Wazo la kabwela
JF-Expert Member
- Feb 13, 2013
- 1,894
- 1,485
Tulipoambiwa "Watumishi hewa" tukashangilia sana, japo hatukuwaona
Wakaja waliofoji vyeti na kutumia "Vyeti fake" wakapugwa bila huruma, ndipo wengine tukahoji uhalali wa DAUDI Albert.
Limekuja la wenye elimu ya Darasa la saba, watu ambao waliajiriwa kwa Qualification hiyo, wanajua kuendesha magari, wanajua kufagia vyoo, wanapiga deki, na kweli wengi wanajua kututengea chai na chakula maofisini. Na leo hii tunaambiwa waondoke. Yaani kazi zao na Taaluma ya makaratasi wapi na wapi?
Unajiuliza Dereva ambaye aliajiriwa kwa cheti chake cha Darasa la Saba, na veta, ameendesha Gari la Mkurugenzi kwa Zaidi ya miaka mitanno bila kupata ajari, yaani hakuwahi kuiba mafuta, anaondolewa kazini, haambiwi hata hatima yake iwapo atalipwa chochote au lah.
Yupo mhudumu, mfagizi wa chooni, anajua sana kupiga deki, kama ilivyo kwa Dereva, naye Amefanya kazi takribani miaka kumi, ghafla anasitishiwa mshahara anaambiwa Ondoka ofsini, kabidhi kila kitu.
Anao watoto kibao, anaye mke ambaye naye hana kazi, Watoto wake wanasoma, yeye mwenyewe alipoanzisha kibiashara chake, alihamishwa kazi, kwahiyo hana hata kibanda cha kuuza mchicha, Naye ni Mtanzania, nasema si Mkimbizi, jiulize ingekuwa wewe.
Tunaposema haya mambo yakikufika ndipo utajua hali ilivyo ngumu na ngafu, tuendelee kusifu ili likitufika nasi tusimulie kama wenzetu.
Lakini katikati ya haya, unasikia eti Sifa ya Mkuu wa mkoa au Waziri haihitaji kuwa msomi wa kiwango kikubwa, yaani kwamba ati Nafasi zao ni za kisiasa. Wewe shangilia yanayowakuta wenzako, kwani hata hawa darasa la saba yanayowakuta, hawakujua kama itakuwa hivi. Kipindi yanawakuta wenye vyeti fake walidhani wako salama.
Sijafahamu kama hili agizo la Darasa la saba limetoka kwa Rais, nakumbuka Rais alisema "Mtu afanye kazi inayolingana na Taaluma yake" Najiuliza iwapo Udereva unahitaji taaluma kubwa Zaidi ya uendeshaji vizuri? Je Ufagizi au uhudumu unahitaji taaluma gani?
Anyway Yangu macho, na masikio nayatega kushuhudia mengi Zaidi. kwani ndo kwanza mwaka wa pili huu.
Fundi Mkuu
Kupika mtori lazima ujue kiingereza? Kupika makongoro nako ujue kiingereza?Magari ya siku hizi ni computer controlled, inatakiwa awe na uelewa wa kusomea na kuelewa maelekezo kwenye dashboard. Sasa darasa la saba la miaka hii si anafanya miujiza?
Hata jikoni siku hizi kama haujuwi kusoma na kuelewa Kingereza ni kasheshe.
Nawashauri walioishia darasa la saba wote wakipata fursa waende hata shule za watu wazima wakajiendeleze na masomo.
We mama unaelewa lakini jamaa anachokisema au unaamua tu kujitoa ufahamu?,sasa hilo gari computer controlled miaka ya nyuma kabla hajatolewa kazini alikuwa analiendeshaje,hawa hawakufoji vyeti,waliajiriwa ilhali mwajiri akijua kuwa wemeishia la saba.ila wewe huoni kama kilichofanyika sio fair,siku zote aliyeshiba hawezi jua adha ya mwenye njaa.unadhani walipenda kuishia la saba?Magari ya siku hizi ni computer controlled, inatakiwa awe na uelewa wa kusomea na kuelewa maelekezo kwenye dashboard. Sasa darasa la saba la miaka hii si anafanya miujiza?
Hata jikoni siku hizi kama haujuwi kusoma na kuelewa Kingereza ni kasheshe.
Nawashauri walioishia darasa la saba wote wakipata fursa waende hata shule za watu wazima wakajiendeleze na masomo.
Hivi hayo magari computer control hayatumii krach wala staring??? AuMagari ya siku hizi ni computer controlled, inatakiwa awe na uelewa wa kusomea na kuelewa maelekezo kwenye dashboard. Sasa darasa la saba la miaka hii si anafanya miujiza?
Hata jikoni siku hizi kama haujuwi kusoma na kuelewa Kingereza ni kasheshe.
Nawashauri walioishia darasa la saba wote wakipata fursa waende hata shule za watu wazima wakajiendeleze na masomo.
Sikia sababu zao sasa we unataka kunambia cku hz kuna magari mapya yenye maelekezo kwny dashboard tofauti na magari ya miaka mi5 iliyopita? Duuuh watu hata vitu vibaya wanavyofanyiwa wenzenu nyie mnaviremba tu vionekane vzr experience ndo ina matter hapo iyo sio sheria au sindano bnaMagari ya siku hizi ni computer controlled, inatakiwa awe na uelewa wa kusomea na kuelewa maelekezo kwenye dashboard. Sasa darasa la saba la miaka hii si anafanya miujiza?
Hata jikoni siku hizi kama haujuwi kusoma na kuelewa Kingereza ni kasheshe.
Nawashauri walioishia darasa la saba wote wakipata fursa waende hata shule za watu wazima wakajiendeleze na masomo.