Tumsaidie Magufuli kutumbua vijipu na vipele vidogo vidogo ili kuirudishia nchi heshima iliyopotea

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Hali ya kisiasa nchini imebadilika kwa kipindi kifupi sana kwa namna moaj au nyingine zipo dalili za wazi za mabadiliko katika serikali ya awamu ya tano ya Dk. John Pombe Magufuli.

Kwanza kabisa ni mabadiliko ya kisaikoloji na kiutendaji kazi, ambapo tumeona hamasa kubwa pamoja na njia ya kuelekea katika Tanzania yenye heshima,

Kwa muda mrefu tumekuwa Tanzania yenye kulaumiwa huku tukilea uzembe katika maeneo mbalimbali ya nchi, hilo ni kutokana na uungwana uliopitiliza wa rais aliyemaliza muda wake Jakaya Kikwete.

Tumeona mara tu baada ya kuingia Rais wa awamu ya Tano Dk. Magufuli tumeona mabadiliko kwa baadhi ya mambo tuliyokuwa tukifanya kwa mazoea.

Tumeona katika siku ya uhuru Dec 9, amabo kila mwaka hufanyika sherehe kubwa ya kutumia mabilioni ya shilingi lakini mwaka huu hali imekuwa tofauti taifa liliadhimisha siku hiyo kwa kufanya usafi katika maeneo mbali mbali ya miji na nchi kwa ujumla huku Dr. Magufuli akiongoza mwenyewe zoezi hilo la kufanya usafi.

Ambapo katika tukio hilo la kipekee nchi ilibadilisha mtazamo wa serikali ya awamu ya tano ya Dk. Magufuli. Na wananchi walivyotayari kukubaliana na ujenzi wa taifa lao

Ni dhahiri rais Dk. Magufuli tangu aingie Madarakani amefanya mambo mengi makubwa, hata hivyo kama kawaida ya binadamu kila penye jambo zuri wabezaji hakosi kujitokeza .

Wabezaji wakimfananisha Magufuli na Kikwete kwa kusema hata rais mstaafu Kikwete naye alipoingia Madarakani aliingia kwa staili hiyo hiyo ya kushitukiza katikla mambo mbalimbali yaliyoyawavutia wananchi lakini baadaye yakapotea na kuibuliwa kwa sura ya uzembe katika utendaji pamoja na ubadhirifu katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Huenda wanaobeza ziara za kushitukiza na hatua yake ya kutumbua majipu wanajidanganya au wamesahau mambo Fulani kuhusu Magufuli ambaye amekuwa mwiba tangu alipokuwa waziri wa ujenzi miaka 20 ya uwaziri serikalini

Jambo la msingi ni kufahamu kuwa kila binadamu wanatofautiana na mwingine tusitumie muda mwingi wa kumfananisha Rais Magufuli na rais Mstaafu Kikwete, kwa sababu Magufuli rais tofauti aliyeingia madarakani muda tofauti na hulka tofauti kabisa na waliomtangulia.

Anachofanya kwa sasa rais Magufuli na mawaziri wake ni kuimairisha nidhamu ya utumishi wa umma iliyopotea miaka ya hivi karibuni na anafanya hivyo ili kulet tija kwa wananchi n nchi kwa ujumla.

Kwa sasa Tanazania inatakiwa kuimarisha heshima yake iliyopotea miaka kdha iliyopita na yatusa kukubali kuwa heshima yetu ilipotea kwa kuwa hatukuwa na uwezo wa kujitegemea.

Hali hiyo ilichangia sana kupoteza heshima kwani uchumi wetu na bajeti vilitegemea sana nchi wafadhili, pia nchi haikuwa na uwezo wa kukusanya kodi hali amabayo iliyotengeneza mianya mingi ya kukwepa kodi na ulaji rushwa.

Lazima tuseme tumechoka kusaidiwa nadhani huo ndio msimamo wa wa rais Dk. Magufuli na serikali yake, Nasema hivyo kwa kuwa mara nyingi misaada imekuwa yenye kutudharaulisha kama taifa kuliko kutuendeleza.

Hivyo basi wananchi tuungane kwa pamoja na Rais Magufuli katika kutumbua majipu na vipele vidogo vidogo wakati yeye akitumbua majipu makubwa makubwa ili kuirudishia nchi heshima yake iliyopotea miaka mingi
 
Back
Top Bottom