Nimerudia humu same thing kama mara mia kua internet asilimia kubwa imejaa information za uongo watu wanajifanya hawaelewi. Chukua mshamba mpe internet ndiyo matokeo yake, wanafikiri computer ni viumbe flani hivi vinavyosema ukweli, watu hawana idea blog za uongo zinalipa sana coz habari zinasambaa ka kirusi, hela za matangazo kiulaini kabisa. Bongo hadi watu na elimu zao wanaweka akili yao pembeni kisa neno 'fox-news' hehehe, natumai hili litakua limewafunza. Hii ni aibu kubwa balaa.
Na hapo ndipo siri ya ushindi wa kimbunga sijui tsunami kwa watawala Afrika ulipo. Unatumia ujinga wao kuwatawala upendavyo pasi na wao kuhoji.... Mtu ambaye ni masikini kielimu huwezi kumtofautisha na kokoro ambalo linabeba chochote ndani ya maji. Kila anachokisoma kwenye mitandao anakiamini ....
Ahsante mkuu typographical error.Duh! Hiyo 'foxchennel.com' lazima nayo itakuwa ya uongo tu maana hata mi mwenyewe niliye news junkie sijawahi kuisikia😀😀😀
Ahsante mkuu typographical error.
Ni foxchannel.com. Ahsante kwa masahihisho.
Ndio maana kuna watu wengine wanasema hii dhana ya demokrasia haifai katika nchi ambazo hazijaendelea kwa sababu wananchi wake wengi ni wajinga.Na hapo ndipo siri ya ushindi wa kimbunga sijui tsunami kwa watawala Afrika ulipo. Unatumia ujinga wao kuwatawala upendavyo pasi na wao kuhoji.
Fake news ni hatari sana kwa usalama wa nchi masikini hasa zile masikini kielimu.
Mtu ambaye ni masikini kielimu huwezi kumtofautisha na kokoro ambalo linabeba chochote ndani ya maji. Kila anachokisoma kwenye mitandao anakiamini.
Nimesikia hata bunge la Uingereza limeunda kamati maalum kuchunguza athari za fake news na njia ya kupambana nazo kisheria.
Waingereza wameona namna ambavyo fake news zimetumika katika uchaguzi mkuu wa Marekani na kwa maana hiyo wanataka kutafuta njia ya kudhibiti kabla hawajaingia kwenye Uchaguzi Mkuu.
Wameidhibiti kiasi sasa.Hata hiyo 'foxchannel.com' kwangu ni ngeni😀.
Ni lini na wapi dhana isiyo ya kidemokrasia (udikteta) ilifaa au ilileta maendeleo katika nchi za "wajinga" hususan Afrika? Zaire ya Mobutu? CA ya Bokassa? Samalia ya Siad Bare? Au Chad ya Habre? Au pengine Nyasaland ya Kamuzu? Nipe japo mfano mmoja ambako udikteta ulileta nafuu katika Afrika ya "wajinga".Ndio maana kuna watu wengine wanasema hii dhana ya demokrasia haifai katika nchi ambazo hazijaendelea kwa sababu wananchi wake wengi ni wajinga.
...
Bora wewe, Mimi nilinyofolewa kwenye group la wakereketwa kwamba sio mzalendo.nadhani Leo admin anaweza kunifikiria.Hii hoax news ilipelekea nikamuita mfanyakazi mwenzangu kilaza baada ya kupost kwenye group la kazini, bado hajanisamehe....🙁
Bora wewe, Mimi nilinyofolewa kwenye group la wakereketwa kwamba sio mzalendo.nadhani Leo admin anaweza kunifikiria.
Ha ha ha! Tatizo liko hapa:Bora wewe, Mimi nilinyofolewa kwenye group la wakereketwa kwamba sio mzalendo.nadhani Leo admin anaweza kunifikiria.
Ya BASHITE vyanzo vya habariHata mimi naanza kuwa na wasiwasi na Kashfa ya Bashite. Nina mashaka kama habari zinazosambaa za kughushi cheti na jina kama ni za kweli. We need confirmation from trusted source! Lakini hivyo vyombo/source za kuaminika zipo kama TV rasmi ya serikali, ambayo, kimsingi, tunaamini ndipo penye magwiji wa habari na vyanzo vyake inaweza kuingia mkenge kiasi kile? Tutaendelea kuishi kwa uzushi.
