Dr. ukiona Majipu yameisha basi tumbua hata Upele/Vijipu Uchungu. Usibaki Idle

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,523
24,010
Ni muda mrefu toka tumekaa hapa kwenye benchi tukisubiria folen ya kuingia kumwona Dr. Masaa moja na dk kadhaa lililopita aliingia Dr. Akiwa amekunja uso na zana zake za kazi.

Mara wagonjwa wakaanza kuingia mmoja baada ya mmoja. Zilisikika kelele nyingi na kufuatiwa na ukimya. Halafu akatoka mgonjwa macho mekundu kabisa akiwa amenyong'onyea. Walipita kama watatu Uvumilivu ukanishinda nikaona nimuulize nurse kuna nini kinatokea humo ndani. Alinijibu kwa upole" Dr. Katoka Chuo Mtaalam wa kutumbua majipu ndo anawatumbua watu humo ndani"

Nikamwambia "ila mi sina jipu nina ulcers /vidonda vya tumbo kwa sababu ya kutokula na pia mawazo"
Akanijibu tu nisubiri awahudumie wenye majipu. Basi nikaendelea kusubiri na wenzangu pale kwenye benchi. Nikaona wengine wakipita kuingia ndani wenye saratani. Kukawa tu kimya wakatoka wakitabasamu. Nasikia walipewa dawa za kutuliza maumivu. Hawa hawakuonekana kama ni tatizo kubwa. Hivyo Dr. Aliwapa dawa tu za kutuliza maumivu na kuwapatia ushaur akaagana nao.

Halii iliendelea mpaka muda mrefu kukawa kimya sana. Baadaye wakaja jamaa kadhaa na ndugu yao wamemshika akiugulia kwa maumivu akaingia ndani. Huyu bwana alionekana ana uvimbe mkubwa umeiva katika ya paji lake la uso. Kiukwel jipu lake lilikaa sehemu mbaya sana.

Basi akalazimishwa kuingia ndani kwa Dr. Kukawa kimya sana. Ulipita muda mwingi sana kukiwa kimya. Mara mlango ukafunguliwa tukamwona yule mgonjwa akitoka na nduguze waliokuwa wamehuzunika ila mgonjwa akiwa na furaha akiongea na Dr akisindikizwa nje. Inasemekana Dr. Hakuona kama lile ni Jipu. Alisema ni chunusi/kipele tu wala hakina shida. Kitapotelea ndani kwa ndani akaruhusiwa.

Tukaendelea kukaa kwenye benchi. Muda ulizid kwenda Dr. Akiwa tu ofisini lkimya. Sisi wenye matatizo mengine hatukuruhusiwa kwenda wanasema Dr. Alikuwa amesomea tu kutumbua majipu. Nikapata wazo kumshauri basi sasa aanze kutumbua hata Vipele, Chunusi na Vijipu Uchungu. Asibaki kuwa idle. Wazungu wanasema " an iidle mind is the workshop of the devil"
 
Majipu mengine yanatokea sehemu mbaya mkuu...just imagine jipu limetokea kwenye mning'inio wa ngozi ya p*mb* utalipasuaje?ni kulisubiri tu hadi litakapopata pa kuhamia na ndo mategemeo ya wengi kuhusu huyu doctor na huyu mgonjwa wake mwenye jipu la uso.
 
Majipu mengine yanatokea sehemu mbaya mkuu...just imagine jipu limetokea kwenye mning'inio wa ngozi ya p*mb* utalipasuaje?ni kulisubiri tu hadi litakapopata pa kuhamia na ndo mategemeo ya wengi kuhusu huyu doctor na huyu mgonjwa wake mwenye jipu la uso.
HAHAHA JF JAMANI
 
Jipu la usoni unaliacha likauke lenyewe ukilitumbua tuu usaha unaweza kutiririka mpaka mdomoni imagini lina radha gani na harufu.....?
 
Daktari anatumbua majibu lakini anafunga magonjwa, mpaka kwenye jumba la kule dodoma kalichaguwa gonjwa moja juzi la mstaafu yule.


Ndukiiiii
 
Back
Top Bottom