Tume: Hakuna gharama kuendesha Serikali tatu

Tume: Hakuna gharama kuendesha Serikali tatu

Haki kwa kila mtz, taasisi na mabaraza halali ya katiba kutoa maoni, magaidi mnaoona ccm haina haki hiyo mnajidanganya. Ni sawa na kujitekenya kisha kujichekesha mwenyewe, kelele zenu ni upuuzi mtupu. Tumieni forum mnaopata kutoa maoni sio kuponda maoni ya wengine. Look at you

inaonekana unamsongo wa mawazo sana...poleni sana chama cha wauza dawa za kulevya..
 
Huyu jamaa ni mashine, ni jembe. Aliyemfuatilia leo star tv amepata mengi mazuri.
Ombi langu kwa star tv ni kurudiwa kwa kipindi hiki cha leo hata mara tatu na wajenge utaratibu wa vipindi vinavyorushwa LIVE kama hiki kuwa vinarudiwa kwani wapenzi wengi wa star tv wanakosa muda wa kuvifuatilia vinaporushwa LIVE.
Naamin hata vcd zake wakiamua kuziuza zitapata soko kubwa sana.
 
Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, imewabeza watu, hususan wanasiasa wanaosimama majukwaani kueleza Muundo wa Muungano wa Serikali tatu utaongeza gharama za kiuendeshaji kuwa ni uongo na sababu hizo hazina tija.
Mjumbe wa Tume hiyo, Humphrey Polepole alisema hayo jana wakati wa mkutano wa kuijadili Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba Mpya mbele wa Wajumbe wa Baraza la Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara.
Alisema Muundo wa Serikali tatu hauna gharama zozote kwani chanzo cha mapato cha kuongoza Serikali ya Muungano kuwa tayari kimebainishwa.
Polepole alisema gharama za kuongoza Serikali hiyo zitatokana na Kodi ya Ushuru wa Bidhaa ambapo jumla yake zinazokusanywa si chini ya Sh1 trilioni.
“Mpaka sasa Serikali ya Muungano inakusanya zaidi ya Sh3 trilioni hivyo kama itatumika Sh1 trilioni na zitakazobaki zitaelekezwa katika shuguli zingine, fedha zitakuwepo,” alisema Polepole na kuongeza:
“Nashangaa wanasiasa wanaosimama majukwaani kueleza wananchi kuwa kutakuwa na mzigo wa gharama, hii si kweli kwani Tume tumekwisha bainisha chanzo chake cha mapato na hao wanaozungumza hayo hawafuatilii mchakato kwa umakini.”
Alisema uchambuzi walioufanya juu ya kodi inayokusanywa mwaka 2003/04 zilikusanywa jumla ya Sh500 bilioni na mwaka 2011/12 zilikusanywa Sh1 trilioni ambapo kila mwaka mapato hayo yanaongezeka.
“Uzoefu unaonyesha kila mwaka mapato yanaongezeka hivyo uwepo wa Muungano wa Serikali tatu ni dhahiri hautaathiri kitu chochote na utasaidia kutatua kero zilizopo zinazojitokeza kila mwaka kila kukicha,” alisema Polepole
Polepole aliwataka Wananchi kutokuwa na shaka na mapendekezo hayo ya Tume juu ya Muundo wa Muungano kuwa wa Serikali tatu kwani utapunguza malalamiko ya muda mrefu yaliyopo.
“Hivi sasa kuna kero zaidi ya 47 na kwa Muungano huu uliopo hautamaliza na wala hauwezi kuyafanyia kazi lakini kutokana na mapendekezo ya Tume ya Serikali tatu ninahakika yatapungua na kila upande kutokuwa na malalamiko,” alisema Polepole.
Polepole amesisitiza kwa kuwaomba wananchi kuendelea kutoa maoni katika hali ya kutoshinikizwa kwa namna yoyote.
“Kila mtu anapaswa kuwa huru kutoa maoni yake bila kuogopa chochote. Lengo la uwepo wa katiba mpya ni kujua hitaji hasa la wananchi ni nini na kwamba katika kutoa maoni wananchi wanapaswa kufanya hivyo bila woga,” alisisitiza Polepole.
Baadhi ya watu wengine walioshiriki kwenye tukio hilo waliomba Tume ya Katiba kuangalia namna ya kufanya ili hatimaye kweli Katiba itakayopatikana iwe ni kwa ajili ya wengi, si zaidi.
Walisema kwamba kuna watu wamekuwa maoni ambayo mengine yanaweza kuonekana kutokuwa na masilahi kwa baadhi ya vyama au viongozi, ni suala la msingi sana kufanya kila wanaloweza kuhakikisha kuwa maoni ya wengi yanazingatiwa ili hata watu wawe na wepesi katika kuzingatia yale ambayo yatakuwemo kwenye Katiba hiyo.
Ni wazi kwamba ikiwa katiba itazingatiwa vizuri kwa maana ya kujali wanachosema wananchi, hakutakuwa na ugumu wa kuitekeleza

Mimi nadhani si jukumu la tume kutetea/kulazimisha uwepo wa serikali 3 au ngapi! wao walishapokea maoni ya wananchi na kuandaa rasimu, sasa wawaache wananchi mbalimbali waendelee kutoa maoni juu ya rasimu hiyo na hatimae kupata katiba waitakayo!
Suala hili la muungano na mfumo wa serikali 1 au 2 au 3 lisiwatoe kwenye majukumu yao ya msingi, wamshauri raisi kuumaliza ubishani huu kwa wananchi kupiga kura ya maoni!
 
Hiv kwanini mods kaondoa ile mada ya sita??
 
Yeyote anayesema serikali 3 ni gharama analinganisha na nn?atoe mchanganuo na si ubabaishaji.
Mbona serikali 2 tulizonazo ndio gharama kuliko 3?
serikali 2 zimezalisha kero za muungano.
Vyama vinavyolisha maneno wajumbe wa mabaraza ya katiba hawavunji sheria?
Katiba itakayo buniwa haitapingwa mahakamani na LHRC/TLS?
Wajumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba wawaelimishe wajumbe wa mabaraza waache kulishwa maneno na badala yake wachangie mawazo ya wanachi na kuboresha mawazo mazuri ya wananchi yaliyopo kwenye rasmu ya awali
 
Back
Top Bottom