Unaweza usiamini.
Hili zoezi la kutumbua majipu limesababisha hadi vipele na chunusi vimetumbuliwa.
Kuna ndugu yangu ni mwalimu, alikuwa halmashauri ya Chato, akaomba uhamisho kwenda Morogoro. Uhamisho wake ukakubaliwa na akafuata taratibu zote na akaripoti Morogoro na kupangiwa kazi. Hivi sasa ni zaidi ya miezi sita tangu ahamie Morogoro.
Tarehe 25 March wakati mishahara inatoka, aliangalia through NMB mobile akaona mshahara wake umeingia. Kesho yake akataka kutoa hela akakuta hakuna hata shilingi, tena mbaya zaidi muda huo kulikuwa na tatizo la kifamilia hivyo alikuwa na shida ya hela sana. Alipofuatilia akaambiwa mshahara wake umesitishwa kwa sababu ya zoezi la kutumbua watumishi hewa. Daah alipanic sana, akanipigia simu kunieleza, ikabidi nimtafutie amount fulani ili asogeze siku. Akaanza kufuatilia, akaambiwa ishu ilikuwa mshahara kuhamishwa kutoka Chato kuja Moro. Anyway, akaambiwa apige simu Chato, ambapo alijibiwa kuwa mbona mshahara wako tumeshauhamishia Moro? Baada ya kufuatilia tena ikaonekana tena huo mshahara uko benki ila umezuiliwa tuu. Ndio maana uliingizwa alafu ukatolewa kwenye account ya mhusika.
Hakukata tamaa, akafuatilia halmashauri ya Morogoro Vijijini, Mkurugenzi ikawa hapatikani mpaka leo. Sasa imekuwa danadana, anaambiwa njoo kesho, njoo kesho kutwa mpaka sasa hajapewa mshahara wake. Jamani huu ni unyanyasaji wa hali ya juu. Huyu mtu yuko kazini na amehama kihalali na ana nyaraka zote na amefuata taratibu zote sasa huo uhakiki unahitaji nini? Mwalimu mkuu ndiye shahidi kuwa huyu mtu yuko kituoni au la? Na Afisa elimu naye pia analijua hilo. Kuna wakati alienda akajibiwa kuwa ngoja tunafanya uhakiki, kwani uhakiki ni siku ngapi?
Mimi nimehisi huyu mkurugenzi anataka rushwa, la sivyo anataka sifa za kijinga ili aonekane anafanya kazi apewe sifa na Magufuli. Nimemwambia huyu mwalimu aende kesho kwa mara ya mwisho na asipohudumiwa niko radhi kutafuta namba za PM Majaliwa au waziri wa wizara husika ajue watumishi wanavyonyanyswa. Inawezekana huyu mkurugenzi ni jipu akatumbuliwee. Je, kazi zingine zina thamani kuliko familia ya huyu mama anayelala njaa wiki ya tatu sasa, watoto wameshindwa kwenda shule kisa mshahara umesitishwa, na uko benki? Je, kama mkurugenzi yuko busy hakuna watu wengine wa kuhudumia wateja ofisini kwake?
Na taarifa nilizo nazo, siyo huyu mwalimu tuu, kuna wengine wengi wana matatizo kama hayo.