Consigliere
Platinum Member
- Sep 9, 2010
- 12,802
- 27,026
Mngerudi ili kuvumilia muone na kuthibitisha kama kweli mngeingiliwa ua ni imani na story za watu tu.
Walitaka wakutoeni marinda?Hekima kwa anaye kwenda ugenini ni kuwauliza wenyeji kuhusu mazingira,mandhari,utamaduni na kanuni za sehemu uhusika.Lakini imekuwa jambo la kawaida siku hizi mtu akisafiri kwenda ugenini hafati taratibu hizi bali hufanya masuala yake kimya kimya binafsi nimejifunza haswa huu mkoa wa Tabora umenifunza unapoenda ugenini kabla ya kufanya jambo dadisi kwanza.
Nakumbuka mimi na wenzangu 4 tulipata safari ya kwenda Tabora tulipofika mkoa husika ilikuwa nyakati ya usiku na tuliamua kutafuta gesti nzuri ili tujipumzishe na uchovu wa safari na kwa bahati nzuri tulipata gesti moja wapo na kulipia 30,000. Kwenye hio gesti tulimkuta mzee mmoja kapanda hewani alivyo kama mtu wa kanda ya kati. Alitupokea vizuri na kutupa maelekezo na kwenye ile gesti tulikuwepo sisi wenyewe tu hatukuona wateja wengine.
Changamoto kwenye ile gesti ilikuwa ni maji, maji ya pale yalikuwa ni kama yenye rangi ya maziwa hayakuwa masafi hivyo tabu ilikuwa kwenye kuoga wapo walioenda kuoga katika sisi mara ghafla mwenzetu mmoja tuliyekuwa naye akaanza kupiga kelele ikatubidi tuende tukamuone ili tufahamu tatizo nn.
Ikafahamika kuwa amepandisha majini sijui mashetani lakini uzuri mmoja wetu alikuwa na uzoefu na watu wenye matatizo yale akawa anamshika kichwa na kuongea naye na kumuuliza anataka nini na shida nini,kwa masikio yangu nashuhudia conversation ya hawa wawili yule jamaa akawa anadai tuondoke pale kwakuwa ni pachafu na alikuwa anasisitiza hivyo ikatubidi tukubali ili kelele na yule mgonjwa atulie na pili ilituogopesha kauli aliyotoa.
Ikatubidi tumuite yule mzee tumuambie tumepata udhuru hivyo imetulazimu tuondoke na hatukudai pesa na hata hatukulala wala kupumzika hata kwa dakika, tuliondoka mule na kumuita bajaji atupeleke sehemu nyingine cha kushangaza yule dereva wa bajaji alitushangaa sana sie kwenda kwenye ile gesti na alituambia mna bahati sana watu huwa hawaendi kupumzika kwenye ile gesti labda wageni tu wasiojua.
Alituambia mule watu huingiliwa kinyume na maumbile wakilala na kuna mauza uza mengi na kweli kwenye ile gesti vyumba vyote havikuwa na watu kasoro sie tu na kuuliza uliza mjini pale kila mmoja anatueleza hivyo hata hio gesti nyingine hatukuitafuta tena tulikesha usiku wote.
Yule aliyepandisha ametunusuru aise ilikuwa tufanywe vibaya ila watu wa Tabora mnazingua sana.
Jamani ukienda mikoani tuweni waangalifu
Kivumishi kijumuishi chenye kitenzi kikurupushi...?(nimecheka).Mwishoni umehitimisha vibaya kwa kusema watu wa watabora, maana siyo wote na wala siyo gesti zote za Tabora. Umetumia kivumishi kijumuishi 😕😕😕
Dunia ina mengi ni sawa kabisa hata nami nilikuwa siamini hayo mambo hadi yaliponikutaga lakini Mungu ni mwema alinishindia kabisa hizo nguvu za giza.Naweza kukuunga mkono kwa kuwa nilishawahi kukutana na kisa kinacho karibiana na hicho miaka takriban sita iliyopita, maeneo ya Mombo Tanga.
Katika kuhangaika na mambo ya maisha nikajikuta mimi na rafiki zangu wawili tumeingia katika biashara za madini haya ya bei za chini kidogo na tulikuwa tunakwenda vijiji tofauti vya wachimbaji ili kununua na sisi kwenda kuuza sehemu husika, siku ya tukio tulielekezwa kijiji fulani (jina limenitoka) kilichopo Sambaani na kuambiwa huko yupo mzee ni mchimbaji hivyo ipo nafasi ya biashara.
