Tulishinikize Bunge limfute kazi JK... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tulishinikize Bunge limfute kazi JK...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 22, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  Viongozi wote wa CCM baada ya uchaguzi wa 2011 wamekuwa wakiimba udini lakini hawaelezei ni kwa nini mwaka 2005 JK alipopata ushindi wa kihistoria hakuna aliyekuwa akilalama na udini..........................Udini wa baada ya uchaguzi wa 2010 unaashiria JK hakushinda ila alishindwa na Dr. Slaa...............

  masheikh walio upande wa JK hawataki kusikia lawama muumini wao akitupiwa jinsi anavyohamisha utajiri wa nchi na kuupeleka ng'ambo na kutuongezea maumivu ya ufukara..............................

  Hakuna mahali masheikh wamewahi kukemea maovu JK na maswahiba wake wanayotufanzia........................................Hata hili la DOWANS ambalo ni wazi Masheikh wamepiga ganzi huku wao ndiyo wanaathirika mno kama raia wengineo wenye kipato kidogo.........................................

  Kwa kuutumia udini kutugawa baada ya uchaguzi wa 2010 wengi ambao siyo waislamu wanaogopa kumkosoa JK wakiogopa kubandikwa jina la udini...........ya kuwa wanampinga Jk kwa sababu tu eti ni Muislamu..............na hivyo kufunika ukweli ndugu yetu huyu ni FISADI NAMBARI ONE..

  mbinu hizi zimempa JK kiburi cha kuendelea kufuja na kupora taifa hili bila woga kwa sababu......once divided apart we fall........................

  Ushauri wangu tuweke mbinu chafu hizi za JK pembeni na kulishinikiza Bunge limchunguze na kama likimtia hatiani limfute kazi.......na tuanze mara moja kazi ya kuijenga nchi yetu upya kwa manufaa ya vizazi vijavyo..........................

  Wabunge JK hakuwachagua hata hao wa CCM ila ni sisi kwa hiyo tuwashinikize wamchunguze kwa maumivu makali aliyotusababishia kwa hili la DOWANS.......na mengineyo yatafuata.......................kama yale ya EPA, RADAR, MEREMETA, KIWIRA.......n.k

  haiwezekani mtu mmoja na vikaragosi vyake vichache wakatuweka rehani sisi watu tulio wengi kwa msingi wa kutugawa na dini zetu ambazo tunaziabudu..........

  Tusipofanya hivyo vizazi vijavyo vitatukumbuka kwa kukumbatia maovu hata kama hatukuwa wanufaikaji wa kwanza.........................
   
 2. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,257
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Ni swala la timing tu, akishtuka yeye ndie atalivunja bunge.
  Na sidhani kama wabunge wenyewe wana uwezo huo kwa kuangalia dhamira zao.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  Akilivunja Bunge ndiyo itakuwa tamu zaidi....................Raisi hawezi kulivunja Bunge kama tayari kashitakiwa.................na hata kama akifanikiwa kulivunja Bunge acha turudi kwenye uchaguzi halafu yeye atakuwa siyo mgombea kwa ni atakuwa amemaliza vipindi vyake viwili...................................inamaansiha atakuwa kajimaliza yeye mwenyewe..........

  Kitendo cha kumshitaki tu kinatosha..........aibu atakayoipata itakuwa imetosha.................................atakuwa Raisi wa kwanza kwenye historia yetu kushitakiwa na Bunge.....................hilo litamwuuma sana JK ambaye amekuwa akihaha kutafuta kujiwekea historia ya kukumbukwa kwa mema.......................................
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  TUnahitaji wabunge asilimia 20 tu ya wabunge wote kufanikisha hii azma.....................wabunge wa Chadema pekee wanatosha kumwandikia spika na kumwomba aanzishe mchakato wa kuchunguza na kumfuta kazi JK kutokana na DOWANS........hili tu litamtikisa...........Na sisi tuanzishe maandamano nchi nzima kuwashinikiza wabunge wa CCM wawaunge mkono wa Chadema kwenye huu mswada.ushahidi upo wazi kabisa kuwa suala zima la DOWANS limevunja katiba ya nchi hii............

