Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,231
- 44,438
usishangae sheria hiyo ilipopitishwa hakuwa macho bungeni.................na hakujua hasa kuwa sheria kama hiyo imepitishwa.
wabunge wetu ni vichekesho kwa kweli
Mongella alisema hayo baada ya Kamanda wa Tasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (Takukuru) Wilaya ya Ukerewe, Leonidas Rugemalila, na Msimamizi wa Uchaguzi wa wilaya hiyo, Dk. Leonard Masale, kuwasilisha mada zao kuhusu sheria hiyo katika kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Ukerewe.
Nnaloliona mm ni ufinyu wa fikra katika viongozi wetu.....Hv hawa watu wangekuwa makini ,wangetumia busara wakati wa kuitunga hii sheria na sio kulalamika sasa!!ametaka busara itumike katika kutekeleza Sheria ya Gharama za Uchaguzi, vinginevyo wagombea watatengwa na jamii.
wabunge wetu woote sehemu kubwa ni 'shake well be for use' hawana wanalolijua kwa sababu wengi wao ni vilaza, but they are there for their own benefits and prostitusion practicesHalafu sheria ilisharudishwa tena kufanyiwa marekebisho kabla hata ya kuanza kutumika hawakusema lolote!
Mama Mongella naona analalamika bure wakati huu. TAKUKURU wamepewa maelekezo ya kutosha juu ya nini ni rushwa na nini sio rushwa.
Sio kweli kwamba mheshimiwa akitembelewa na marafiki nyumbani na kula nao chakula eti TAKUKURU wataingilia. Kuna mambo ambayo wameyapa uzito ikiwa ni pamoja na hilo la kugawa kadi kinyemela, kutoa zawadi kwenye mikutano ya hadhara, kutoa zawadi au michango makanisani na kukutana na wananchi au viongozi kwa lengo la kuwashawishi kukupigia kura na kisha kuwapa zawadi.
Kwenye mikutano mingi ya wabunge sasa, kabla haijaanza, TAKUKURU humwaga makaratasi ya kuonya juu ya kutoa na kupokea rushwa. Wabunge wengi wamekimbia bungeni ili kuanza kampeni mapema kwa kisingizio cha kwamba wanatimiza majukumu yao jimboni. Huu ndio muda ambao walikuwa wanajiandaa kutoa misaada na zawadi nyingine mbalimbali. Kuwepo kwa hii sheria kunawabana na hata mikutano yao inaishia malalamiko tu maana wananchi wanategemea posho.
Kwa mtu ambaye hana pesa za kutoa hii ni habari njema. Ukiwaita wananchi na kuwaacha waondoke bila posho unakuwa umejiletea maadui. Hivyo huko mbele wagombea wengi wataona bora wafuate ratiba za chama au tume ya uchaguzi ili wasilaumiwe kwa kuita wananchi kwenye mikutano yao na kuwanyima hata soda.
Wacha tuone mwisho wake ila ni kweli TAKUKURU wapo kila sehemu wakikusanya ushahidi. Labda tatizo kwa Tanzania ni je huo ushahidi wanaoupata wanautumia vizuri kuhakikisha wenye makosa wanaadhibiwa? Kibaya ni pale wanapoamua kuchagua watu wa kuwashughulikia na kuwaacha wengine ambao huenda makosa yao hata ni makubwa zaidi.
Wacha tuone mwisho wake ila ni kweli TAKUKURU wapo kila sehemu wakikusanya ushahidi. Labda tatizo kwa Tanzania ni je huo ushahidi wanaoupata wanautumia vizuri kuhakikisha wenye makosa wanaadhibiwa? Kibaya ni pale wanapoamua kuchagua watu wa kuwashughulikia na kuwaacha wengine ambao huenda makosa yao hata ni makubwa zaidi.
Mongella: Sheria ya Gharama za Uchaguzi itekelezwe kwa umakini
Mmezidi Ubishi, wabunge nyinyi, kulalamika mlalamike nyinyi.. tuliwaimbia na kuwapigia kelele hii sheria mbovu mkaizunguka kwa mbwembwe kama watu wanaomzunguka mganga wa kienyeji.. sasa wacha igeuke iwanyofoe ndio mkome. Inakuwaje mtunga sheria anailalamikia sheria ambayo alikuwa na uwezo wa kuifanyia mabadiliko!HTML: