oyieko
JF-Expert Member
- Dec 31, 2015
- 308
- 375
Ngogoyo
Sent using kvant
Mwaka fulani nkiwa nipo mjini Tarime kimakazi,around 2000s Sasa pale Tarime mjini kila siku ya Jpili huwa kuna Gulio wenyewe wanaitaga siku ya soko,nkiwa napita mitaa fulani hv kuna jamaa nkawakuta wanacheza ile michezo ya kuchanganya viberiti au kekundu na keusi.
Kwa wakati ule ukizingatia na udogo nilokuwa nao ikabidi nkae nitazame wenye fweza zao wanavyonaswa nao hao jamaa,kiukweli pipo zilikuwa nyomi,sasa kuna Mkurya mmoja alikuwa na wenzake wakawa wamepita pale na wakavutiwa kucheza,na kwamujibu wa maongezi yao baada ya tukio lile inaeleka jamaa walikuwa wametoka kuuza mikungu ya ndizi kadhaa pale gulioni.
MKASA NA VURUMAI
Mmoja wa wale jamaa akavutika na hatimaye akajikuta ana nasa kwenye ule mchezo,mchezo ukaendelea kwa kasi huku raia wengine tukiwa watazamaji na mashuhuda,jamaa akaliwa kipindi cha kwanza,na akacheza tena hatimaye akala,alipo bahatisha kiberiti chenye njiti husika yaani kula wale jamaa wakamwambia inabidi uweke kiasi fulani cha pesa ili ukomboe pesa yako uliyoliwa,jamaa pasi na hiyana akatia mzigo,akapigwa!,kuanzia hapo sasa mwendo ukawa wa kuliwa tu,yeye akila anaambiwa tia mzigo ukomboe uliyoliwa,Jamaa baadae anakuja kushtuka kapigwa pesa yote na kabaki mtupu.
Sasa inaonekana wale wenzake wakaanza kumnanga kwa ki-lugha (kikurya) " Leo utaenda kumwambia nini baba yako,leo utapigwa mpaka ufe Chacha"-nimejaribu kutafsiri kikurya,Jamaa kusikia vile akaanza kulia mpaka kamasi zinamtoka sasa ikabidi aanze kuwaambia jamaa wamrudishie pesa yake,wale jamaa wakawa wanachukulia kama utani huku wakiendelea kuliza watu wengine kama kawaida.
Aisee usiombe kushuhudia vita ya Mkurya akiwa kachachamaa,wale jamaa zake walitoa mapanga na wakaanza kuwacharaza wale jamaa huku jamaa akidai pesa zake,sasa miongoni mwa wale jamaa wachezesha viberiti alipata upenyo akakimbia na zile hela na jamaa wakaanza kumfukuza,nilichoshuhudia ni jamaa kakamatwa na kapigwa mapanga ya kufa raia,Wale jamaa walifanikiwa kuzipata hela zao na ikabidi warudi kule kwa wale jamaa wa mwanzo waloanza kuwashughulikia,sasa kwa madai yao walianza kuwaita "WASAGHANE"-Tafsiri yake ni mwanamke ambaye hajatahiriwa,walipigwa mapanga mpaka difenda ya polisi inakuja pale ilibidi waondoke maana wakurya wamechachamaa na walishindwa kutuliza ule "Mzuka"wa wale jamaa....
Kiukweli mi ilibidi nichanje mbuga maana nilihofu usalama wangu...
TOKA HAPO NKASEMA HAWA JAMAA ZETU (WAKURYA)HAWAFAI HATA KIDOGO,NYIE WAONENI TU
Tulia hivyo hivyo dawa ikuingie..![]()
Sent using kvant