  Na mwajibikaji mkuu siyo PM bali ni JK mwenyewe......let us begin to learn to call a spade a spade but not a big spoon...............or even a ladle.................
   
 5. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  hili swala si rahisi kwa nchi inayoongozwa kihuni kama tz, kwani wana CCM wabunge wote ni wanafiki na hawatakuwa wazi kutimiza hilo takwa. si umeona Kamati kuu ya CCM ilivyoongelea hilo la Dowans? inaonekana kwao kuilipa Dowans ni sawa tu, sembuse na wabunge ambao asilimia 60 ni wageni?
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  Kabla ya msukuma mkototeni kule Tunisia hajaamua kujichoma na petroli hakuna aliyeamini inawezekana kumng'oa Ben Ali....kwa hiyo la msingi ni kuamini linawezekana na mengineyo yatafuata.........................................kwanza akumbwe na kura ya kutokua na imani naye na kadamnasi ya wapenda mabadiliko kukusanya sahihi kila jimbo kuwashinikiza wabunge wa CCM kutuunga mkono kwenye hili........................
   
 7. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  The only thing we can do is to make Kikwete resign but how do we start and where??
   
 8. Quinty

  Quinty JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 463
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hiyo ni njia sahihi kabisa ya kumtoa raisi madarakani kwa bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na raisi. Ilanikumbukwe kwamba wabunge wengi bungeni ni wa CCM na itakuwa ngumu kumuaibisha mwenyekiti wao maana wanaangalia zaidi maslahi ya chama dhidi ya maslahi ya taifa. Ule uzalendo wa miaka ya 70 80 haupo tena....!
   
 9. Wakumwitu

  Wakumwitu JF-Expert Member

  #9
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ni hoja nzuri sana kaka lakini siyo kwa Tanzania yetu. Ingekuwa kama Tunisia ingewezekana. Tatizo la watanzania unafiki mwingi, kama serikali inaweza kuridhia kuilipa Dowans mabilioni ya pesa, Pia serikali hiyo hiyo itatumia pesa hizohizo za wananchi kuhakikisha kila mbuge wa CCM anapewa bilioni moja ama mbili na mjadala utakuwa kwushinei. Alafu utasikia bodi ya mikopo haina hela kwa sababu bado hajapewa kutoka hazina, walimu hawajalipwa masurufu yao, nk. Uliza pesa zimeenda wapi, mifukoni mwa watu ili tuu walinde masilahi yao. Hii ni Tanzania bwana.
   
 10. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #10
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,728
  Likes Received: 1,636
  Trophy Points: 280
  labda peoples power , sitta tu kadhubutu kumwambia ukweli, mzee chill sos, siju chillgati kamkemea, wapo wengi wanaolindana waoga kama fisi, lait kama angekuwepo Seleleii ambaye walifanya kilamja kumtoa, wwengi wanajali matumbo yao , pia anasupportiwa na Udini aliouanzisha kutuziba midomo, ukisema wanatelea kuwa kaonewa kwa kuwa yeye ni mwislam wakati Hana Uislam wowote, wanaojua maana ya kuitwa Muislam ni mtu Nyenyekefu kwa Mungu sio dhulumati, Mpenda haki, sasa yeye anaongoza CCM kudhulumu haki za Watz, kwa kivuli cha kutokewewa kwa kuwa eti kumkemea tayari umembagua, sasa kilichobaki ni PP, sio Bunge, waambie wabunge kwanza wajari matumbo yety na sie sio kujijazia hizo hela wakatusahau
   
 11. B

  Batale JF-Expert Member

  #11
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,070
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Hilo litakuwa gumu ndugu yangu, kwa wabunge wasiojiamini wa CCM? Labda ingekuwepo sheria rais akipingwa bungeni na idadi ya wabunge kufikia 45 naamini hoja yako ingekubalika, lamsingi ni ss wananchi kuandamana mpaka yeye mwenyewe aseme basi kama Tunisia.

  [
   
 12. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Je? Wabunge wa CCM wako tayari kumuwajibisha Mweneyekiti wao kwa kumpigia kura ya kutokuwa na imani nae the answer is no maana ni wanafiki na wazandiki wakiishapewa hela na kupelekwa semina wanakuwa wamefungwa midomo
   
 13. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #13
  Jan 22, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  wananchi wakianza kudai na kukiwa na msukumo wa mabadiliko inawezekana ila kinachonipa wasiwasi ni wabunge wa ccm maana mimi naona ni wanafiki wa kutupwa
   
 14. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #14
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kuwa na akili ni pamoja na kujua linalowezekana na lisilowezekana.