Tukaanza safari kutoka Dar na kushuka Mombo na ikawa tumechelewa bus la kwenda huko ndani ndani ikatubidi tutafute guest ya kupumzika.
Ilikuwa ni mwisho wa wiki kila guest ikawa imejaa ila tukapata muhuni akasema tumtoe atupeleke sehemu ya uhakika, tukaenda kufika ni jengo la ghorofa safi sana na lina vyumba vya maana ila ajabu alikuwepo mlinzi tu na hakukuwa na wateja wengine pamoja ya kuwa jengo hilo halikuwa mbali na barabara kuu!
Hatukujali hilo tukachukua chumba ghorofa ya kwanza ambacho ni kikubwa na kina vitanda viwili, kimoja nikalala mimi na kingine wakalala rafiki zangu.
Kufika nane za usiku niliamshwa na upepo mkali sana na kufumbua macho mlango ulikuwa wazi kabisa japo mimi ndiye niliyeufunga! Sikuwa na nguvu hata ya kusogeza mkono kwani mwili wote ulikuwa na ganzi na ghafla kutokea mlangoni aliingia kiumbe wa ajabu kwa madaha huku akitoa sauti za kutisha zenye mwangwi! Alikuwa kama sokwe ila anatembea na miguu miwili, alikuwa na pembe kichwani, alikuwa na macho mekundu kama damu na pia akiongea anatoa kitu kama moto mdomoni.
Kutupia jicho wenzangu walikuwa wanagaragara kama wanaohangaika usingizini, ghafla kile kiumbe kikajigawa na kuwa wawili na ikumbukwe hatua zao ni za pole pole sana mfano anaweza kupiga hatua moja ikapita hata robo saa ndio akanyanyua mguu mwengine.
Akili ikanijia kusoma Quraan kimoyo moyo kwa muda na kumbe muda ule wenzangu nao walikuwa wanayapitia ninayopitia mimi na kila mmoja anaomba kwa Imani yake! Ghafla vile viumbe vikatoweka na kufuatiwa na giza zito ajabu na hapo ndipo sote nguvu zikatujia na kuamka ila hakuna aliyethubutu kwenda kuwasha taa wala kumhadithia mwenzake ila baada ya muda tukazungumza machache na itoshe kusema tulikwenda kukesha stand.
Asubuhi tulipouliza watu walitushangaa sana kwenda pale na walitujuza kuwa pale hakuna huduma kwani lile jengo ni la urithi hivyo lina ugomvi wa ndugu hivyo limewekwa mizimu ili kusikalike kuwe na tisho ili kumkomoa kaka yao aliyelitawala.
Dunia ina mengi hii ni zaidi ya uijuavyo.
Ndugu una comment kumzidi mleta uziNaweza kukuunga mkono kwa kuwa nilishawahi kukutana na kisa kinacho karibiana na hicho miaka takriban sita iliyopita, maeneo ya Mombo Tanga.

Nimetembelea mara nyingi mkoa huo, sina mwenyeji na hufikia guest house tofauti tofauti, hii mara ya kwanza kusikia habari kama hii.Mwishoni umehitimisha vibaya kwa kusema watu wa watabora, maana siyo wote na wala siyo gesti zote za Tabora. Umetumia kivumishi kijumuishi 😕😕😕
Kwetu yanaitwa mamweneHuyo aliewaokoa alikuwa na masamva....
Naona wengi hapo wamempinga hivyo si vibaya kueleza kuwa yapo yanayofanana nayo.Ndugu una comment kumzidi mleta uzi
Da umenikumbusha mbali hillo jinasawa mboka manyema
A true lie!Hekima kwa anaye kwenda ugenini ni kuwauliza wenyeji kuhusu mazingira,mandhari,utamaduni na kanuni za sehemu uhusika.Lakini imekuwa jambo la kawaida siku hizi mtu akisafiri kwenda ugenini hafati taratibu hizi bali hufanya masuala yake kimya kimya binafsi nimejifunza haswa huu mkoa wa Tabora umenifunza unapoenda ugenini kabla ya kufanya jambo dadisi kwanza.