Tumbo wa CHADEMA ataka kurithi 'viatu' vya Rostam

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
HUKU CCM ikiwa imefungua milango kwa wanachama wake kujitokeza kuchukua fomu juzi za kurithi ‘viatu' Rostam Aziz, wanachama watatu wa Chadema wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo kwenye uchaguzi mdogo Jimbo la Igunga, mkoani Tabora.

Mkurugenzi wa Sera na Utafiti wa Chadema, Waitara Mwikabwe, alisema kuna kila dalili wanachama wengi zaidi watajitokeza kabla ya siku ya mwisho ambayo ni Agosti 16, saa 10:00 jioni.

Waitara alisema wanachama waliojitokeza jana ni Gideon Kwandu, Anwari Luhumbiza Kashaga na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chadema, Erasto Tumbo.

Alisema milango bado ipo wazi kwa mwanachama yeyote mwenye nia ya kugombea na kwamba, gharama ya fomu ni Sh50,000.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Erasto Tumbo, ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Kisesa, wilayani Meatu, kwa tiketi ya UDP, alisema ameguswa na msukumo wa wananchi wa Igunga waliomwomba kugombea nafasi hiyo.

Kwa upande wa CCM, ikiwa ni siku ya pili tangu kuanza zoezi hilo, wanachama wanne wamejitokeza kuchukua fomu.Katibu wa CCM Wilaya ya Igunga, Neema Adamu, alisema licha ya Amina Said Fundikira aliyechukua fomu juzi, wengine waliojitokeza ni Shamshu Ibrahim, Adam Kamange na Ngasa George.

Adam alisema mwisho wa wanachama wanaotaka kuchukua fomu ni Jumamosi ijayo, hivyo aliwataka wenye nia ya kufanya hivyo kujitokeza mapema.

Kwa upande wa CUF, taarifa zilizopatikana mjini Igunga zinadai aliyejitokeza ni aliyewahi kuwania ubunge na kushindwa na Rostam kwenye uchaguzi uliopita. "Ni kweli nagombea tena chama changu kimenipendekeza, mwisho wa wiki baraza kuu watatoa taarifa," alisema Lucas Mahona.

Source: Mwananchi
 
who is erasto tumbo ? CV ikoje? alikuwa mbunge lini? na inaonekana alikuwa mbunge wa bukene sasa inakuwaje aje kugombea igunga?
Hapa chadema inabidi kuwa makini sana msije tu na siyo kuchukua mtu miongoni mwa viongozi wa kitaifa na kumsimamisha. inabidi mumtumie kwa karibu sana yule diwani wenu wa Igunga mjjini anaweza kuwa msaada mkubwa ktk kupata mtu anayekubalika. chadema inabidi kuwa makini sana
Igunga naamini kuwa chama hakijajimaarisha sana maeneno hayo kwahiyo nguvu, umaarufu na utendaji wa mtu unaweza kuwa msaada mkubwa
katika kupata ushindi yaani kama ikiwezekana mgombea wa chadema awe na sifa mara mbili za yule wa ccm ili kutuwezesha kuumuza kwa watu kirahisi.
 
Igunga kweli tuweke mtu makini ,anayekubalika na kuuzika.Pia achunguzwe kwa umakini tusije mpata mtu nusu magamba nusu cdm,Nawatakia upembuzi mwema!
 
Mi napendekeza kwa dhati kabisa kuwa wamtumie diwani wao wa pale Igunga mjini anaweza akawa msaada mzuri ktk kumtafuta mgombea anayeweza kuuzika vizuri!
 
HUKU CCM ikiwa imefungua milango kwa wanachama wake kujitokeza kuchukua fomu juzi za kurithi ‘viatu' Rostam Aziz, wanachama watatu wa Chadema wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo kwenye uchaguzi mdogo Jimbo la Igunga, mkoani Tabora.

Mkurugenzi wa Sera na Utafiti wa Chadema, Waitara Mwikabwe, alisema kuna kila dalili wanachama wengi zaidi watajitokeza kabla ya siku ya mwisho ambayo ni Agosti 16, saa 10:00 jioni.

Waitara alisema wanachama waliojitokeza jana ni Gideon Kwandu, Anwari Luhumbiza Kashaga na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chadema, Erasto Tumbo.