  Hili ni jambo zuri na rahisi sana kuliongea na kulisikiliza lakini lisilowezekana kwa mazingira ya Tanzania, CCM ina uwingi wa kutosha bungeni na majority ya Watanzania hawayajali haya maneno maneno ya kisiasa yanayoendelea kwenye vyombo vya habari, wanachojua wao ni kuwa walishamaliza uchaguzi wa 2010 na sasa wanasubiri tu kumchagua Rais mwingine mwaka 2015, hawana haja ya kuangalia kama ahadi walizoahidiwa zimetekelezwa au la, na wala hawajui uhusiano wa ugumu wa maisha yao na serikali iliyopo madarakani.

  Ndio maana JK alikuwa akijigamba bila hofu kuwa aliitekeleza ilani ya 2005-2010 kwa zaidi ya 98% na Watanzania bila hiyana wakawa wanampigia makofi tu na kushangilia, bado tuna safari ndefu sana kuliko unavyoweza kuona ukiwa nyuma ya PC.
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Jan 22, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa nini Bunge? Kwa nini si wananchi ambao tumemuajiri?
   
 16. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #16
  Jan 22, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Inasikitisha pale ambapo wanamchi tunapewa madaraka ya kuamua nani atuongoze tunayatumia vibaya, ni miezi miwili na ushee tu, tangu tumekubali kumrudisha madarakani. Why tunataka aachishwe kazi wakati sie ndo tumemweka?? Nafikiri watanzania tukiungana pamoja na kuwa na maamuzi ya pamoja tutaepuka haya yote.

  Najua wapo watakaosema juu ya uchakachuaji wa kura, lakini bado kama watu tungekuwa na msimamo na uhakika wa kura zetu hata wao wangeshindwa kuchakachua
   
 17. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #17
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Haya ya uchakuaji ni kisingizio tu cha kujaribu kuepuka kuitazama hali halisi isiyovutia kuitazama.
   
 18. popiexo

  popiexo JF-Expert Member

  #18
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 743
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  % 60 ya wabunge ni watu wake hivyo kura ya kutokuwa na imani nae bungeni sio rahisi kupita. Nashauri ni bora tuamue moja kuwaiga waTunisia, waYugoslavia au waRomania.
   
 19. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #19
  Jan 22, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  ujue alichakachua kura. Uyu msafiri nakuhakikishia %100 hawezi kuvunja bunge hata siku moja. Kumbuka akivunja bunge alaf 2/3 wa wabunge wa sasa wakachaguliwa tena basi yeye anajiuzuru. Kumbuka tangu uhuru kuna zaidi ya 40%ya wabunge wa ccm kila uchaguzi wanarudi bungeni,pia msafiri akiitisha uchaguzi mwingne lazima %iyo irudi,ukiunganisha na wale wapya akina shingongo,maji marefu na wabunge woote wa upinzani wakirudi,itafikia 68%ya bunge la sasa na hapo mkwere atakuwa amejipeleka Msoga kupumzika. Jamani kuvunja bunge ni very technical si rahisi ivo,sheria zake zaweza kumweka mkwere pembeni. Bora tu aliache bunge liamue kwa busara za sheria zenyewe!
   
 20. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #20
  Jan 22, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,741
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  Mimi hapa ndipo napochoka kwa nini watanzania tuna mtindo wa kukatishana tamaa badala ya kujengana moyo. Linawezekana kwa nini lisiwezekane. Tunisia hawakujua lingekuwa lililokuwa sasa ni vipi Tz. tushindwe. Anaweza akatoka tu kwani aliingiaje? Kibarua kitaota nyasi tu mwaka huu asituletee za kuleta. Tumechoka kila siku kusikia mara DOWANS,ATC,RAILWAYS,EPA,RICHMOND tutalipa tubakie hatuna kitu kwa uzembe wa mtu mmoja na vilaza wake. Mimi nimewachoka hawa watu.
   
Loading...