Tumalize Utata: Messi Vs Ronaldo ulimkubali yupi zaidi?

Messi na Ronaldo wote wachezaji wazuri sana.

Tofauti kubwa kati yao sio mafanikio yao kwenye vipengele vya kufunga magoli, kubeba makombe au tuzo binafsi. Katika nanya hizo wote wamefanya vizuri sana na kuvunja records mbalimbali.

Sana sana kigezo mashabiki mtakachotumia ni 'unazi wa team' tu na mapenzi binafsi ila kwa mtu anaejua soka ni ngumu sana kuwashindanisha hao jamaa. Mimi nawapa 50/50. Wote wamefanya maajabu kwenye soka.

Kidogo utofauti naoweza kuwapa ni kuwa Messi kama Messi ana kipaji chakuzaliwa, yani yule mpira upo kwenye DNA. Ronaldo yule jamaa ni mtu anaejituma sana na mwenye malengo japo kipaji anacho lakini kujituma ndio kumemfanya akafikia hapo alipo. Wazungu wanasema "hardwork beats talent" yani kujituma kunashinda kipaji.

Hilo limedhihirishwa Ronaldo kwakuwa kuna wachezaji wengi sana walikuwa na potential pengine kushinda hata yeye lakini waliishia kuwa wachezaji wakawaida tu. Yeye amafika alipofika kwa kujituma sana.

Hivyo basi huu mjadala tukiuangalia kwa jicho la kimpira sio rahisi ku pick kuwa huyu ni bora kuliko huyu. Hao watu wote wana uwezo, japo kwa njia tofauti.
 
Huwezi kumlinganisha Messi na mtu ambaye kaisha kiuchezaji
Hadi jana jumapili Messi katupia mbili kambani Valencia akifa 3,timu yake inaongoza ligi
Ronaldo mlinganishe na akina Van persie,Didier drogba,Rooney nk

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Jana hiyo hiyo Ronaldo nae kafunga magoli mawili Juve ikishinda 2-1 mzee.

Halafu Barcelona haongozi ligi asee acha unazi khaaaa.
 
Makocha wote nguli na wachezaji wengi wakubwa hapa Duniani walisha maliza mjadala huu wa Messi na CR7.

Mimi ni nani nibishe kuwa Messi ndio bora zaidi ya Ronaldo.
Ila ukiniambia Messi na Ronadihno nitamuchagua Ronadihno,kisha Messi akifuatiwa na Garrincha.
 
Jana la pulga amefunga goli kwa free kick yake ya 51

Ila ukitaka mlinganishe na wachezaji wengine duniani wanaokaribia inabidi usogee na uanzie msimu wa 2010/2011

FREE KICKS GOALS

Messi 36 goals
Meralis Pjanic 16 goals
Christian Ronaldo 14 goals

kwa hilo tu la free KICKS goals utaona kua mtu huyu ni hatariiiii


Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Huwezi kumaliza Utata huu ndugu...... Tatizo wanazi Wa Messi Wanampima Pale Pale Barca.......Wakati CR7 Kawika Man U, Madrid,Juve na Timu Ya Taifa....! Sasa mtoe Messi Barca mpeleke kwingine...Huyu anaweza kufanana Pape Ndaw Wa Simba kwa mnaomkumbuka au Ykipe Wa Yanga....Acha Kabisa
 
Tukiwa tunaenda ukingoni kabisa mwa career za soka za Messi na Ronaldo, hawa jamaa hakuna tunachowadai tena, ila tumalize utata ulimkubali nani zaidi katika wakati wakiwa katika ubora wao?

Mimi kwa upande wangu ni Messi, wewe je?
Messi ni Left Footer
Vs
Ronaldo ni Both Footer, na anafunga mpaka na vichwa.

Messi kawika Barcelona
Vs
Ronaldo kawika Lisbon, Man U, Real Madrid and now Juve.

Nje ya Barca hata Sarpong anamzidi Messi.
 
Huwezi kumaliza Utata huu ndugu...... Tatizo wanazi Wa Messi Wanampima Pale Pale Barca.......Wakati CR7 Kawika Man U, Madrid,Juve na Timu Ya Taifa....! Sasa mtoe Messi Barca mpeleke kwingine...Huyu anaweza kufanana Pape Ndaw Wa Simba kwa mnaomkumbuka au Ykipe Wa Yanga....Acha Kabisa
Kwangu mimi MESSI ni bora na siwezi kumjudge wala kumlaumu kwa timu ya taifa maana ameifanyia makubwa pia..Ngoja nikukumbushe, 2014 argentina imeenda WC fainali kwa mgongo wake...Unazikumbuka zile Copa america mbili mfululizo ambazo argentina ilifika final?, zote ilikuwa kupitia mgongo wa Messi...pia usisahau hata hatrick ya Messi ndio imewapeleka Argentina world cup ya 2018...Bado ni TOP SCORER wa Argentina na kupitia timu ya taifa alibeba tuzo ya mchezaji bora kombe la dunia 2018...Amefanya makubwa sana timu ya taifa na wala siwezi kumjudge, bahati haikuwa upande wake ila ameifikisha timu fainali 3 kubwa duniani.


Pia kusema amecheza ligi moja nayo ni sababu haina mashiko...Steven Gerrald kacheza liverpool peke yake lakini anatambulika kama mmoja wa viungo bora kutokea pale epl...bado akina Iniesta, Xavi na wengine wengi kama hao...Ina maana utampuuza Ramos au Buffon kisa tu 90% za maisha yao ya soka wameitumikia timu moja?...MESSI IS THE BEST.


 

Similar Discussions

Back
Top Bottom