Tuliowahi kutapeliwa tukutane hapa

Tuliowahi kutapeliwa tukutane hapa

Ngogoyo
Mwaka fulani nkiwa nipo mjini Tarime kimakazi,around 2000s Sasa pale Tarime mjini kila siku ya Jpili huwa kuna Gulio wenyewe wanaitaga siku ya soko,nkiwa napita mitaa fulani hv kuna jamaa nkawakuta wanacheza ile michezo ya kuchanganya viberiti au kekundu na keusi.
Kwa wakati ule ukizingatia na udogo nilokuwa nao ikabidi nkae nitazame wenye fweza zao wanavyonaswa nao hao jamaa,kiukweli pipo zilikuwa nyomi,sasa kuna Mkurya mmoja alikuwa na wenzake wakawa wamepita pale na wakavutiwa kucheza,na kwamujibu wa maongezi yao baada ya tukio lile inaeleka jamaa walikuwa wametoka kuuza mikungu ya ndizi kadhaa pale gulioni.

MKASA NA VURUMAI

Mmoja wa wale jamaa akavutika na hatimaye akajikuta ana nasa kwenye ule mchezo,mchezo ukaendelea kwa kasi huku raia wengine tukiwa watazamaji na mashuhuda,jamaa akaliwa kipindi cha kwanza,na akacheza tena hatimaye akala,alipo bahatisha kiberiti chenye njiti husika yaani kula wale jamaa wakamwambia inabidi uweke kiasi fulani cha pesa ili ukomboe pesa yako uliyoliwa,jamaa pasi na hiyana akatia mzigo,akapigwa!,kuanzia hapo sasa mwendo ukawa wa kuliwa tu,yeye akila anaambiwa tia mzigo ukomboe uliyoliwa,Jamaa baadae anakuja kushtuka kapigwa pesa yote na kabaki mtupu.

Sasa inaonekana wale wenzake wakaanza kumnanga kwa ki-lugha (kikurya) " Leo utaenda kumwambia nini baba yako,leo utapigwa mpaka ufe Chacha"-nimejaribu kutafsiri kikurya,Jamaa kusikia vile akaanza kulia mpaka kamasi zinamtoka sasa ikabidi aanze kuwaambia jamaa wamrudishie pesa yake,wale jamaa wakawa wanachukulia kama utani huku wakiendelea kuliza watu wengine kama kawaida.
Aisee usiombe kushuhudia vita ya Mkurya akiwa kachachamaa,wale jamaa zake walitoa mapanga na wakaanza kuwacharaza wale jamaa huku jamaa akidai pesa zake,sasa miongoni mwa wale jamaa wachezesha viberiti alipata upenyo akakimbia na zile hela na jamaa wakaanza kumfukuza,nilichoshuhudia ni jamaa kakamatwa na kapigwa mapanga ya kufa raia,Wale jamaa walifanikiwa kuzipata hela zao na ikabidi warudi kule kwa wale jamaa wa mwanzo waloanza kuwashughulikia,sasa kwa madai yao walianza kuwaita "WASAGHANE"-Tafsiri yake ni mwanamke ambaye hajatahiriwa,walipigwa mapanga mpaka difenda ya polisi inakuja pale ilibidi waondoke maana wakurya wamechachamaa na walishindwa kutuliza ule "Mzuka"wa wale jamaa....

Kiukweli mi ilibidi nichanje mbuga maana nilihofu usalama wangu...

TOKA HAPO NKASEMA HAWA JAMAA ZETU (WAKURYA)HAWAFAI HATA KIDOGO,NYIE WAONENI TU

Tulia hivyo hivyo dawa ikuingie..

