaka sasa Serikali ya Muungano inakusanya zaidi ya Sh3 trilioni hivyo kama itatumika Sh1 trilioni na zitakazobaki zitaelekezwa katika shuguli zingine, fedha zitakuwepo,” alisema Polepole na kuongeza:

“Nashangaa wanasiasa wanaosimama majukwaani kueleza wananchi kuwa kutakuwa na mzigo wa gharama, hii si kweli kwani Tume tumekwisha bainisha chanzo chake cha mapato na hao wanaozungumza hayo hawafuatilii mchakato kwa umakini.”

Alisema uchambuzi walioufanya juu ya kodi inayokusanywa mwaka 2003/04 zilikusanywa jumla ya Sh500 bilioni na mwaka 2011/12 zilikusanywa Sh1 trilioni ambapo kila mwaka mapato hayo yanaongezeka.

“Uzoefu unaonyesha kila mwaka mapato yanaongezeka hivyo uwepo wa Muungano wa Serikali tatu ni dhahiri hautaathiri kitu chochote na utasaidia kutatua kero zilizopo zinazojitokeza kila mwaka kila kukicha,” alisema Polepole

Polepole aliwataka Wananchi kutokuwa na shaka na mapendekezo hayo ya Tume juu ya Muundo wa Muungano kuwa wa Serikali tatu kwani utapunguza malalamiko ya muda mrefu yaliyopo.

“Hivi sasa kuna kero zaidi ya 47 na kwa Muungano huu uliopo hautamaliza na wala hauwezi kuyafanyia kazi lakini kutokana na mapendekezo ya Tume ya Serikali tatu ninahakika yatapungua na kila upande kutokuwa na malalamiko,” alisema Polepole.

Polepole amesisitiza kwa kuwaomba wananchi kuendelea kutoa maoni katika hali ya kutoshinikizwa kwa namna yoyote.

“Kila mtu anapaswa kuwa huru kutoa maoni yake bila kuogopa chochote. Lengo la uwepo wa katiba mpya ni kujua hitaji hasa la wananchi ni nini na kwamba katika kutoa maoni wananchi wanapaswa kufanya hivyo bila woga,” alisisitiza Polepole.

Baadhi ya watu wengine walioshiriki kwenye tukio hilo waliomba Tume ya Katiba kuangalia namna ya kufanya ili hatimaye kweli Katiba itakayopatikana iwe ni kwa ajili ya wengi, si zaidi.

Walisema kwamba kuna watu wamekuwa maoni ambayo mengine yanaweza kuonekana kutokuwa na masilahi kwa baadhi ya vyama au viongozi, ni suala la msingi sana kufanya kila wanaloweza kuhakikisha kuwa maoni ya wengi yanazingatiwa ili hata watu wawe na wepesi katika kuzingatia yale ambayo yatakuwemo kwenye Katiba hiyo.

Ni wazi kwamba ikiwa katiba itazingatiwa vizuri kwa maana ya kujali wanachosema wananchi, hakutakuwa na ugumu wa kuitekeleza.
 
Hajui alisemalo. Katika maelezo yake anasema kuna vyanzo vya mapato wamesha vianisha kwa ajili ya uendeshaji wa serikali hiyo. Hivi vyanzo havitoki hewani bali vitamegwa kutoka katika vyanzo vya Tanganyika na Zanzibar. Hii ndiyo gharama inayozungumziwa.
 
Tuna serikali mbili, mbona gharama yake ni kubwa mpaka mnakopa fedha ya kulipa mishahara ya watumishi wa umma kwa kina Rostam

Nyambaf kabisa, fedha ya serikali inaendesha shughuli za ccm mpaka mnashindwa hadi kununua madawa hospitalini, watoto hawana madawati nk!...

Mgekuwa mnajua kuwa serikali tatu ni gharama mbona mnatuingiza hasara kuweka mikatab ya kijinga kwenye madini,kuiba wanyama wetu, kurulipisha kodi walala hoi na kuwasamehe matajiri na makampuni?...

Waranzania mnatufanya makuwadi eti?..
 
halafu nyie mnaosema serikali 3 ni gharama mbona mikoa inagawanywa kila uchao, hamuoni serikali ya sasa ndio inatumia gharama zaidi!
 
haya maoni ya tume nimeyapenda sana maana hayabainishi nini kitatokea endapo muungano wa serikali tatu utashindwa kujibu hizo kero 47 za muungano. Hapo tu mie ndio nimepapenda.

Kiundani sana tuna serikali tatu moja ikiwa sio rasmi. Kwa mfano waziri wa nishati na madini wa Tanganyika au JMT
 
Back
Top Bottom