Tulivyonusurika kufanyiwa mchezo mchafu Tabora

junky

JF-Expert Member
May 11, 2017
413
976
Hekima kwa anaye kwenda ugenini ni kuwauliza wenyeji kuhusu mazingira,mandhari,utamaduni na kanuni za sehemu uhusika.Lakini imekuwa jambo la kawaida siku hizi mtu akisafiri kwenda ugenini hafati taratibu hizi bali hufanya masuala yake kimya kimya binafsi nimejifunza haswa huu mkoa wa Tabora umenifunza unapoenda ugenini kabla ya kufanya jambo dadisi kwanza.

Nakumbuka mimi na wenzangu 4 tulipata safari ya kwenda Tabora tulipofika mkoa husika ilikuwa nyakati ya usiku na tuliamua kutafuta gesti nzuri ili tujipumzishe na uchovu wa safari na kwa bahati nzuri tulipata gesti moja wapo na kulipia 30,000. Kwenye hio gesti tulimkuta mzee mmoja kapanda hewani alivyo kama mtu wa kanda ya kati. Alitupokea vizuri na kutupa maelekezo na kwenye ile gesti tulikuwepo sisi wenyewe tu hatukuona wateja wengine.

Changamoto kwenye ile gesti ilikuwa ni maji, maji ya pale yalikuwa ni kama yenye rangi ya maziwa hayakuwa masafi hivyo tabu ilikuwa kwenye kuoga wapo walioenda kuoga katika sisi mara ghafla mwenzetu mmoja tuliyekuwa naye akaanza kupiga kelele ikatubidi tuende tukamuone ili tufahamu tatizo nn.

Ikafahamika kuwa amepandisha majini sijui mashetani lakini uzuri mmoja wetu alikuwa na uzoefu na watu wenye matatizo yale akawa anamshika kichwa na kuongea naye na kumuuliza anataka nini na shida nini,kwa masikio yangu nashuhudia conversation ya hawa wawili yule jamaa akawa anadai tuondoke pale kwakuwa ni pachafu na alikuwa anasisitiza hivyo ikatubidi tukubali ili kelele na yule mgonjwa atulie na pili ilituogopesha kauli aliyotoa.

Ikatubidi tumuite yule mzee tumuambie tumepata udhuru hivyo imetulazimu tuondoke na hatukudai pesa na hata hatukulala wala kupumzika hata kwa dakika, tuliondoka mule na kumuita bajaji atupeleke sehemu nyingine cha kushangaza yule dereva wa bajaji alitushangaa sana sie kwenda kwenye ile gesti na alituambia mna bahati sana watu huwa hawaendi kupumzika kwenye ile gesti labda wageni tu wasiojua.

Alituambia mule watu huingiliwa kinyume na maumbile wakilala na kuna mauza uza mengi na kweli kwenye ile gesti vyumba vyote havikuwa na watu kasoro sie tu na kuuliza uliza mjini pale kila mmoja anatueleza hivyo hata hio gesti nyingine hatukuitafuta tena tulikesha usiku wote.

Yule aliyepandisha ametunusuru aise ilikuwa tufanywe vibaya ila watu wa Tabora mnazingua sana.

Jamani ukienda mikoani tuweni waangalifu
 
Kwahiyo majini ya jamaa yaliona yamuikoe kiti wao asitatuliwa malinda..😂
Sasa Kama ni hivyo hiyo gesti si ndo wangejaa mashoga ili watimiziwe haja zao.. 🤣
 
Taarifa nzuri ila mwishon umeboronga kabisa "et mukienda mikoani muwe Waangalifu". Mbona sisi baadhi yakija huda Dar kufanyiwa vituko, kukabwa, kuchanwa marinda, halafu hata kama munaona, mkijua ni mtu wa mkoan hapati msaada!!
Kwahyo wewe ulipotaka kuliwa kimasihara huko tabora, basi ukajua ni mikoa yote, Kwan huko Dar hakuna maruerue kama hayo!?

Habari yenyewe imekaa kibaguz baguz tu!
 
Ungekuwa umefanya la maana sana kueleza hata hilo eneo ni eneo gani, wilaya, au mtaa gsni, , halafu pili ukatutajia na jina la hiyo guest house kukamilisha uzi wako. Vinginevyo haina maana kushea uzi mrefu hivi halafu waende watu wengine gest hiyo wakapate shida, umeamua kushea basi shea vyote tujue tujihadhari.
 
Taarifa nzuri ila mwishon umeboronga kabisa "et mukienda mikoani muwe Waangalifu". Mbona sisi baadhi yakija huda Dar kufanyiwa vituko, kukabwa, kuchanwa marinda, halafu hata kama munaona, mkijua ni mtu wa mkoan hapati msaada!!
Kwahyo wewe ulipotaka kuliwa kimasihara huko tabora, basi ukajua ni mikoa yote, Kwan huko Dar hakuna maruerue kama hayo!?

Habari yenyewe imekaa kibaguz baguz tu!
Haijakaa kibaguzi nisamehe kwenye mapungufu kila sehemu kuna changamoto zake hata ukija Dar inabidi uwaulize wenyeji ili uepukani na ukabaji na maruerue mengine
 
Hayo mambo Tabora hakuna,kweli zamani imani za kishirikina zilikuwepo na hazikuwa za kulana viboga ila ilikuwa chuma ulete ndio sana
 
Back
Top Bottom