Sent using kvant
 
Mi nilitapeliwa na wauni arusha walinikaribisha mjini kwa kweli nilipita mtaa Fulani nikakuta kuna mnada wa vitu mbali mbali kama laptop, tv ,simu na kadhalika kwa haraka haraka nikaona Samsung s9 nikauliza hii bei gani mi nikakata ofa 50k ikaanza kupigwa mnada Mara kunamwingine kapanda mpaka 120k mi nikaamuwa kufunga hesabu nikatamka 150k Mara baada ya kutamka 150k nikaskia top 150k kumaanisha Mimi ndio nimeshinda nikachukua chaja na simu na kilakitu kufika getto nikaweka simu kwenye chaji ikalala kabisa kesho yake nawasha simu ,simu inawaka na kwenye kioo yakatoka maandishi ya neno ( princess ) nikajua hapa nishaliwa nikatafuta demu nikamwonga tu .

Sent using Jamii Forums mobile app
karibu mjini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umenikumbusha mbali stori yako ni kama ya kwangu, mwanza vile vile maeneo ya kirumba natokea tuition jioni nyakabungo mwaka 2015, jamaa alitokea mbele angu amechakaa kweli kweli maelezo kama uliotoa . Yeye alidai anaitaji msaada wa mtu kumpeleka sehemu wanaponunua madini au kwa sonara.. nilimwambia kuwa mimi ni mgeni hapa mjini kwahyo sijui ni wapi wanapatikana masonara.. nilpokuwa bado naongea nae nataka kuondoka gafla katokea jamaa mwingine, kaja kajifanya ajui kinachoendelea ndo jamaa kamsimlia yule akasema anafahamu walipo masonara kwo atamsaidia kumpeleka. Hapo nkataka kuondoka zangu wakasema hapa subiri tumsaidie jamaa kumpeleka kwa sonara akiuza tutakupa mgao kidogo ... Safari ikaanza kutembea kwenda kwa sonara, mbele kidogo yule jamaa mwenye mali akasema ana njaa ajala siku nzima ndo wakanambia una shingap hapo tumpe jamaa ale chakula kwanza tukiuza unapata hela yako .. mfukoni nilikuwa na na elfu 5 noti na simu ya smart yenye touch na batati kwa pamoja nahis mnazikumbuka hiz simu .. wakasema mimi niende na mzigo had kwa sonara watanikuta hapo nawasubiri, maana yule aliekuja kujifanya kutoa msaada wa wapi wanapatikana masonara alisema wanapatikana Misheni. Wakanambia nimwachie mwenye mzigo simu ili nisije kukimbia na mali . Nkaacha simu na hela nshawapa, mimi uyo hadi misheni kulikuepo na jengo la ghorofa kabla alijavunjwa , nilikaa misheni tangu saa kumi na mbili hadi saa mbili kasoro bila wale jamaa kutokea .. ndo nkaanza kuhisi nshaibiwa, Ikabidi nainze kutembea tena kutoka mishen hadi bwiru kwa bro... Nilifika nawaelezea kwamba nimekuja na madini .... Kabla sijamalza kuwasimlia walishaanza kucheka kwamba tiyari ushaibiwa . Kuwapa bahasha ya kaki kuifungua ndan kokoto sio madini tena wakati niliona kwa macho yangu hapo kabla ... Yaani nilitokwa jasho mwili mzima .. ndo nkawa nimeliwa simu na hela hivyo....

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilivyoibiwa boda boda

Nipo kijiwen nikisubiri abiria mara wakaja waaume wawili mmja mtu wa makamo 40/55 amevaa miwani mweusi akionekana ni mtu mwenye ulemavu wa macho (kipofu) na mwengine ambae ni kijana Kati ya miaka 18/25 akimsadia kumuongoza njia huku wote wamekamata ile fimbo.
Wamefika kwangu yule kijana akanambia huyu abiria anaenda manzese darajani sh ngap?.Nikamwmbia buku tatu kipofu akaomba nimsaidie ana elf 2 nikakubali nikampakia mbele kdogo kipofu akaangusha fimbo yake akanmbia samahn fimbo yang imeanguka nikasimam nikaangalia kweli nikaiona haikuwa mbal na niliposimama

