Tuliowahi kupambana na vichaa tuelezane ilikuwaje!

k.koo kichaa alinifatilia muda mrefu afu sijui.nikawa navuka barabara kwenda kupanda daladala aisee akanishika ta.ko na kuninga'ng'ania nikajitoa kwa nguvu.ndani ya sekunde moja sikumuona yaani kama aliyeyuka hivi.ghagla namuona kaka mmoja mtanashati (sitadescribe mavazi yake maana mtahusisha na dini za watu bure) nakumbuka alichovaa hadi leo na ilikua kama sikosei 2015 basi yule kaka akaniambia hapa nenda kapande gari haraka huyo kichaa amekupenda
hahhah akasema ukiendelea kuepo maeneo haya atakufata hadi home
aisee nikiikumbuka ile picha naumia sana roho
maana jinsi alivyonishika aisee
Uliskiaa raha eee!
 
Binadamu wabaya sana


Ubarikiwe lakini
Kuna dada mmoja chizi aliletwa kijijini kwetu akitokea Arusha alikuwa ni muhasibu kwenye kampuni moja huko Arusha (ana advance diploma yake). Aliletwa kijijini amefungwa kamba mikono miwili halafu anafungwa kwenye mti kwa ajili ya matibabu.

Akipita shule wanafunzi wanamtania anawakimbiza, wakati mwingine anawarushia mawe. Hata baadhi ya maskani vijana wakimtania huwa anawakimbiza na hata kuwatukana matusi makubwa makubwa.

Mimi nilikuwa tu naskia story zake, ni chizi amesoma na anaongea english safi. Siku moja ghafla huyu hapa amekuja ofisini kwangu (dukani), kuna makabati ya vioo pia. Mimi nikamuomba urafiki kwa kizungu tunaongea mwanzo mwisho, nikamkaribisha ofisini ndani kabisa akakaa kwenye kiti. Nampa kalamu na karatasi ananipa concept za ki-accounts na story nyingi za mambo ya shule shule na maisha.

Nikamuuliza anatumia soda gani nikamuagizia na hata alipoondoka nilimpa business card yangu (kiufupi mimi sikuwahi kumchukulia kama ni chizi, hata hisia/maongezi sikuwahi kumuonyesha kwamba yeye ni chizi). Mara nyingi alikuwa anakuja tunazungumza, tunapiga selfie mpk wanafunzi na vijana pamoja na wanakijiji wakamchukulia kawaida kabisa na ni msomi, wateja walikuwa wakija wananikuta nazungumza nae english safi

Kidogo kidogo akaanza kure-cover, baadae akapona kabisa, namba yangu ya simu kutoka kwenye business card (ameikariri). Pale kijijini anakumbuka kila kitu, mara kwa mara alikuwa ananipigia simu naongea nae, alipona kabisa huwezi kumjua kama ni yeye.

Tangu nipo kijijini mpaka sasa nipo mjini tunawasiliana fresh tu, maisha yame-change kila mtu na maisha yake, tunakumbukana siku 1 moja kwa simu kujuliana hali. (Niliambiwa ukichaa wake ulisababishwa na cheo/maslahi ofisini mfanyakazi mwenzake hakupenda)
 
Nilikua primary,, chizi alinipiga jiwe akanipasua kichwa, mamangu alimchapa vibaya mno,,,
 
Najaribu kuwakumbuka vichaa kadhaa, miaka ya 94 hivi nikiwa shule ya msingi wanginyi kule Lupembe, kulikuwa na kichaa kuna wakati akija shule wanafunzi wanakimbizana na walimu wanajifungia ofisini, na alikuwa anakuja mara kwa mara, nilikuwa namwogopa sana.

Pia miaka ya 98 mjini TUNDUMA alikuwepo chizi anaandika barabarani maneno Mengi ya kiingereza na mengi yao yalikuwa Sahihi .
Sijui alipata masahibu yake.
 
Amefanyiwa ushirikina
Daah! Mada ya Leo imenigusa haswaa wapendwa...mie Nina ofisi yangu yaani duka la vitu mchanganyiko rugha nyepesi 'takataka kuna chizi hapa kijijn kwetu nilimkuta tangu nakuja hadi sasa mashaallh huyo chizi kila siku asubuhi lazima aje hapo ofisini kunisalimu yaani daily!!! Vipi hapo kuna tatizo au nn maana yake??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom