MWANASIASA HURU
Senior Member
- Oct 4, 2012
- 180
- 245
Wadau salamu zenu ziwafikie kila mmoja kwa heshima anayostahili.
Nimewiwa kushirikishana nanyi hiki kidogo kiwe kama kihuisho cha nguvu mpya kwa wale wenzetu ambao pengine wanataka kukata tamaa ama kupoteza tumaini la kuyaendea malengo yao katika maeneo fulani ya maisha kutokana na changamoto wanazopitia. Naomba niende moja kwa moja kwenye mada.
Kumbuka kwamba kataliwa au kushindwa jambo/mambo Fulani haimaanishi kwamba wewe huwezi, inamaanisha kwamba kile kilicho kwa ajili yako bado hakijawa tayari.
Kujiamini kwako ni kuiamini ile hekima iliyokuumba
Si kila lango utakaloliendea mbele yako litafunguliwa uingie
Si kila usahili utakaohudhuria utakufanya upate kazi
Na pia si kila unayempenda atakua na hisia kama zako
Ukweli ni huu
Hatupaswi au sio lazima tushinde punde tunapojaribu kwa mara ya kwanza
Ni sawa kushindwa mara kadhaa lakini si sawa kuacha kujaribu.
Ili tuweze kufikia kiwango cha juu cha uwezo wetu na kutimiza malengo yetu, lazima au tunaweza kujikuta tunapitia haya;
Kukataliwa, kuvunjwa moyo na kukatishwa tamaa kwingi
Vinaumiza lakini hakuna namna, thawabu ni kubwa mbeleni
Usijitabirie matokeo Fulani ya kipekee. Huwezi jua kinachokusubiri au kilichowekwa kwa ajili yako mbeleni
Wakati mwingine katika mawimbi ya mabadiliko na kupoteza ama kupata hasara tunapata mwelekeo sahihi.
Tukijaribu kujitenga na vitu Fulani, wakati mwingine tunapata faraja zaidi
Kilichomaanishwa kwa ajili yako utakipata hata kama kiko katikati ya mlima wa miamba.
Lakini pia kisicho kwa ajili yako hutakipata hata kama kiko hatua moja mbele yako
Sahau vyote ulivyopoteza na utengeneze nafasi ili kile unachokihitaji kiweze kupata njia ya kujionyesha ama kuonekana kwenye mazingira yaliyo mbele yako
Uwe tayari tu kupokea, na ndipo utakapoweza kikiona kile unachokihitaji.
Utashinda, pengine si kwa muda mfupi ila kwa hakika utashinda
Uwe na tumaini daima.