Si nikajichanga kwenda kumuokotea fimbo bila kuizima boxer yangu kudadeq hatua kama tano hivi nikasikia chombo inapigwa race ya kufa mtu kugeuka nyuma mtumeee kipofu anaendasha pikipiki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umenikumbusha mbali stori yako ni kama ya kwangu, mwanza vile vile maeneo ya kirumba natokea tuition jioni nyakabungo mwaka 2015, jamaa alitokea mbele angu amechakaa kweli kweli maelezo kama uliotoa . Yeye alidai anaitaji msaada wa mtu kumpeleka sehemu wanaponunua madini au kwa sonara.. nilimwambia kuwa mimi ni mgeni hapa mjini kwahyo sijui ni wapi wanapatikana masonara.. nilpokuwa bado naongea nae nataka kuondoka gafla katokea jamaa mwingine, kaja kajifanya ajui kinachoendelea ndo jamaa kamsimlia yule akasema anafahamu walipo masonara kwo atamsaidia kumpeleka. Hapo nkataka kuondoka zangu wakasema hapa subiri tumsaidie jamaa kumpeleka kwa sonara akiuza tutakupa mgao kidogo ... Safari ikaanza kutembea kwenda kwa sonara, mbele kidogo yule jamaa mwenye mali akasema ana njaa ajala siku nzima ndo wakanambia una shingap hapo tumpe jamaa ale chakula kwanza tukiuza unapata hela yako .. mfukoni nilikuwa na na elfu 5 noti na simu ya smart yenye touch na batati kwa pamoja nahis mnazikumbuka hiz simu .. wakasema mimi niende na mzigo had kwa sonara watanikuta hapo nawasubiri, maana yule aliekuja kujifanya kutoa msaada wa wapi wanapatikana masonara alisema wanapatikana Misheni. Wakanambia nimwachie mwenye mzigo simu ili nisije kukimbia na mali . Nkaacha simu na hela nshawapa, mimi uyo hadi misheni kulikuepo na jengo la ghorofa kabla alijavunjwa , nilikaa misheni tangu saa kumi na mbili hadi saa mbili kasoro bila wale jamaa kutokea .. ndo nkaanza kuhisi nshaibiwa, Ikabidi nainze kutembea tena kutoka mishen hadi bwiru kwa bro... Nilifika nawaelezea kwamba nimekuja na madini .... Kabla sijamalza kuwasimlia walishaanza kucheka kwamba tiyari ushaibiwa . Kuwapa bahasha ya kaki kuifungua ndan kokoto sio madini tena wakati niliona kwa macho yangu hapo kabla ... Yaani nilitokwa jasho mwili mzima .. ndo nkawa nimeliwa simu na hela hivyo....

Sent using Jamii Forums mobile app
😂😂Nyakabungo kwa Maiko
 
nipp ofisini maeneo ya josam House, mwenge. simu inaita ni namba mpya.
haloo!
mambo vipi? za siku nyingi aisee bora nimekupata maana nimetafuta namba yako nimepewa na Alex( alex yupi?) akaendelea yule jamaa mpole hivi pale chuo?? nkamwambia ni kitambo. okey unasemaje?

akaanza kusema anahitaji msaada kuna ndugu yake anafanya kazi ya ulinzi Tamco wanatafuta sehemu wakauze mzigo wa chuma chakavu kama tani 40. ila wana mzigo zaidi ya tan 100, ukifanikisha unapata tan 25. dili watu 4.
nkasema hapa ndo penyewe. nipe dakika 20 nipge Tabata Dampo, wakaniambia dampo hawana hela kuna wakala wa kununua chuma chakavu kiwanda cha Nondo kilo wanauza 450. ila wanatoa 500 kama gharama za usafiri ni zako. Sasa kwa sababu huu mzigo umetolewa usiku na jamaa anaingia shift saa 8 wewe tunakuamini tunakupa namba ya simu ya wakala mpgie umalizane naye sie tutafute gari( akili ikachangamka nkasema hapa naingizwa mjini, kuna shemeji yangu yupo mlimani nkampgia nkampanga nkasema ntajie location ya hizi namba)
akanijibu hazipo pwani zipo.makumbusho. nkamwambia poa asante.

