Tumaini Bridge Mabwepande Limekatika

Tumaini Bridge Mabwepande Limekatika

Amalinze

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2012
Posts
6,780
Reaction score
5,325
Habari wadau wa HnH,

Kufuatia mvua zilizonyesha kwa wiki hii mfulilizo, Sisi wakazi wa Mabwepande tumepata hadha ya kubomokewa na daraja la tumaini linalounganisha "Kwa Wahanga" na Block 14 Mabwepande viwanja vya Manispaa.

Tulimuita Diwani wetu aje kuona na kutufikishia ujumbe kwa wadau husika akatuambia kwamba ujenzi wa madaraja haupo tena chini ya mkurugenzi wa manispaa bali upo chini ya mkurugenzi wa TARURA hivyo wao hawana "SAY" yeyote.

Mpaka hivi tunavyoongea magari hayapiti,pikipiki hazipiti na hizi mvua zinazoendelea hata wanafunzi wa msingi na sekondary wanapata tabu sana kuvuka kwa jinsi miundombinu ya daraja ilivyoharibika.

Pale kuna mkandarasi anajenga daraja la kudumu lakini mpaka sasa lipo katika hatua ya chini sana na limeshachafuliwa na matope na zege ya kushika chini "landing" ilikuwa bado haijapigwa na tukimuuliza mkandarasi mbona umeacha nondo na marine wazi mda wote hamjamwaga zege akasema walishatoa "order" mda mrefu sana Wazo wapelekewe gari ya zege lakini mpaka muda huu zege halijaletwa.

Tunaomba mamlaka husika watusaidie hata kujenga daraja temporary kwa kutumia maringi madogo yale ya zege ili tuweze kupita pale na pikipiki pamoja na magari.

1097933


1097937
 
Habari wadau wa HnH,

Kufuatia mvua zilizonyesha kwa wiki hii mfulilizo, Sisi wakazi wa Mabwepande tumepata hadha ya kubomokewa na daraja la tumaini linalounganisha "Kwa Wahanga" na Block 14 Mabwepande viwanja vya Manispaa.

Tulimuita Diwani wetu aje kuona na kutufikishia ujumbe kwa wadau husika akatuambia kwamba ujenzi wa madaraja haupo tena chini ya mkurugenzi wa manispaa bali upo chini ya mkurugenzi wa TURURA hivyo wao hawana "SAY" yeyote.

Mpaka hivi tunavyoongea magari hayapiti,pikipiki hazipiti na hizi mvua zinazoendelea hata wanafunzi wa msingi na sekondary wanapata tabu sana kuvuka kwa jinsi miundombinu ya daraja ilivyoharibika.

Pale kuna mkandarasi anajenga daraja la kudumu lakini mpaka sasa lipo katika hatua ya chini sana na limeshachafuliwa na matope na zege ya kushika chini "landing" ilikuwa bado haijapigwa na tukimuuliza mkandarasi mboma umeacha nondo na marine wazi mda wote hamjamwaga zege akasema walishatoa "order" mda mrefu sana Wazo wapelekewa gari ya zege lakini mpaka muda huu zege haijaletwa.

Tunaomba mamlaka husika watusaidie hata kujenga daraja temporary kwa kutumia maringi madogo yale ya zege ili tuweze kupita pale na pikipiki pamoja na magari.

View attachment 1097933

View attachment 1097937
Wamelala sasa hivi tumebaki sisi tu walinzi. Anyway tutawajulisha wakiingia kazini kesho mkuu.
 
duhhh,poleni sana,kwa nini kama tumeshindwa kuyatengeneza wenyewe...tusiite watalaam kutoka nje,waje wayasome mazingira afu wajenge hayo madaraja… 🙄🙄
 
Poleni sana, shughuli zenu za uzalishaji zinakwama kwa ajili hiyo kwa mko wangapi hapo?
Mkisubiri hao mtalala njaa
 
Wamelala sasa hivi tumebaki sisi tu walinzi. Anyway tutawajulisha wakiingia kazini kesho mkuu.
Tunashukuru sana in advance kwa hoja yako ya kutuwasilishia matatizo yetu kwa watu husika.
 
duhhh,poleni sana,kwa nini kama tumeshindwa kuyatengeneza wenyewe...tusiite watalaam kutoka nje,waje wayasome mazingira afu wajenge hayo madaraja… 🙄🙄
Asante sana,bora tuwape wachina,wapo shapu sana katika ujenzi,wao hawasubiri sijui kulipwa 20% ndio waanze kazi,wao wanaanza kazi mwanzo mpaka mwisho mtakuja kulipana kazi ikishaisha.
 
Poleni sana, shughuli zenu za uzalishaji zinakwama kwa ajili hiyo kwa mko wangapi hapo?
Mkisubiri hao mtalala njaa
Tupo wengi mkuu ila changamoto ya pale sisi wananchi hatuwezi kuitatua maana ni gharama sana kupafanya paweze kupita gari na pikipiki.
 
Asante sana,bora tuwape wachina,wapo shapu sana katika ujenzi,wao hawasubiri sijui kulipwa 20% ndio waanze kazi,wao wanaanza kazi mwanzo mpaka mwisho mtakuja kulipana kazi ikishaisha.
Acha ulongo wewe mtu mzima
 
Back
Top Bottom