Suphian Juma
Senior Member
- Apr 2, 2019
- 140
- 579
Unashangaa keki ya miti ikoje? Karibu, ungana nami tupige soga.
Katika utamaduni wa kawaida kama tulivyokopa duniani kote kutoka Misri keki zilipoanza kutengenezwa kwa mara ya kwanza, kila ifikapo siku ya kumbukizi ya kuzaliwa rafiki ama ndugu zetu huwa tunawanunulia ama kuwatengenezea keki kama ishara ya kuonesha upendo.
Leo Januari 27, 2023 ni Siku muhimu mno Tanzania na duniani kwani Rais wa kwanza Mwanamke Tanzania tangu tupate uhuru, Daktari Samia Suluhu Hassan anasherekea siku yake ya KUZALIWA.
Sisi Miss Jungle International kama mradi wa Kimataifa unaolenga kukuza Utalii, kutunza Mazingira na kutangaza Madini yetu duniani, ambapo mimi Suphian Juma ni mmoja wa waanzilishi na waratibu wake, leo Babati mkoani Manyara tumeamua kumzadia Mhe. Rais Dkt Samia miti 500 kama zawadi ya "keki" ya aina yake katika "Birthday" yake.
Tukio hili tumelifanya leo Mjini Babati baada ya mazungumzo ya wiki kadhaa nyuma ya kuishawishi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara chini ya RC Mhe. Makongoro Nyerere kushirikiana nasi katika zoezi la Uzinduzi wa upandaji miti ili kudhibiti athari zitokanazo na Mabadiliko ya tabianchi.
Katika kuenzi Juhudi za dhati za Rais Dkt Samia katika kuhimiza upandaji miti kama alivyosisitiza mara kadhaa alipohudhuria mikutano mbalimbali ya Kimataifa ikiwemo ule wa Umoja wa Mataifa uliofanyika New York Marekani mwaka juzi ambapo alisema hali ya kupanda kwa joto nchini imesababisha ukame, ambao ni athari mbaya kwa sekta zinazotegemea maliasili ambazo ni kilimo, uvuvi na misitu zinazochangia asilimia 30 ya pato la Taifa na kuathiri asilimia 60 ya wananchi;
Hivyo nasi kama vijana wa Kitanzania kupitia mradi wetu wa Miss Jungle International tumeona ni vema tujikite kupanda miti kama zawadi yake Mkuu wa Nchi katika Birthday yake ambapo kwa kuambatana na Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe Makongoro Nyerere na viongozi mbalimbali wa Serikali wa Mkoa na Wilaya zake, leo tumepanda miti 500 pembezoni mwa ziwa Babati.
Kwa upande wetu Miss Jungle International katika zoezi hilo mapema leo nilikwepo mimi nikiambatana na Rais wa Miss Jungle International, Sam Charles Malugu pamoja na Walimbwende wetu Miss Jungle International Tanzania, Dorine Gibson na Beatrice Elias ambapo sote baada ya kupanda miti kama keki kwa Mama, tuliwaongoza pia wananchi wa Babati kumwimbia wimbo Maalum wa Birthday, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.
Mpango wetu Miss Jungle International ni kupanda miti 500 kwa kila Mkoa nchini yaani Bara na visiwani ili kuisaidia Serikali yetu pendwa ya awamu ya Sita kudhibiti Mabadiliko ya tabia Nchi na kuwapa morali wananchi wenzetu kuacha kukata miti hovyo.
Aidha Miss Jungle International tunaishukuru sana Ofisi ya Mkoa wa Manyara kwa Ushirikiano mkubwa wa hali na mali waliyotupatia kufanikisha zoezi hili kwa pamoja, bila kusahau pia wadhamini wetu Mati Super Brands, watengenezaji wa kinywaji cha Tanzanite, pamoja na wananchi wote waliojitokeza kwa wingi kupanda miti nasi na kupokea kwa unyenyekevu mkubwa maelekezo kutoka kwa RC Makongoro ya kuwa na utamaduni endelevu wa kupanda miti kwa wingi majumbani.
Happy Birthday Rais wetu kipenzi, Daktari Samia Suluhu Hassan, tunakutakia kila lililo kheri uzidi kuwa daraja la Umoja, amani, upendo na maendeleo tija kwa Nchi yetu hadi ifikapo 2030.. Inshallah!!
Suphian Juma Nkuwi,
Babati - Manyara
Januari 27, 2023.
Simu: 0717027973