Nkamwendea wakala wa kununua chuma chakavu, akasema hali ya uchumi imeshuka kwa hyo wananunua 350 usafiri juu yako. ila kama zinazidi tani 50 wanaweza fanya kwa kilo 400 pamoja na usafir.

nkarudisha majibu kwa jamaa, wakaniambia poa inabidi wewe tukuongezee tani 5 maana umepambana kinoma, nkamwambia asante.

sasa Brother inabidi uje na gari, mpgie yule wakala. umwelekeze kuwa mkifika tamko Kibaha kuna kama kibanda hivi unakuta wanakagua malori ya michanga jamaa anawasubiria hapo, fasta mzee baba.

Mara wakala anapga simu, brother kuna changamoto kidogo imetokea dereva hana mafuta anakwepa foleni na trafiki so tuma hata 300k ili tuanze naye.

nkawajibu poa, mie nakuja inabdi nije CRDB kijitonyama kutoa hela so tukutane ubungo.
nkakaa kimya mara mwanapga mara kibao, nkawaambia foleni kubwa benk hapa, mwishowe nkawaambia mbona naona namba zenu zipo hapa jirani na makumbusho. wapi makumbusho wanakodi malory ya tan30? nkacheka, aisee nilitukanwa matusi. mie nkasema sawa .
kwa sababu kila nilsave namba zao, siku nashangaa Msg inaingia jina saved tapel 1.
"Mjukuu wangu ile, dawa ya kukupa utajir...mavi! mavi na..."
nkamjibu siku hizi babu huuzi vyuma chakavu?

Mbwa sana wale

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka fulani nkiwa nipo mjini Tarime kimakazi,around 2000s Sasa pale Tarime mjini kila siku ya Jpili huwa kuna Gulio wenyewe wanaitaga siku ya soko,nkiwa napita mitaa fulani hv kuna jamaa nkawakuta wanacheza ile michezo ya kuchanganya viberiti au kekundu na keusi.
Kwa wakati ule ukizingatia na udogo nilokuwa nao ikabidi nkae nitazame wenye fweza zao wanavyonaswa nao hao jamaa,kiukweli pipo zilikuwa nyomi,sasa kuna Mkurya mmoja alikuwa na wenzake wakawa wamepita pale na wakavutiwa kucheza,na kwamujibu wa maongezi yao baada ya tukio lile inaeleka jamaa walikuwa wametoka kuuza mikungu ya ndizi kadhaa pale gulioni.

MKASA NA VURUMAI

Mmoja wa wale jamaa akavutika na hatimaye akajikuta ana nasa kwenye ule mchezo,mchezo ukaendelea kwa kasi huku raia wengine tukiwa watazamaji na mashuhuda,jamaa akaliwa kipindi cha kwanza,na akacheza tena hatimaye akala,alipo bahatisha kiberiti chenye njiti husika yaani kula wale jamaa wakamwambia inabidi uweke kiasi fulani cha pesa ili ukomboe pesa yako uliyoliwa,jamaa pasi na hiyana akatia mzigo,akapigwa!,kuanzia hapo sasa mwendo ukawa wa kuliwa tu,yeye akila anaambiwa tia mzigo ukomboe uliyoliwa,Jamaa baadae anakuja kushtuka kapigwa pesa yote na kabaki mtupu.