Alisema milango bado ipo wazi kwa mwanachama yeyote mwenye nia ya kugombea na kwamba, gharama ya fomu ni Sh50,000.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Erasto Tumbo, ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Kisesa, wilayani Meatu, kwa tiketi ya UDP, alisema ameguswa na msukumo wa wananchi wa Igunga waliomwomba kugombea nafasi hiyo.

Kwa upande wa CCM, ikiwa ni siku ya pili tangu kuanza zoezi hilo, wanachama wanne wamejitokeza kuchukua fomu.Katibu wa CCM Wilaya ya Igunga, Neema Adamu, alisema licha ya Amina Said Fundikira aliyechukua fomu juzi, wengine waliojitokeza ni Shamshu Ibrahim, Adam Kamange na Ngasa George.

Adam alisema mwisho wa wanachama wanaotaka kuchukua fomu ni Jumamosi ijayo, hivyo aliwataka wenye nia ya kufanya hivyo kujitokeza mapema.

Kwa upande wa CUF, taarifa zilizopatikana mjini Igunga zinadai aliyejitokeza ni aliyewahi kuwania ubunge na kushindwa na Rostam kwenye uchaguzi uliopita. "Ni kweli nagombea tena chama changu kimenipendekeza, mwisho wa wiki baraza kuu watatoa taarifa," alisema Lucas Mahona.
 
chadema bado ni chama dhaifu hata mgombea igunga imekuwa tabu kumpata, mwanzoni walimshawishi mgombea wa cuf akawatolea nje, cdm wanaamini ktk rushwa.
 
Nawashauri CDM wachague mtu anaekubalika kwa wananchi si kwamba kutuletea mtu ambae ana dalili za upendo kwa ccm aje alete usumbufu kama ambavyo Shibuda anafanya
 
Tumbo asubiri bukene 2015,anapaswa mgombea mwenye asili ya Igunga ndo agombee..
 
who is erasto tumbo ? CV ikoje? alikuwa mbunge lini? na inaonekana alikuwa mbunge wa bukene sasa inakuwaje aje kugombea igunga?
Hapa chadema inabidi kuwa makini sana msije tu na siyo kuchukua mtu miongoni mwa viongozi wa kitaifa na kumsimamisha. inabidi mumtumie kwa karibu sana yule diwani wenu wa Igunga mjjini anaweza kuwa msaada mkubwa ktk kupata mtu anayekubalika. chadema inabidi kuwa makini sana
Igunga naamini kuwa chama hakijajimaarisha sana maeneno hayo kwahiyo nguvu, umaarufu na utendaji wa mtu unaweza kuwa msaada mkubwa
katika kupata ushindi yaani kama ikiwezekana mgombea wa chadema awe na sifa mara mbili za yule wa ccm ili kutuwezesha kuumuza kwa watu kirahisi.

huo ni mchakato wa awali tu wa kuchukua fomu ambapo kila mwanachama ana haki akitimiza masharti halafu kutakuwa mchujo wa wagombea kwa kuzingatia sifa zinazofaa na katika hatua hiyo ndipo chama inabidi kiwe makini katika kupata mgombea bora, mwenye sifa na anaeonekana kukubalika.
 
chadema bado ni chama dhaifu hata mgombea igunga imekuwa tabu kumpata, mwanzoni walimshawishi mgombea wa cuf akawatolea nje, cdm wanaamini ktk rushwa.
Kwa mawazo kama haya, nalazimika kumshukuru sana Mh. Mstahiki Meya wa jiji Bw Masaburi kwa kutujulisha kwamba kuna watu wanaofikiri kwa kutumia makalio!
 
chadema bado ni chama dhaifu hata mgombea igunga imekuwa tabu kumpata, mwanzoni walimshawishi mgombea wa cuf akawatolea nje, cdm wanaamini ktk rushwa.
kwa vigezo vyako cdm ni dhaifu lakini kwa vigezo vya wanamagamba wenzako cdm ni hatari na imara kwani hawapati usingizi
 
Tumbo asubiri bukene 2015,anapaswa mgombea mwenye asili ya Igunga ndo agombee..

Augustine Mrema aliposhinda Ubunge Temeke, kabila lake lilibadilika ghafla na kuwa Mzaramo? ...... Na mwaka jana likabadilika tena kurudi kwenye orijino.
 
Back
Top Bottom