Tulipofika kama ni injini ya gari tunatakiwa kununua mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tulipofika kama ni injini ya gari tunatakiwa kununua mpya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Inkoskazi, Apr 20, 2010.

 1. I

  Inkoskazi Member

  #1
  Apr 20, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Wakati tunapata uhuru nchi yetu ilikuwa ni kama injini mpya ya gari (standard), ikaongozwa na baba wa taifa hadi alipoamua kung'atuka ili apishe wengine kuongoza na kurekebisha pale yeye alipokosea na kuendeleza mazuri aliyoyaanzisha. Kwahali hiyo, tukachonga upya "crank shaft" na kubadlisha vipuri vya injini (utawala) wetu na kumuingiza mzee ruksa madarakani.
  Baada ya miaka kumi, ili gari letu liweze kuendelea na safari tukachonga tena "crank shaft" kwenda size kubwa na kubadlisha vipuri vingi pamoja na ushauri wa mafundi kwamba kuna injini nyingine nzuri (CUF, NCCR-MAGEUZI, CHADEMA, TLP, nk) zinazoweza kufungwa kwenye gari yetu lakini hatukufuata ashauri wao, tukamsikiliza baba wa taifa kwamba safari hii tusiwe na wasi wasi kwani uchongaji wa "crank shaft" umefanywa kimakini mno na vipuri vyote ni genuine.
  Lahaula alakuat!!!!! Guarantee ya miaka kumi tuliyopewa na mafundi wala haikufika, kwani baada ya miaka mitano tuu injini imeanza kugonga upya na kutoa moshi mithili ya treni. Bahati mbaya zaidi baba wa taifa ambaye ndie aliyetupeleka kwenye hii garage ameshafariki na mwenye garage hatutambui. Tukahadaika kutumia mafundi wa miembeni ili kulinusuru gari letu kwani pamoja na kwamba zile injini nyingine(mpya)bado zipo tena safari hii zimekuja na nyingine nzuri tuu, mabangaizaji hawa wa mitaani wakatuhakikishia kuwa hakuna shida yoyote kwani watatupa hata na fundi mmoja wa kuendelea nae na safari yetu. Wakavipiga msasa na kuvisafisha vipuri vile vile vikang'aa kama vipya tukavinunua huku tukifurahia kwamba sasa naam safari tutafika na fundi makanika tunae. Looh, hata miaka mitano ya guarantee haijatimia balaa kubwa limetukuta. Radiator imepasuka, exhaust pipe imekatika, timming belt imeruka kiasi kwamba gari haikai silence, carburator imepanuka jets kiasi kwamba gari inakunywa mafuta kuliko uwezo wetu na bado makanika tuliye nae anasema msiwe na wasiwasi, kwa vile bado mko kwenye guarantee nitawachomea radiator na exhaust pipe bure,nitaunganisha timming belt na super glue na hata carburator nitawasafishia bure na safari nitawapeleka salama.
  Jamani nadhani tunachosubiri ni kukatikiwa break na hili gari kwenye mteremko mkali na madhara yake kila mmoja wetu anayajua. Tusikubali tena maneno ya mafundi wa garage iwe ni dealer au ya mwembeni, hii injini (utawala) ilipofika basi haiwezi tena kuchongwa "crank shaft" kwani imeshafika size ya mwisho na ni ya kizamani mno hata vipuri vyake hakuna tena madukani. Kilichobaki ni kutizama katika injini mpya zinazouzwa hivi sasa (CUF, CHADEMA, TLP, PONA, NCCR,nk) nasikia kuna nyingine iko bandarini inamalizia taratibu za forodha/ushuru kabla ya kuingia kwenye soko (CCJ) tuzisome manual zake vizuri ili tuweze kununua inayofaa kulingana na matumizi yetu.
  "Moringe wote ni Wamasai lakini sio kila Mmasai ni Moringe"
   
Loading...