Sasa inaonekana wale wenzake wakaanza kumnanga kwa ki-lugha (kikurya) " Leo utaenda kumwambia nini baba yako,leo utapigwa mpaka ufe Chacha"-nimejaribu kutafsiri kikurya,Jamaa kusikia vile akaanza kulia mpaka kamasi zinamtoka sasa ikabidi aanze kuwaambia jamaa wamrudishie pesa yake,wale jamaa wakawa wanachukulia kama utani huku wakiendelea kuliza watu wengine kama kawaida.
Aisee usiombe kushuhudia vita ya Mkurya akiwa kachachamaa,wale jamaa zake walitoa mapanga na wakaanza kuwacharaza wale jamaa huku jamaa akidai pesa zake,sasa miongoni mwa wale jamaa wachezesha viberiti alipata upenyo akakimbia na zile hela na jamaa wakaanza kumfukuza,nilichoshuhudia ni jamaa kakamatwa na kapigwa mapanga ya kufa raia,Wale jamaa walifanikiwa kuzipata hela zao na ikabidi warudi kule kwa wale jamaa wa mwanzo waloanza kuwashughulikia,sasa kwa madai yao walianza kuwaita "WASAGHANE"-Tafsiri yake ni mwanamke ambaye hajatahiriwa,walipigwa mapanga mpaka difenda ya polisi inakuja pale ilibidi waondoke maana wakurya wamechachamaa na walishindwa kutuliza ule "Mzuka"wa wale jamaa....

Kiukweli mi ilibidi nichanje mbuga maana nilihofu usalama wangu...

TOKA HAPO NKASEMA HAWA JAMAA ZETU (WAKURYA)HAWAFAI HATA KIDOGO,NYIE WAONENI TU

Tulia hivyo hivyo dawa ikuingie..
Vita Ni Vita Mura, Tarime tutaghutuna ubhukangi
 
nipp ofisini maeneo ya josam House, mwenge. simu inaita ni namba mpya.
haloo!
mambo vipi? za siku nyingi aisee bora nimekupata maana nimetafuta namba yako nimepewa na Alex( alex yupi?) akaendelea yule jamaa mpole hivi pale chuo?? nkamwambia ni kitambo. okey unasemaje?

akaanza kusema anahitaji msaada kuna ndugu yake anafanya kazi ya ulinzi Tamco wanatafuta sehemu wakauze mzigo wa chuma chakavu kama tani 40. ila wana mzigo zaidi ya tan 100, ukifanikisha unapata tan 25. dili watu 4.
nkasema hapa ndo penyewe. nipe dakika 20 nipge Tabata Dampo, wakaniambia dampo hawana hela kuna wakala wa kununua chuma chakavu kiwanda cha Nondo kilo wanauza 450. ila wanatoa 500 kama gharama za usafiri ni zako. Sasa kwa sababu huu mzigo umetolewa usiku na jamaa anaingia shift saa 8 wewe tunakuamini tunakupa namba ya simu ya wakala mpgie umalizane naye sie tutafute gari( akili ikachangamka nkasema hapa naingizwa mjini, kuna shemeji yangu yupo mlimani nkampgia nkampanga nkasema ntajie location ya hizi namba)
akanijibu hazipo pwani zipo.makumbusho. nkamwambia poa asante.

Nkamwendea wakala wa kununua chuma chakavu, akasema hali ya uchumi imeshuka kwa hyo wananunua 350 usafiri juu yako. ila kama zinazidi tani 50 wanaweza fanya kwa kilo 400 pamoja na usafir.

nkarudisha majibu kwa jamaa, wakaniambia poa inabidi wewe tukuongezee tani 5 maana umepambana kinoma, nkamwambia asante.

sasa Brother inabidi uje na gari, mpgie yule wakala. umwelekeze kuwa mkifika tamko Kibaha kuna kama kibanda hivi unakuta wanakagua malori ya michanga jamaa anawasubiria hapo, fasta mzee baba.

Mara wakala anapga simu, brother kuna changamoto kidogo imetokea dereva hana mafuta anakwepa foleni na trafiki so tuma hata 300k ili tuanze naye.

nkawajibu poa, mie nakuja inabdi nije CRDB kijitonyama kutoa hela so tukutane ubungo.
nkakaa kimya mara mwanapga mara kibao, nkawaambia foleni kubwa benk hapa, mwishowe nkawaambia mbona naona namba zenu zipo hapa jirani na makumbusho. wapi makumbusho wanakodi malory ya tan30? nkacheka, aisee nilitukanwa matusi. mie nkasema sawa .
kwa sababu kila nilsave namba zao, siku nashangaa Msg inaingia jina saved tapel 1.
"Mjukuu wangu ile, dawa ya kukupa utajir...mavi! mavi na..."
nkamjibu siku hizi babu huuzi vyuma chakavu?

