Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 93,479
- 119,312
Kipindi cha kampeni za urais wa Marekani mwaka jana kuna habari za kizushi zilizokuwa zinasambazwa mtandaoni kuhusu rais Donald Trump [wakati huo akiwa mgombea] kusema maneno ya kashfa kuhusu Waafrika, viongozi wa Kiafrika, na kadhalika.
Kwamba eti Trump aliwaita Waafrika kuwa ni "lazy fools", kwamba eti alisema Afrika inabidi itawaliwe tena, na blah blah zingine kama hizo.
Hapo chini ni viunganishi vya baadhi ya huo uzushi ambao uliaminiwa sana na idadi kubwa tu ya watu hapa Tanzania na kwingineko barani [Afrika].
'Africans are lazy fools only good at eating, lovemaking and thuggery'
According to fact-checking website Snopes this claim was first posted on 25 October 2015 on Politica, a fake news website. It was later picked up by blogs and other fake and satirical news websites on the continent.
Donald Trump: “There Is No Shortcut To Maturity, Africa Should Be recolonized
https://www.africametro.com/world-n...trump-no-shortcut-maturity-africa-recolonized
Speaking last week in Nebraska, Trump said that Africans are slaves living like slaves in their own land yet they claim they are independent.
Fake Trump Quotes About Africans Have Blown Up On Facebook Thanks To Hoax Sites.
Baadhi yetu humu tulijitahidi sana kuwaelimisha watu kuwa hizo habari ni za kizushi al-maaruf siku hizi kama 'fake news'.
Lakini kwa kiasi kikubwa juhudi zetu hizo ziliangukia patupu. Watu waliendelea kuziamini tu.
Tuliwaambia kuwa hakuna chombo chochote kile cha habari cha kuaminika na kuheshimika kilichoripoti huo uzushi lakini wenzetu hawa hawakukubali.
Tukawaambia kuwa haiwezekani kabisa Trump aseme hayo maneno hadharani halafu vyombo vya habari vya Marekani visiripoti na pia wapinzani wake wasimlaani kwenye midahalo mbalimbali ya ndani ya chama chake pamoja na ile mitatu aliyoshiriki na Hillary Clinton, lakini wapi. Wenzetu hawa wakaendelea tu kuamini huo uzushi.
Na wala haikuwa vigumu kabisa kubaini kuwa hizo habari zilikuwa ni za kizushi. Mtu yeyote yule aliye na werevu wa kawaida kabisa angeweza kubaini haraka mno. Ilikuwa ni kuangalia tu chanzo au vyanzo vya hizo habari, basi. Hitimisho lingekuwa ni rahisi mno kulifikia.
Ila cha kushangaza kuna watu ambao huonekana kama ni werevu lakini kwenye hili nao wakaingia mkenge na kuamini uzushi uliokuwa dhahiri. Aibu!
Sasa baada ya televisheni ya taifa, TBC, kutangaza habari za pongezi za kizushi kuhusu rais Trump kumpongeza rais Magufuli ndo naona watu wamekubali kuwa kweli kuna 'fake news', hususan kuhusu Trump na Afrika.
Natumai wengi watakuwa wamejifunza somo muhimu na lenye thamani kutoka kwenye hiyo blunder ya TBC.
Somo lenyewe ni kuhakikisha na kuthibitisha chanzo au vyanzo vya habari. Kuhakikisha na kuthibitisha kuwa hicho chanzo au hivyo vyanzo ni vya kuaminika kabla ya kurusha au kuandika habari yoyote ile. Kwa kifupi, mara zote hoji chanzo ay vyanzo vya habari. Usimeze tu kila upewalo kama mtu asiye na akili. Hoji mambo.
Ni aibu kubwa mno kwa kituo cha habari cha taifa kuwa na utovu wa umakini wa kiwango hicho walichokionyesha katika urushaji wao wa hiyo habari ya kizushi.
Aibu! Aibu! Aibu!
Na kwa sababu hiyo hawana budi kuwaomba radhi wananchi.