Duh! Hiyo 'foxchennel.com' lazima nayo itakuwa ya uongo tu maana hata mi mwenyewe niliye news junkie sijawahi kuisikia😀😀😀[/QUOT]}
Kaitaja kizenji jamani khaaa. We jamaa bhana
hata mimi sizipendi these so called "fake news". I abhor it in the deepest earnest!Kipindi cha kampeni za urais wa Marekani mwaka jana kuna habari za kizushi zilizokuwa zinasambazwa mtandaoni kuhusu rais Donald Trump [wakati huo akiwa mgombea] kusema maneno ya kashfa kuhusu Waafrika, viongozi wa Kiafrika, na kadhalika.
Kwamba eti Trump aliwaita Waafrika kuwa ni "lazy fools", kwamba eti alisema Afrika inabidi itawaliwe tena, na blah blah zingine kama hizo.
Hapo chini ni viunganishi vya baadhi ya huo uzushi ambao uliaminiwa sana na idadi kubwa tu ya watu hapa Tanzania na kwingineko barani [Afrika].
'Africans are lazy fools only good at eating, lovemaking and thuggery'
According to fact-checking website Snopes this claim was first posted on 25 October 2015 on Politica, a fake news website. It was later picked up by blogs and other fake and satirical news websites on the continent.
Donald Trump: “There Is No Shortcut To Maturity, Africa Should Be recolonized
Speaking last week in Nebraska, Trump said that Africans are slaves living like slaves in their own land yet they claim they are independent.
Fake Trump Quotes About Africans Have Blown Up On Facebook Thanks To Hoax Sites.
Baadhi yetu humu tulijitahidi sana kuwaelimisha watu kuwa hizo habari ni za kizushi al-maaruf siku hizi kama 'fake news'.
Lakini kwa kiasi kikubwa juhudi zetu hizo ziliangukia patupu. Watu waliendelea kuziamini tu.
Tuliwaambia kuwa hakuna chombo chochote kile cha habari cha kuaminika na kuheshimika kilichoripoti huo uzushi lakini wenzetu hawa hawakukubali.
Tukawaambia kuwa haiwezekani kabisa Trump aseme hayo maneno hadharani halafu vyombo vya habari vya Marekani visiripoti na pia wapinzani wake wasimlaani kwenye midahalo mbalimbali ya ndani ya chama chake pamoja na ile mitatu aliyoshiriki na Hillary Clinton, lakini wapi. Wenzetu hawa wakaendelea tu kuamini huo uzushi.
Na wala haikuwa vigumu kabisa kubaini kuwa hizo habari zilikuwa ni za kizushi. Mtu yeyote yule aliye na werevu wa kawaida kabisa angeweza kubaini haraka mno. Ilikuwa ni kuangalia tu chanzo au vyanzo vya hizo habari, basi. Hitimisho lingekuwa ni rahisi mno kulifikia.
Ila cha kushangaza kuna watu ambao huonekana kama ni werevu lakini kwenye hili nao wakaingia mkenge na kuamini uzushi uliokuwa dhahiri. Aibu!
Sasa baada ya televisheni ya taifa, TBC, kutangaza habari za pongezi za kizushi kuhusu rais Trump kumpongeza rais Magufuli ndo naona watu wamekubali kuwa kweli kuna 'fake news', hususan kuhusu Trump na Afrika.
Natumai wengi watakuwa wamejifunza somo muhimu na lenye thamani kutoka kwenye hiyo blunder ya TBC.
Somo lenyewe ni kuhakikisha na kuthibitisha chanzo au vyanzo vya habari. Kuhakikisha na kuthibitisha kuwa hicho chanzo au hivyo vyanzo ni vya kuaminika kabla ya kurusha au kuandika habari yoyote ile. Kwa kifupi, mara zote hoji chanzo ay vyanzo vya habari. Usimeze tu kila upewalo kama mtu asiye na akili. Hoji mambo.
Ni aibu kubwa mno kwa kituo cha habari cha taifa kuwa na utovu wa umakini wa kiwango hicho walichokionyesha katika urushaji wao wa hiyo habari ya kizushi.
Aibu! Aibu! Aibu!
Na kwa sababu hiyo hawana budi kuwaomba radhi wananchi.
hata mimi sizipendi these so called "fake news". I abhor it in the deepest earnest!
lakini ningekuwa mimi ningeweka akiba ya maneno....what if it eventually turns out kuwa ni za ukweli? kwa sababu ninaona sababu inayotumika hapa ku-discredit hizi news ni eti tu kwa vile haziku-originate from a credible source. really?
how much credible is credible? we all know that man Trump can do any and every crazy thing that you can subscribe to under the sun.....which does not exclude doing the credible incredibly!
akiba ya maneno ni hekma!
Mbona hawa wa fake news wamesimamishwa haraka sana lakin wenye vyeti fake bado wapo kazin?