UrbanGentleman
JF-Expert Member
- Jun 19, 2016
- 2,584
- 1,886
Shule ilikua musoma vijijini uko BWASI mbele ya BUKIMA, km 83 toka musoma mjini haikua na walimu kabisa na umeme hakuna ni jeneretor tuu na solar.
Chanzo cha kufukuzwa nilianzisha mgomo uliopelekea kudai ada zetu... Kwa sababu ya kukosa walimu na kuhoji ada zetu zinakwenda wapi kama upatikanaji wa walimu umekua mgumu turudishiwe ela zetu turudi makwetu
Daah head master alikua anaogopwa balaa lakini mzee nilimkazia assemble nikimhoji mbele ya wanafunzi wote kuwa vipi mbna pesa zetu mnatumia kwa kulipana mishahara lakini kutuletea walimu walau tuone mnahangaika imekua ngumu, sasa turudishieni pesa zetu... Kama kutufukuza mtufukuze ila pesa zetu tupewe lasivyo tufikishane mahakamani...nimekunja ndita na wenzangu kama wanne nyuso kavuuu... Mkuu alikua anahaha balaa....daah nimekumbuka mbali sana.