Tumbaku inapoipiku dhahabu kwa mapato | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumbaku inapoipiku dhahabu kwa mapato

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by steering, Apr 19, 2012.

 1. s

  steering Member

  #1
  Apr 19, 2012
  Joined: Nov 28, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Tumbaku yaipuku dhahabu kuingizia mapato ya halmashauri
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Wednesday, 18 April 2012 19:51
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0diggsdigg

  Shija Felician, Kahama
  KILIMO cha tumbaku ambacho ni maarufu Kanda ya Ziwa, kinaonyesha kuongoza katika kuingizia mapato makubwa Halmashauri ya Wilaya Kahama na kuishinda migodi miwili ya dhahabu ya Bulyanhulu na Buzwagi inayomilikiwa na Kampuni ya African Barrick Gold Mine.

  Katika makadirio ya bajeti ya mwaka 2012/13, halmashauri hiyo inatarajia kukusanya zaidi ya Sh43 bilioni kutoka vyanzo mbalimbali, likiwa ni ongezeko la asilimia 27.6 ya mwaka 2011/12.

  Akiwasilisha bajeti hiyo kwa madiwani, Ofisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama, Duncan Thebas alisema Sh4.9 bilioni zinatarajiwa kutoka vyanzo vya ndani vya mapato ikiwamo migodi ya dhahabu ya Bulyanhulu na Buzwagi na kampuni za kununua la tumbaku.

  Thebas alisema migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu itachangia Dola 400,000 za Marekani (Sh6 milioni), huku kampuni za kununua tumbaku zikitarajiwa kulipa ushuru wa Sh720 milioni.

  Kutokana na bajeti hiyo, tumbaku inaonyesha ndiyo inayoongoza kuchangia mapato kwenye bajeti tofauti na jamii inavyofikiri, kuwa dhahabu ndiyo inayochangia mapato zaidi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama.

  Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama, Eliza Bwana alisema miradi mingi ya mwaka jana ilishindwa kukamilika kutokana na ucheleweshaji fedha za ruzuku kutoka Srikali na baadhi ya wadau kushindwa kulipa ushuru.

  Bwana alisema sababu zingine zilizochangia kukwama kwa miradi hiyo, ni kupanda kwa gharama za uendeshaji ikiwamo mafuta mitambo, dizeli na petroli na uwapo kwa bajeti finyu iliyopangiwa Idara ya Ujenzi kukarabati barabara.

  Alisema mtandao unaotolewa fedha na Serikali ni kilometa 484 za barabara, hali ambayo ni kidogo ukilinganisha na uharibifu wa barabara unaofanywa na wananchi kwa kuendesha shughuli za kilimo kwenye hifadhi na kupitisha mifugo.

  Hata hivyo, Bwana alisema tayari mikakati imeshafanyika kwa kushirikiana na mkoa, Tamisemi kuhusu mtandao halisi wa barabara Wilaya ya Kahama ili ziweze kupata bajeti halisi na kilichosalia ni wizara kwenda kuhakiki.

  Madiwani walipitisha bajeti ya Sh43,760,610,726 ikiwa ni ongezeko la asilimia 1.5 ya bajeti iliyopita ya Sh43,112,652,848.
  CHANZO: Tumbaku yaipuku dhahabu kuingizia mapato ya halmashauri

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Only in Tanzania
   
 3. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,303
  Likes Received: 973
  Trophy Points: 280
  Tanzania ni zaidi ya uijuavyo.
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Dola 400,000 za Marekani (Sh6 milioni) vs Sh720 milioni.
  Yaani ata HAYA hawana hawa Barrick!
  Kuna haja ya kuiweka hii kwenye guiness book of record na dunia nzima walijue hili!
   
 5. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,575
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  Ipo siku tutashtukia watanzania tunaambiwa tuondoke inchoate imeshauzwa wenyewe wanaihitaji nchi yako.
   
 6. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,717
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  inaelezeka....

  tumbaku inalimwa na wenyeji na kuuzwa kwa makampuni AOTTL, TLTC na PREMIUM.

  kwa kila kilo wanayonunua hao wenye makampuni, kuna dola zaidi wanazilipa kwenye halmashauri in the name of CESS(equivalent ya City Service Levies).

  hiyo ni kinyume na kampuni za dhahabu, mitaji yao, wanachimba dhahabu wao, wanajua wamepata nini ni wao na hakuna wa kuthibitisha walichokipata zaidi ya hao wenye ku-sign mikataba usiku wa manane kwenye mahoteli wakiwa ughaibuni(rejea mkataba wa Buzwagi ulivyosainiwa na Karamagi hotelini usiku huko Uingereza na Lowasa akiwa ni mgeni katika hoteli hiyo hiyo na siku hiyo hiyo ya kusainiwa mkataba....a coincidence??? may be!!!).

  kama kuna kitu migodi imesaidia kwenye hayo maeneo basi pengine ni zile ajira chache kwa wa-TZ na ile economic spill over effect iliyofuatia baada ya hizo ajira rasmi.
   
 7. Kuku wa Kabanga

  Kuku wa Kabanga JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 804
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 80
  Dola 400,000 ni milioni 600 za kitanzania.
   
 8. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,850
  Likes Received: 2,776
  Trophy Points: 280
  Huyu mwandishi naye sijui ni kanjanja? Dola 400,000 ni sawa na milioni 6? Hata haliwezi kushughulisha ubongo? Nyamb..f! Mhariri naye hovyo tu!
   
Loading...