Wadau yamkini mimi ni mjinga, naomba mnijulishe kwa sasa huku niliko kuna mijadala moto moto juu ya dhana hii ya kutumbua majipu na usiri wa vikao vya bunge gizani.
Kuna watu wanasema eti, falsafa ya sasa ya kutumbua majipu ina walakini. Wanadai, vipele na chunusi ndivyo vinatumbuliwa, ila havijatumbuka kabisa. Kwa upande wa majipu eti yenyewe yamebaki kuwasha tu, hivyo, hukunwa.
Nikabaki kushangaa, vipele ni nini na majipu ni nini?
Eti, kujilipa TZS 40m ni kichunusi. Afisa Ardhi kumiliki viwanja, rushwa wahamiaji haramu, wafanyakazi hewa.
Bali, Majipu ni Tegeta Escrow Account, Meremeta, EPA, TZs 231bn za Wizara ya Ujenzi, Mikataba ya Madini, gesi na mafuta, miradi ya ujenzi (mfano, daraja la Nyerere), UDA, Lugumi, Uzwaji nyumba za serikali, Fedha za wakubwa ughaibuni (Australia, Uswisi nk)
Tafadhali, tuelimishane tupeane mwanga.