Mbwa sana wale

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shieee ero layoni subai. Amekula kwako asee jamaangu
Dah kuna Mmasai mmoja aliwahi kunikuta kistoni (kijiweni) nimechill enzi hizo ndio nipo o'level likizo. Akanikuta pale akaanza kunitangazia dawa zake mara mkuyati, lodwaa mara mkongoraa n.k nikamwambia "ndauwoo ashenale sitaki kitu leo" (rafiki asante sana sitaki kitu leo).

Mara akachomoa dawa fulani akaniambia hii ni kwaajili ya "Ndito" (Wasichana) akaniambia nimpe buku alafu nikanunue baby care ile ndogo akanichanganyia ile dawa na mafuta kisha akaniambia kila nikioga tu nijipake fresh kisha ndito yoyote ninayemtaka nikitupia vocal lazima anase. Yani haruki.

Masai kasepa zake kashanikamua buku yangu nikasogea home nikapiga maji fasta nikajipaka wese fresh lenye dawa kisha nikatoka rodi kupiga misele. Sasa kuna kamanzi flani nilikua nakatamani kitambo siku hiyo nikawa na confidence kinyama kumuona nikamtupia vocal kweli alizingua zingua ila baada ya siku mbili tatu akakubali. Nikajua Masai noma. Siku kapita pale nikampa mrejesho na kumuongezea buku ingine.

Basi nikajaribu bahati kwa Ndito mwingine alikuwa yeye yupo A'level nikaambulia matusi tu. Confidence ikashuka kila nilipotamani kutongoza nikashindwa. Nikajua tu yule masai alinitapeli alicheza tu na akili yangu. Kumbe ile dawa haifanyi kazi ila tu ilisaidia kuni boost confidence.

Siku nyingine anapita ananiuliza kama aniongezee nikamwambia inatosha nilishapata demu na sitaki mwingine. Asijue nilisanuka kuwa alinitapeli.

Mnaoendaga kwa waganga mjue tu wanacheza na psychology zenu wala hawana utaalamu wowote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nipo hapa mkuu wangu. Acha tu haielezeki hilo sakata maana nilikula hasara kubwa mnoooooo.....lile jengo lilikua zuri sana nilijua sio musikiti ni jumba la mufalume
Yule mmasai aliyeuziwa msikiti mkuu pale morogoro mjini kama yuko huku anyooshe mkono atuhadithie ilikuwaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi niliwahi kuuziwa dhahabu miaka ya 2000s kipindi hicho ndo naingia mjini.

Nilitoka kwetu kijijini kuelekea mwanza mjini nilifika stendi nilishuka vizuri tatizo lilianza nilipoanza kukatiza mitaani mbele yangu alitokea jamaa mmoja amechakaa Sana akiwa anaongea lafudhi ya kisukuma aliniambia Kuna wazungu wamepata ajali maeneo ya Geita na yeye alifanikiwa kupata dhahabu kidogo katika ajari ile hivyo alikuja Mwanza mjini kutafuta wateja aliniambia nimsaidie atanipa kiasi kidogo
Sikuwa tayali kuachia utajili fasta nilimuuliza Ni shi ngapi aliniambia nimpe 40k by that time.

Mfukoni nilikua na 10k nilishusha mpaka akakubali akanipa mzigo nikalipa tukaachana.

Baadae nilikuja kucheki mzigo umegeuka mawe daaaah ! Jamaa aliniotea.

Tupia story yako ulivotapeliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na mkiendelea na ushamba shamba wenu, tutaendelea kuwatapeli

Acha kukaa kihasara hasara
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom