Ushauri kwa wahandishi wa habari na kwa Jpm

mtima nyongo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
1,947
2,047
Nianze na wanahabari hivi nyie mna matatizo gani?
Taifa hili linachangamoto nyingi kuliko mnavyotuletea habari za kuuzia magazeti yenu tu.
Mbona zile habari zinazotuhusu sisi wananchi wa kawaida hatuziskii kwa nini au mnabagua?
Hapa vigwaza kuna shule ya msingi kisogo hii ina darasa moja tu na mwalimu ni mmoja tu.kinachofanyika ndani ya darasa hilo ni wanafunzi kupokezana tu na nwalimu ni mmoja na anakaa mbali na shule na usafiri wake ni baiskeli.
Na hiyo ni moja ya shule zenye matatizo hapo ujaja hapa maili moja kuna shule kibao zina matatizo kibao hayo hayo lakini cha ajabu wana habari wao ni kuzurula dar tu na kumsifia mh.jpm hivi mnafikiri bila nyie kutoa habari za huku viongozi watajuaje?
Yaani sio siri wanahabari na nyie mnachangia udumavu wa taifa hili.

Kwako jpm najua uko bize na vipele vya joto ingawa wewe unaona ni majipu pale uliposema tukusaidie kutumbua hivyo sasa mimi nataka nikwambie majipu achana na hivyo vipele.

Escrow tumbua hili maana limetufilisi na bado linaendelea kututafuna maana mpaka sasa umeme uko juu
Epa
meremeta
kagoda
Haya ndio majipu tena majipu kweli tumbua haya maana yanaliangamiza taifa bila kuyafanyia kazi haya ni sawa na kupiga makitaim
Na pia kuna ubadhilifu mwingi sana mfano wizara ya ujenzi kuna malipo kwa wakandarasi hewa na pia kivuko kibovu na
pia kuna mikataba ya madini na gesi uku pitia tena la sivyo itakua ni porojo tu na matokeo yake nchi ikashindwa kusonga na ukumbuke hawa wanaokusifia leo na ndio hao hao watakaokucheka kesho maana wa Tz kwa unafiki atujambo


nawasilisha
 
Najua sio waandishi wote wana tabia hiyo lkn bora mkuu umewakumbusha.
Viongozi wako bize kuuza sura na Wanahabari wengi wamekazana kuripoti habari utafikiri kasuku.
Leo kuna mfanyakazi wa Tumbi hospital amenithibitishia kuwa wale waliosimamishwa kazi Tumbi wamerudishwa kazini kimya kimya. Masamaki pia nasikia karudi kazini kimya kimya lkn vyombo vya habari havisemi hayo ili ionekane waliosimamishwa hawakuonewa.

Wanahabari, Magu na serikali yake sio malaika. Tujaribu kumkosoa pale anapokosea
Tutamsaidia kulijenga taifa.
 
Mbona umeiruka RICHMOND wewe nyumbu?
MAJIPU ni
1.Escrow
2.Richmond
3.Kigoda.
4.Meremeta
 
Vijana hawa wa Lowassa wana wakati mgumu mno kipindi hiki..

Yani unaumia sana kuona magazeti mengine hayafuati mlengo wa tanzania daima?

Mkuu... Vumilia tu, hii inaitwa usie mpenda kaja
 
Hivi katika nchi yenye changamoto
Lukuki unakuta gazeti linakichwa
cha habari Magufuli amesali kanisa fulani. Hivi kweli hakuna
habari za maana zinazo gusa
Jamii kama sio ukasuku huu.
 
Umeanza vizuri. Kwa hilo hongera, tena sana.

Ila ulipofika kwenye escrow na hizo kigoda sijui nini kimekukumba hapo umeharibu hoja yako kabisaa. Naona ni pepo la mizuka ya kuropoka

Kila zama na kitabu chake. Nawewe tafuta kitabu chako. Itakuwa poa ukikitumia kumshauri raisi.

Nchi hii watu wajitia wajuaji sana. Yaan mtu akiskia jambo alikomalia ka deni finka.

Tubadilike. Kuna mambo mengi ajabu yanatendeka kinyume na utaratibu na kinyume na sheria na hata sera. Wala hayahitaj darubini kuyagundua.

Komaa na issue zako za matatizo ya shule hapo. Hayo unayajua bora tena una ushuhuda. Mengine unayosikia tu kutoka kupitia spika ya redio yako ni public notice. Yanajulikana. Raisi anajua, waandishi wanajua na wananchi wanajua. Basi tu wananchi wameuchuna raisi ajipambanue mwenyew.

Na kama kuna mwandishi alikuwa ameanza kushawishika na hoja yako. Umemvuruga kabisa. Na hayupo, nakuhakikishia atakayefuata usemacho.

Ni hayo tu

Fake: facebook/likemikelove
 
Wewe Likemike haikosi baba yako ni mhusika katika hayo majipu? Kwani kina masamaki wameiba mwaka huu! Acha tumtake Rais Magufuli amesema tumwombee anatumbua majipu ndio hayo tunamkumbusha ni wajibu wetu
 
waandishi wa habari walifikiri wakiandika habari za lowasa ndio watauza magazeti kwa kipindi cha miaka kumi walihakikisha wanaandika kila tukio kutoa msaada kanisani au misikitini na hiyo yote kwa sababu walikuwa wanalipwa lakini wananchi wamegundua usanii wake kwa hiyo magazeti yaliyokuwa yanaandika habari zake yanadoda sasa waangaliaji wa taarifa ya habari kwenye tv wameongezeka sababu Magufuli yuko busy kutumbua majipu hivyo inabidi uvumilie tu
 
Back
Top Bottom